Wednesday, December 12, 2007

Nani Anakumbuka


Nani anakumbuka sinema za:

Muhogo Mchungu (Mzee Rashid Mfaume Kawawa)

Fimbo ya Mnyonge

YombaYomba


Je, hizi sinema zinapatikana kweli? Kanda ziko wapi maana ni sinema muhimu kwa nchi yetu. Zisipotee.

Nani anakumbuka walioigiza ni akina nani na zilihusu nini?

Hiyo ya Muhogo Mchungu ulifichwa enzi za Mwalimu kwa vile Mzee Kawawa aliigiza kama mwizi.

4 comments:

Anonymous said...

Kumbe Mzee Kawawa alikuwa bomba hivyo.

Anonymous said...

Pia aliigiza sinema moja ya Dawa ya Mapenzi.

Kulikuwepo na sinema nyingine ya Charo Afika Dar es Salaam.

Najua nakala walikuwa nazo katika Idara ya Maendeleo ya Jamii (Department of Community Development).

Isiwe zilichomwa moto! Nyaraka nyingi za kikoloni zilichomwa mara baada ya uhuru (kulipa kisasi - kama nyaraka za wilaya na mikoa ambazo halikupekwa Dar zitunzwe).

Niliwahi kuwauliza akina British Council endapo wanazo nakala. Lakini sikupata jibu.

Chemi Che-Mponda said...

Kama hizo kanda zilichomwa moto basi ni HASARA kwa taifa letu. Hizo ni sehemu ya historia yetu.

Nakumbuka sana walichoma moto vitabu na vitu vingine eti vya wakoloni! Eti kuondoa KASUMBA.

Na kama hizo kanda zipo zipelekwe Restoration zikahifadhiwe na kuwekwa kwenye DVD.

John Mwaipopo said...

Mengi huwa yanasemwa kuhusu filamu za huyu mzee mojawapo likiwa zilifichwa kwa kuwa alikuwa kiongozi, eti isingekuwa vema kiongozi kuonwa-onwa kila uchao.

Leo umeleta jambo jema. hivi kwa nini tusiwaulize iliyokuwa sijui mamlaka ya filamu tanzania. Zitakuwepo somewhere tu otherwise some guy must be brought to task.

Hii ndio shida yetu: badala ya kuviona vitu kama hivi kuwa fahari tunaona vya kijinga na badala ya kuona vitu vya kijinga ujinga tunaona vya fahari.