Wednesday, October 17, 2007

MKenya aua mama watoto wake mjini Lynn, Massachusetts

Marehemu Esther Kinyanjui na wanae

DUH! Haya sasa waKenya wako kwenye taarifa ya habari tena hapa Boston. Safari hii huyo jamaa aliyekuwa na mazoea ya kumpiga mama watoto wake kaamua kumtoa roho kabisa! Kamchoma huyo mama kisu zaidi ya mara ishirini!

Mungu ailaze roho yake mahali pema mbinguni. AMEN.

*********************************************************************************
A 28-year-old father was in Lynn District Court Wednesday, charged with the stabbing death of the mother his two children. Patrick Waweru, 28, of Lynn, is charged in connection with the stabbing of Esther Kinyanjui, 31, the mother of his children.

The victim's sister, Margaret Kinyanjui, 27, was also injured in the attack and the family was speaking out at the courthouse. NewsCenter 5's Pam Cross reported that Esther Kinyanjui was hiding inside her sister's apartment at 4 Kingsley Terrace when her estranged boyfriend broke in. He had allegedly made threats to kill in the past.

Kinyanjui was stabbed in the basement apartment with her youngest child nearby. Her sister and mother tried to stop the attack."I tried to hold the knife and I was cut here. Then he got that knife and then ... do that," Ruth Kinyanjui said, making a gesture of a knife being drawn across the throat."

She was the most loving person. She was helping all of us. Myself, my mother, the children. She loved her two children very much. She obviously loved the father of the children and that's why she was always covering for him," Margaret Kinyanjui said.

Family said the pair had a long history of domestic violence dating back until at least 2000. They said Esther would often bail him out after he hurt her, but she moved to Delaware five months ago in an attempt to get away from Waweru. She apparently was lured back, this time to her death.

Waweru pleaded not guilty to murder, kidnapping, two counts of assault and battery with a dangerous weapon and six counts of armed assault in a dwelling and home invasion. He was ordered held without bail and sent to Bridgewater State Hospital for observation.

6 comments:

Kaka Poli said...

Pole kwa huyo dada na familia yake jamani!!

By the way (naomba kiswahili cha maneno hayo), Da Chemi hujambo?

Anonymous said...

Ni msiba wa kutisha sana ila ukiangalia kwa makini utaona kuwa chanzo ni huyo mama kuwa na ama mme mwingine au kutaka kumwacha huyo mme wake wa mwanzo.
Hapa marekani ndoa nyingi za waafrica zinavunjika sana.Hii ni baada ya wa kina mama kujifanya wanakuwa na washauri kuhusu mambo ya ndoa na kujifanya wanajua sheria za Marekani sana.
Pole na msiba

NDAKI GOMBERA said...

Inasikitisha sana hiyo habari.Mwenyezi Munu aiweke roho yake mahali pema peponi,amina.

DA CHEMi,jana tumeondokewa na zaidi ya mwanamuziki kutoka Afrika kusini.Lucky Dube ameuawa kwa kupigwa Risasi alhamisi.

Inasikitisha sana.Kama alivyosema mwenyewe kwenye moja ya wimbo wake.Unaweza kuua manabii wa raggae lakini KATU huwezi kuuwa raggae kwani ina nguvu.

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Dube,mwanaharakati na mwanamuziki,mwanahalisi wa Afrika.

Rest in peace.

maelezo ya kifo chake
http://www.mg.co.za/articlePage.aspx?articleid=322400&area=/breaking_news/breaking_news__national/

Anonymous said...

Hapana,hakuna ruhusa ya kumpiga mkewe ata mpaka afe. Na wewe anonymous unaonekana unaelewa hali ilivyo ukiwapatia wanawake sababu ya ndoa zao kuvunjika. Ndoa zote zinahitaji kazi ya watu wawili, uvumilivu, upendo, na kusameheana. Na nani wakusema eti wanaume pia hawana kosa lolote?

Anonymous said...

ananymous 6:20pm ,kama mwanamke anacheat inamaana umemkosea sana,si angemwacha tu,mpaka umuue?hiyo si sawa,je ni haki ,wanawake wawe wavumilivu tu peke yao?

Kazungu Samuel said...

Mimi ni shabiki mkubwa wa hii blog Da Chemi.ninaishi jijini Mombasa,Kenya sawia nikiwa mzaliwa wa nchi hii.Kwa kweli hii habari ya huyu mama kuuawa na huyo bwanake wa migogoro ya miaka mingi imekuwa gumzo kubwa hapa nchini Kenya.Inasikithisa jinsi alivyokumbana na kifo hicho kikatili.Hata hivyo mimi kama mkenya,ninataka kuwaeleza wana blog wenzangu kuhusu mambo kadhaa ambayo wanapasa kujua kuhusu wanawake wa Kenya wanapopata fedha na uwezo wa kujisimamia kimaisha.

Kama mchangiaji mmoja alivyosema,hili lazima litakuwa ni suala la ufuska na kutoaminiana ndiko kulikoleta haya yote.

Wanawake hapa nchini Kenya,tofauti na Tanzania na hata labda Uganda wakishapata fedha hasa kupitia labda juhudi za waume zao,wanawake hawa huruka kichwa na kuanza kujiona wao ni bora kuliko hata waume zao.Tumewahi kuwaona wanawake wenye fedha zao na ambao wamejistawisha sana kimaisha jinsi wanavyowadharau tena waziwazi wanaume wanaokutana nao njiani.Ningependa kusema au kusifu wanawake wa nchi hizi jirani kwa kukumbuka nyuma walikotoka hata wanapopata uwezo na kupiga hatua kubwa kimaisha.

Kisa hiki kiliripotiwa na vyombo vya kimataifa kwa vile kilitendeka katika taifa kubwa kama Marekani lakini Da Chemi ningetaka kukuambia tu kuwa visa hivi hutokea hata katika familia za wakenya matajiri hapa Kenya.Na ajabu visa hivi vinafanyika katika mitaa ya mabwenyenye.Je hili si suala la fedha kupita watu akili.Halafu Da Chemi mimi niko na blog yangu www.mhimili.blogspot.com lakini ninashida ya kuload picha(Yaani sijajua picha zinawekewa wapi).Tafadhali nisaidie.Otherwise blog yako ni nzuri na nimepita archives zako zote.

Ahsante ni mimi Kazungu Samuel kutoka Mombasa Kenya.Email yangu ni kazungu9@gmail.com