Saturday, October 13, 2007

Mwandishi wa Habari Nellie Kidela amefariki dunia.

Leo nimepata habari kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa siku nyingi wa Radio Tanzania Dar es Salaam, Nellie Kidela, amefariki dunia.

Dada Nelly ni moja wa waanzilishi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, TAMWA. Mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwake.

Taarifa niliyonayo ni kuwa Dada Nellie alifariki siku ya Jumatatu tarehe nane Oktoba na alizikwa, jumatano tarehe 10 Oktoba katika makaburi ya Kinondoni. Alikuwa ameugua ugonjwa wa kansa siku nyingi. Na miaka ya nyuma aliwahi kupata matibabu hapa Boston.

Dada Nellie alikuwa mama yake mzazi na Nuru Mkeremi wa hapa Boston, Massachusetts.

Mungu ailaze roho take mahali pema mbinguni. AMEN.

3 comments:

Anonymous said...

Poleni kwa msiba wafiwa...

JAMANI JAMANI>> Christopher Columbus wetu AKA Vasco Da Gama AKA JK ameondoka (tena!!!!) nchini leo kwenda kuivumbua dunia safari hii ameenda Italy na Vatican ambako atakutana na Pope Bennedict... Cjui bado ile role yake ya uwaziri wa mambo ya nchi za nje bdo haijamtoka au labda ana alergy na TZ yaani amekuja kwa muda mfupi ameondoka baada ya kuivunja rekodi yake mwenyewe ya RAIS WA TANZANIA ALIYEKAA NJE YA NCHI YAKE KWA ZAIDI YA YA WIKI 3 SAFARI AMEPATA KA-TRIP CHA WIKI 1 NA Cku 1 hivi ziara zake zinatusaidia nini cc wavuja jasho na Walipa Kodi!!!???

Anonymous said...

Maskini! Nakumbuka sana kumsikia Nelly Kidela akitangaza RTD. Mola ailaze roho yake mahali pema peponi. AMIN.

Anonymous said...

Oh pole sana dada Nuru,Mama kidela alikuwa mama yetu na jirani yetu hapo Upanga mtaa wa Mfaume,tunamkumbuka sana,na wote tulishtushwa na kusikitika kwa kuondoka kwake but yote ni mambo ya Mwenyezi Mungu,

Mungu azidi kuwatia nguvu

Jirani