Monday, October 22, 2007

Panda Teksi za Madereva unaowafahamu Bongo

Nimepata hii habari kwa e-mail. Ilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Dar es Salaam.

********************************************************************

Dear all,

Jana I happen to come across a very sad event:

Nilikuwa narudi nyumbani around saa moja jioni kwa kutumia njia ya Chuo Kikuu, kuna njia ya mkato inayopita changanyikeni na kutokea bahama mama. Kuna bonde na daraja na si sehemu salama sana wakati wa usiku.

Nilisimamishwa na dada mmoja aliyeonekana kuchanganyikiwa akiwa ameshika viatu mkononi. Kwa sababu nilikuwa mwenyewe, nilimpita kwanza then nikasimama ili nione kama kuna watu wengine. Yule dada alikuja akiwa analia akasema ameibiwa kila kitu na dereva taxi ambae alimtisha kwa kisu na kumsukuma nje ya gari na dereva kuondoka kwa kasi. Lakini pia, dada huyo alikuwa na mwenzake kwenye gari (mdada pia) ambae alishindwa kutoka na dereva huyo aliondoka nae. Wakina dada hao walikodi taxi hiyo kutokea Msasani wakielekea Ilala.

Nilimsaidia huyo dada hadi Kimara police post na ku-report. Nilimsaidia kufanya mawasiliano na kaka yake na kuwaacha.

Mpaka saa 5 usiku jana walikuwa hawafanikiwa kumpata huyo dada mwingine. Leo asubuhi nimepata habari kuwa, yule dada mwingine alipatikana usiku wa kama saa sita. Alikuwa na hali mbaya sana, kwa maelezo yake..aliingiliwa na watu 9 kimwili. Kesi ipo polisi na kijana mmoja amekamatwa.

This is very sad..sad indeed. Jamani wandugu�.tuwe makini sana na Taxi�

GJ

1 comment:

Anonymous said...

Habari ya kusikitisha hii.

"kwasababu nilikuwa mwenyewe" maaan yake nini?

au "kijana bado amekamatwa"

hivi vishwaili vya wapi hivi?

Hivi ni kweli Tanzania mpaka leo hii bado kuna watu wanasema "mbu nyingi" "hizi ni kuku zangu"