Saturday, December 15, 2007

Mambo yajirudia baada ya miaka 100!



Je, kuna uhusiano gani kati ya marais wa Marekani, Abraham Lincoln na Jack Kennedy? Kwanza wote waliuliwa wakiwa rais.

Zaidi ya hiyo kuna maajabu pia.

- Aliyemwua rais Lincoln, John Wilkes Booth alizaliwa 1839. Aliyemwua rais Kennedy, Lee Harvey Oswald, alizaliwa 1939.


- Aliyekuwa rais baada ya kifo cha rais Lincoln ni Andrew Johnson. Alizaliwa 1808. Aliyekuwa rais baada ya kifo cha rais Kennedy ni Lyndon Johnson. Alizaliwa 1908.

- Aliyekuwa karani wa rais Lincloln alikuwa anaitwa Kennedy. Aliyekuwa karani wa rais Kennedy alikuwa anaitwa Evelyn Lincoln.

- Rais Lincoln alichaguliwa kuwa rais 1860. Rais Kennedy alichaguliwa 1960.

- Wote wawili walisoma sheria, waliweza kuandika vizuri, walikuwa na matatizo ya macho na magonjwa ya kurithi. Wote walikuwa wanajeshi. Wote walipigwa risasi kichwani siku ya Ijumaa.
- Wote walikuwa hawaogopi kifo na pia walikuwa hawapendi mabodigadi. Inadaiwa Rais Lincoln alisema, kama mtu atataka kuniua sitaweza kumzuia." Na rais Kennedy alisema, "Kama mtu atataka kunipiga risasi kutoak dirishani sitaweza kumzuia."

- Rais Kennedy aliuliuwa akiwa ndani ya gari iliyotengenezwa na kampuni ya Ford. Rais Lincoln aliuliwa akiwa anatazama mchezo wa kuigiza ndani ya Ford Theatre.

6 comments:

Anonymous said...

Samahani, Nimeangalia profile yako lakini sikuweza kufahamu kama una mume au uko single!
Unaweza kunijulisha kupitia hapa?

Anonymous said...

wewe huachi, ushafanya infringe copyright za watu, bila kuandika vielelezo wa ulikoitoa hii story, au ndio tafsiri make it yours sis.

Chemi Che-Mponda said...

Actually nimetoa hizi details kutoka sehemu mbalimbali na kutafsiri. Hata hivyo hizi ni historical facts katika public domain. Asante.

Anonymous said...

Chemi,hiyo commet ya huyo rafiki hapo juu isikuvunje moyo.Mimi napenda sana habari zako huwa ni kali na za kusisimua sana.Mimi ni jirani yako na siku ya sumaye tulikuwa wote ulikaa kiti cha 7 toka nilipokaa mimi na nilikuwa bize kutafuta vijiko.Hhahahahhaah

afrikaoye said...

hee! vipi tena jamani mbona watu wanauliza kama msimamizi wa ukurasa (chemi) ana mume au la. hii inahusinaje na anayoyasema au kutoa kama mchango wake kwenye mtandao?

na kama unauliza kwa nia nzuri kwa nini unajificha kama 'anonymous'? ni kweli kwamba kuuliza si ujinga. lakini uliza kinagaubaga ili akujue we nani.

usiogope.

na huyu anonymous mwingine anayesemea mambo ya copyright infringement mbona na yeye kajichimbia? kama chemi kafanya kosa kuandika/kutafsiri basi mwambie wazi wazi. usifanye mambo kinyemela.

kujifichaficha kunafanya muonekane kama hampendi, mna maana nyingine zaidi ya ile mnayoisema au mna nia mbaya.

hayo maoni yenu yamenifanya niwe mdadisi kidogo.

Anonymous said...

Wewe anony, Chemi ni mzaee na Kibonge(kabati). Hiyo picha hapo isikuingize mkenge mdogo wangu, nenda kwenu Chalambe katafute dogodogo mwenzako.