Monday, December 31, 2007

Sinema ya Real Men Cry

Amanda Peet
Mark Ruffalo & Ethan Hawke


Wiki iliyopita niliitwa kuwa extra katika sinema ya, "Real Mean Cry". Inahusu wanaume wawili walivyokuwa marafiki tokea walivyo wadogo huko South Boston. Baadaye wote wanafungwa gerezani.

Sasa scene enyewe ilipigwa kwenye gereza la Billerica House of Corrections. Ambayo ni gereza la medium security. Walikuwa na ulinzi mkali na tulichunguzwa hata kabla ya kufika huko (background check). Kuingia unapita kwenye X-ray na kusachiwa kama unapanda kwenye ndege. Ilibidi tuache simu, kamera na vifaa vingine mlangoni. Halafu kila ukitembea hatua kama ishirini kuna mlango ambayo inabidi ufunguliwe. Kulikuwa hakuna kwenda chooni bila kusindikizwa na mlinzi wa gereza. Halafu tulipewa ID za kuvaa mkononi. Kwa kweli si rahisi mtu kutoka huko.

Kuna waigizaji wa kiume walivalishwa magwanda ya wafungwa. Utadhani ni wafungwa kweli kweli. Ila wamevaa hiyo ID mkononi. Sasa kuna jamaa mzungu alienda chooni. Alivyokuwa huko anasema, mlinzi alimtania na kusema, "Mkamate huyo, mfungwa katoroka!" Mzungu anasema alijisikia vibaya kweli.

Nilikuwa na waigizaji wengine wawili wa kike. Na tulisindikizwa eneo la kusubiri. Njiani tulipita wafungwa wa kweli. DOH! Mbona walianza kupiga makelele kama ngedere! Tulivyowapungia ndo kabisa waliigiwa na kiwewe! Naona walikuwa hawajaona wanawake muda mrefu.

Nilivyofika kwenye seti walisema kwanza nitaigiza mlinzi wa gereza. Nilimcheki mlinzi wa kike wa kweli aliyekuwepo zamu hapo. Alikuwa ni buchi lesbo hasa! Nikasema mungu wangu nitakoma. Lakini mimi ni msanii wakitaka niigize hivyo itabidi. Kwa bahati walinibadilisha na walisema nitakuwa mgeni namtembelea mfungwa. Cha kuchekesha, walikuwa na upungufu wa wanaume weusi waigizaji. Walimchukua jamaa aliyekuwa ana shughulikia chakula (caterer) na kumvisha nguo za mfungwa. Ndo nilifanya scene na huyo. Tulivyo maliza scene jamaa alibadilisha nguo na kuendelea na shughuli zake za catering.

Waliniweka karibu na Amanda Peet. Nilicheka kweli kimya kimya maana kuna wakati madirector (waongozaji) walinigombania. Moja aliniweka sehemu fulani kukaa, mwingine alinihamisha. Nilivyohamishwa jamaa aliingia seti kwa haraka na kumfokea na kumgombeza yule mwingine eiti kwa nini alinihamisha! Loh! Nikasema kumbe watu wanaanza kuni-notice.

Sinema zingine ambazo niliitwa mwaka huu lakini nilishindwa kwenda ni : The Great Debaters starring Denzel Washington (nilikuwa Bongo) na The Lonely Maiden starring Morgan Freeman ( ilikuwa ni short notice).

Mwakani sinema kubwa kama nane zinatarajiwa kupigwa hapa Boston nazo ni zifuatazo,( hiyo ya Shutter Island ya Scorsese ndo itakuwa kiboko ya mwaka 2008):


From Boston Globe:
*******************
"The Ghosts of Girlfriends Past"

When: Production crews are already here, setting up shop in South Boston's Seaport District.Director: Mark WatersStars: Jennifer Garner and Matthew McConaugheyStory: While attending his younger brother's wedding, a bachelor is haunted by the ghost of - you guessed it - his girlfriends past.Release date: February 2009

*******************
"Shutter Island"

When: It's hard to say, but location scouts have been scouring the area looking for suitable locales that could sub for a 1950s hospital for the criminally insane.Director: Martin ScorseseStars: Leonardo DiCaprio, Michelle Williams, Ben Kingsley, and Mark RuffaloStory: A drama based on the Dennis Lehane novel of the same name. US Marshal Teddy Daniels is investigating the disappearance of an escaped murderer who's believed to be hiding on Shutter Island.Release date: 2009
*******************
"The Surrogates"

When: Scouts already have picked a few locations and producers are telling local crews to be ready to go by the spring.Director: Jonathan MostowStars: Bruce Willis and Michael Jai WhiteStory: Based on the popular graphic novels of Robert Venditti and Brett Weldele, the futuristic action flick imagines a world where humans live in isolation but interact through surrogate robots. A cop, played by Willis, investigates the murder of surrogates.Release date: 2010
*******************
"Against All Enemies"

When: Word is scouts have been in town, but it's unknown yet when or where filming will take place.Director: Robert RedfordStars: Bruce Willis (Sean Penn and Vince Vaughn were initially attached, but have reportedly dropped out)Story: Based on the memoir by former counterterrorism adviser Richard Clarke, the story centers on the government's failure to heed warnings about a planned attack on the United States.Release date: 2008

*******************
"Bride Wars"


When: Word is Kate Hudson, who stars and produces, had such a good time in Boston shooting "My Best Friend's Girl" last summer that she wants to return. Timetable unknown.Director: Gary WinickStars: Kate Hudson and Anne HathawayStory: A comedy about best friends who become rivals when they schedule their weddings for the same day.

*******************
"The Town"



When: "The Departed" producer Graham King has scouted here, but the writers' strike may hold things up.Director: Adrian LyneStars: UnknownStory: Based on Chuck Hogan's award-winning novel "Prince of Thieves" about a band of robbers who are hunted in Boston by a tenacious FBI agent and a woman who could destroy them.Release date: 2008
*******************
"The Fighter"

When: With any luck, the production, which could end up being the largest ever filmed in the state, is expected to begin filming in Lowell next fall.Director: Darren AronofskyStars: Mark Wahlberg and Brad Pitt, who signed after Matt Damon dropped outStory: A biopic based on the life of former champ "Irish" Micky Ward and the brother who helped train him.Scheduled release: 2009
*******************

"Hickory Nation"

When: Filming on the North Shore could begin as soon as next month.Director: Rebecca Cook, who'll also get a writing and producing credit.Stars: Aimee TeegardenStory: A drama about life after a mysterious hit-and-run in a small Maine town.Release date: 2009

14 comments:

Anonymous said...

Tatizo unajisifu sana, halafu hatuoni hizo cinema za maana, hem ngoja usifiwe, umekuwa kama muhaya loh....

Anonymous said...

We anony wa 5:29pm umeigiza katika sinema ngapi wewe. Acha wivu.

Anonymous said...

Hongera Dada Chemi! Endelea na moyo huo. Siku moja utapata 'role' kubwa katika sinema ya Hollywood. Kila kitu kina mwanzo.

Anonymous said...

Chemi, nami natoa pongezi kwako na si pongezi za kinafiki. Ni wabongo wangapi ambao wameshiriki sinema za Hollywood, hata kama ni extra au grip? Ni wachache. Nasema hongera maana nyie ndo mnatufungulia mlango. Najua watakaokuja nyuma hawatawatambua. Yupo moja hafucasti kwenye series lakini wala hajitambui kama mbongo siku hizi. Wala usijali comments zenye wivu!

Mungu akubariki katika mwaka mpya.

Anonymous said...

Chemi
Heri ya Mwaka mpya. Hongera, naona unaelekea kwenye umaarufu sasa. Utuletee nasi hizo sinema tuzione Bongo. Ni hatua nzuri, hongera sana.

Nisaidie huu msamiati ulotumia: buchi lesbo ni nini?

Chemi Che-Mponda said...

Mbula,

Asante kwa sala. Heri ya mwaka mpya na wewe.

'buchi lesbo' ni wale shoga wanaojifanya wanaume. Wanavaa kiume na matendo yao ni ya kiume na kwenye shughuli zao za ulesbo wanachukua nafasi ya mwanaume.

Anonymous said...

Sis Chemi

Mi sisemi mengi just Prima!! Keep the ball rolling dear.
Kazi nzuri mara nyingi ni matokeo ya msingi imara

Koleza game

Anonymous said...

kuna mambo mengine ni aibu kweli kujihadisia mwenyewe chemi,umeandika wewe lakini msomaji unasikia aibu.

Anonymous said...

We fala anony wa 6:34am umelazimika kusoma blogu ya Da' Chemi? Loh!

Anonymous said...

Majisifi yamezidi dada.Kama kuwa extra kunaleta majisifu namna hii,sijui itakuwaje siku utapokuwa mshiriki kamili kwenye filamu.Lakini najua nyie wakunyumba ni watu wa ujiko.

Anonymous said...

Mbona mbongo akitokea kwenye sinema ya Marekani inakuwa ni habari kubwa Tanzania. Utasikia inatajwa kwenye vyombo vya habari oh fulani atakuwa kwenye BET au nini na nini. Hakuna cha ajabu hapa. Dada Chemi anawaelezea jinsi ya kuingia huko Hollywood kama hamtaki kusikia basi. Wanataka kuingi huko wanasoma habari zaka kwa makini.

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wadau wote mliotoa maoni hapa. Mungu ni mwema na nashukuru kuwa nimeweza kushiriki sinema za Hollywood hata kama ni kama 'Extra'. Hao wasanii wa Hollywood wengi walipata mwanzo wao kama Extra. Ukiangalia shows za historia za baadhi ya waigizaji utaona wanaonyeshwa wakiwa Extra.

Ningependa kuona waTanzania wengi zaidi wakipata nafasi za kushiriki sinema za Hollywood. Kama nilivyowahi kusema, nina chukia sana kuona MSouth Africa au MNigeria anaigiza kama MTanzania au Mganda. Wenzetu wa Kenya na Nigeria wanapiga hatua Hollywood hivyo kwa nini na sisi tusichukue nafasi yetu?

Anonymous said...

Da chemi acha, mbona katika hiyo picha hakuna jina lako?! kama kweli umeshiriki, mbona haujatajwa katika walioshiriki hata wadogo wadogo?mmh....tutaaminije?
http://www.imdb.com/title/tt1133991/..hakuna katika hiyo acha kujisifu dada fanya kazi utasifiwa siku ikifika

Chemi Che-Mponda said...

Sinema bado haijatoka. Imdb wataendelea kui-update. Jina ikitoka pembeni wataweka (uncredited). Usiwe na wasi wasi niko kwenye scene ambayo Amanda Peet anamtembelea Ethan Hawke gerezani. Tena nimekaa mbele ya Amanda. Sasa sijui kama itakuwa kwenye final cut. Wanashuti sana halafu wana-edit sana.