Monday, December 03, 2007

Rais wa Sudan amsamehe Mwalimu Gibbons!



UPDATE 1:29PM Eastern - Mwalimu Gibbons ameondoka Sudan, kurejea Uingereza.
****************************************************************************
Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir, amemsamehe mwalimu mwingereza Gillian Gibbons (54)! Mwalimu Gibbons alifungwa Sudan wiki iliyopita baada ya kuruhusu darasa lake la wanafunzi wa darasa la pili kuita mdoli wa darasa, Mohamed.

Wasudan walisema kuwa ilikuwa kashfa kwa waislamu. Wengine walidai auliwe. Baada ya mwalimu huyo kufungwa wabunge wawili waislamu kutoka Uingereza walienda Sudan kuongea na rais Al-Bashir. Msamaha huo umetolewa leo asubuhi.

Mwalimu Gibbons naye ameomba msamaha kwa watu wa Sudan na kusema kuwa hakuwa na nia ya kuwakashifu. Hivi sasa yuko chini ya ulinzi ya waingereza ubalozini mwao kwa usalama wake. Ataondoka kwenda Uingereza hivi karibuni.

Wakati huo huo, Serikali ya Sudan bado inaendelea kuua waDinka (waafrika) huko Darfur.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/WORLD/africa/12/03/sudan.teacher/index.html

http://www.thestar.com/comment/article/281848

http://www.news.com.au/heraldsun/story/0,21985,22865462-663,00.html

6 comments:

Anonymous said...

Angemsamehe mara moja siyo mpaka alitumikia sentensi yake. Angewanyazisha watu wake mara moja na kuwaambia ni upuuzi. Sasa watu wanataka kumwua huyo mama. Hivi wasudani ni waislamu kukilo waislamu wengine.

Anonymous said...

If this faculty member, Sarah, Khawad, was that offended why did they not approach Gibbons and let her know that her actions was offense to them instead of inciting violence among the whole country. I feel this faculty member was so jealous of Gibbons having a very positive impact on the children that this was a deliberate act to get her out of Sudan. That faculty member should not be teaching these children as they themselves are still a child

Anonymous said...

Huyo Raisi wa Sudan anatakiwa ashitakiwe kwa kumwonea huyo mama Gibbons

Kwani Jina "Mohamed" lina Copyright? Kiasi kuwa mtu hawezi ita nguruwe wake Mohamed akitaka?

Jina kama halina Copyright huwezi mshitaki mtu kuita Doli lake au choo chake Mohamed.

Wakitaka walisajili hilo jina liwe na Copyright kuwa huruhusiwi kulitumia isipokuwa kwa matumizi ya kidini kama wanataka.

Huo msamaha mimi siukubali raisi ashitakiwe na sudani imlipe fidia huyo mama kwa kumdhalisha na kumsababishia mental torture.

Anonymous said...

Dada Chemi wacha propoganda.Mbona hutuletei Askofu wa Sicily aliyelalamika kwamba tangazo la biashara la Red Bull la 3 wise men linamdhalilisha Yesu Kristo na familia yake.Kilichotokea televisheni zimeondoa tangazo hilo kwa heshima ya Yesu Kristo.
Pili kuhusu hao wa Darfur unawaita wadinka(waafrika) wacha kutoa sweeping statements bila kuwa na uhakika.Darfur wanaishi wasudan ambao ni waafrika kama sehemu yeyote ya Sudan.Kuwagawanya kwa kuwaita wadinka ni ujinga uliokithiri kwani wanaoishi Darfur sio wadinka peke yao.Uganda kaskazini wanauana nao wanauliwa na wazungu???Fanya utafiti kabla ya kusema chochote.Kwani Darfur kuna makundi yanayopingana ambayo yanapigana yenyewe kwa yenyewe kwa upande mmoja na kupigana na Serikali kwa upande mwingine.Kuolewa na padri wa kizungu isiwe sababu ya kuendekeza propoganda.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 10:21qam, hiyi habari ya Red Bull ndo kwanza nimesikia. nitaitafuta.

Anonymous said...

Dada Chemi advert ya Red Bull na kasheshe iliyozua huko Italy bado hujaipata??Au huyatafuta.Nenda reuters.co.uk.Kuna advert ya Madona pia ilipigwa marufuku kwa kukashifu ukristo.Zote hizi hazipewi kipaumbele na vyombo vya habari kwa kuwa hazihusu uislamu na islamphobia yenu.Red Bull ni Dec 3.