Monday, December 17, 2007

Mtangazaji Maarufu Akamatwa polisi!


Alycia Lane (35), ni mtangazaji maarufu wa Philadelphia, CBS, Channel 3. Pamoja na urembo wake ni mkorofi. Amekamtwa na polisi mjini New York kwa madai kuwa alimpiga ngumi usoni polisi wa kike na kumwita msenge.
Chanzo cha ugomvi ni hivi, alikuwa kwenye teksi na rafiki yake wa kiume walikuwa nyuma ya gari ya polisi isiyoandikwa. Hiyo gari ya polisi ulikuwa unaenda pole pole na hasiri ziliwapanda waliokuwa ndani ya teksi.

Leo mahakamani Bi Lane alikana mashitaka.
Huyo dada ni mkorofi kweli kweli. Mwezi Mei, alituma picha za yeye akiwa amevaa bikini kwa mtangazaji Rich Eisen, wa NFL network. Eisen kaoa. Mke wa Eisen aliziona na kamtumia Lane ujumbe mkali na kuwaibisha. Lane alisema kuwa alizituma kwa huyo bwana kama utani.
Huyo Bi Lane anaweza kufukuzwa kazi kwa vile CBS watasema anachafua jina lao na anakosa la jinai. Ikitokea msiwe na wasiwasi maana atapata donge nono. Ataenda kwenye Talk Shows kama Geraldo, na Jerry Springer. Pia msishangae ukiona wanatengeza sinema juu ya Ukoforofi wake, au anakubali kupiga picha kwenye gazeti la wanaume, Playboy kwa dola milioni moja. Watu wanadai watakatifu lakini wanapenda mambo kama hayo.

Kwa habari zaidi soma:

2 comments:

Anonymous said...

Mbona siyo mrembo? Kwa sura na umbile lake huyu hawezi kunifanya "nimsukie mkakati" hata siku moja.

Anonymous said...

LOL! umenichekesha kwa kutafsiri "dyke bitch" kumaanisha "msenge" kwa kiswahili. Nadhani hakuna neno lingine bora kutimiwa kutafsiri hilo tusi la kiMarekani.

(Kutoka mkenya fulani anaoishi ng'ambo)