Wednesday, December 05, 2007

Vichaa waongezeka Dar





















Nimesoma habari kwenye ippmedia.com kuwa vichaa wameongezeka mjini Dar es Salaam. Lazima wataongezeka kwa jinsi maisha yalivyobadilika Tanzania. Tamaa ya vitu pia unafanya watu warukwe na akili. Maisha magumu na ukosefu wa fedha unachangia.

Na wanawake pia wanakuwa kichaa. Juzi nilisoma habari ya mama moja aliyelala barabarani huko anaomba wanaume wafanye naye ngono. Mwingine zilifyatuka baada ya kuwatopeza mume wake na mtoto. Mwingine alitembea uchi Kimara hadi Ubungo alipokamatwa.

Nilipokuwa nasoma Zanaki kuna kichaa alikuwa na mchezo wa kukaa karibu na geti na kuonyesha wasichana ume wake. Huyo alikuwa anavaa nguo safi, asingekuwa anafanya maajabu usingejua ni kichaa. Kulikuwa na jamaa moja alikuwa anajifunga shuka tu na kusimama kwenye kona ya Morogoro Road na United Nations. Kazi yake kutazama wanafunzi. Watu walisema zilimfyatuka akibukua mtihani wa Form 6!
Pia watu kupoteza imani na waganga wa kienyeji na idadi yao kupungua inachangia. Waganaga gao walichangia sana kupunguza idadi ya watu wenye ugonjwa wa akili, maana tiba yao mara nyingi ni 'psychological'.

Kuna haja ya kuongezeka kwa tiba ya psychiatric, huko Tanzania.

***********************************************************************

Wenye matatizo ya akili Jijini Dar waongezeka


2007-12-05

Watu 28,900 mkoani Dar es Salaam, wameugua ugonjwa wa akili mwaka jana. Mratibu wa Afya Wilayani Temeke, Bi. Mary Mgaya ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari. Akasema takwimu hizo na zinahusu wagonjwa waliofikishwa katika vituo mbalimbali vya afya Jijini.


``Mwaka 2000, wagonjwa 6,000 waliugua ugonjwa huu wa akili... Hawa ni wale waliofikishwa katika vituo vya afya na kupatiwa matibabu,``akasema. Kuhusu siku ya wagonjwa wa akili itakayoadhimishwa leo Jijini, Katibu Mkuu wa Chama cha Afya ya Akili, ?Dk. Scolastica Ndonde amesema sikukuu hiyo inafanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke.

Akasema ujumbe wa mwaka huu ni``Afya ya akili na mabadiliko:Mwingiliano wa tamaduni, imani, maadili, desturi na tofauti za kijamii,``. Akasema matibabu ya ugonjwa huo yanahitaji mawasiliano mazuri katika jamii.

Akakemea tabia ya watu kuwafunga kwa kutumia kamba wagonjwa wa akili kwani hiyo ni kutowatendea haki. Aidha, akasema Watanzania wamekuwa wakikimbia kwa waganga ambapo wanaambiwa kuwa wagonjwa hao wamelogwa ama wamepagawa. Akasema jambo hilo limekuwa likiwafanya wagonjwa kuzidi kuumwa.

Akawataka kuwawahisha hospitali wagonjwa hao ili waweze kupatiwa matibabu yaliyosahihi kwa ajili ya afya zao. Akasema baadhi ya watumishi katika sekta ya afya wamekuwa hawasimamiii huduma za wagonjwa wa akili kwa namna inavyotakiwa.

Akasema wengine wanashindwa kufanya maamuzi mazuri kuhusu tiba ya wagonjwa wa akili kutokana na fikra zao juu ya umuhimu wa huduma hizo. ``Wamaweza kujua wajibu wao lakini mazoea yao na tabia walizozizoea zinawafanya washindwe kutimiza majukumu yao vizuri,``akasema.

5 comments:

Anonymous said...

Kutokana na uzoefu nilionao kwa hivi sasa hususani suala zima la kuongezeka kwa vichaa mkoani Dar mi naona ifikie hatua serikali ikiri ya kwamba kuna baadhi ya huduma za msingi haiwezi kuzitoa moja kwa moja kwa wananchi wake na badala yake iyaombe mashirika mbalimbali yakiwemo ya kidini ili yaweze kusaidia katika suala zima la afya. Hivi karibuni nilipata bahati ya kutembelea kijiji kimoja mkoani Kigoma katika wilaya ya Kasulu kiitwacho Marumba. Kwa kweli nilishangaa kuona jinsi vichaa wanavyopewa huduma nzuri na za uhakika na shirika moja la kidini liitwalo Brothers of Charity (Kaka wa Upendo), lenye makao yake makuu nchini Italia, Roma na Ghent Ubelgiji. Nilishangaa kuonyeshwa mtu mmoja ambaye inasemekana alikuwa akizurula ovyo katika mji wa Kigoma ujiji lakini baada ya kupelekwa kule na kupewa matibabu alipona kabisa nakujikuta akirudi salama salmini kwenye familia yake ambayo hapo awali ilikuwa imemtenga. Nilivyodadisi gharama za dawa zinazotolewa ni ndogo kabisa ikilinganishwa na gharama halisi za dawa zenyewe, kwani baadhi ya watu ambao kipato chao ni kidogo hutibiwa bure bila hata ya kutoa senti hata moja. Kwa kifupi tu ningeiomba serikali iyaangalie mashirika ya namna hii na iyasaidie kwa namna moja ama nyingine katika kuboresha mazingira ya kazi zake ambazo zina mchango mkubwa sana katika nguvu kazi ya taifa. Serikali yaweza kushirikiana na mashirika kama haya katika hospitali zake za mkoa katika vitengo vya watu wenye matatizo ya akili na kwa hakika hali hii yaweza kubadilika. Tusibweteke kwa kusubiri bali tuangalie hali halisi jinsi ilivyo na tutende. Naamini wachache watakaopata muda wa kusoma maoni yangu haya wanaweza kufanya utafiti zaidi juu ya hili shirika ili kama wana jamaa zao wenye matatizo kama hayo ni vyema wakawasiliana nao kwa maelezo zaidi. Natoa shukrani zangu vilevile kwa hawa waliotoa tathmini ya hali halisi ya suala lenyewe jinsi lilivyo katika mji wetu huu wa Dar. Asanteni sana.

Anonymous said...

Nilimwona kichaa akinya mavi barabarani na kuanza kuyachezea.

Anonymous said...

Lazima Vichaa waongezeke kwa sababu Madawa ya kulevya yamezidi kuingia nchini tena mpaka wanawake wanatumia.Athari ya bangi sio kubwa kama ya Cocaine na heorine. Tena cocaine inayouzwa kwa walala hoi ni ile inyo haribu kabisa mfumo wa akili nakuufanya uwe tegemezi kwa madawa hayo. Serekali ispo kaza buti kudhibiti madawa kutakuwa na vichaa wengi sana.Zamani tulimjua mapisto tu siku hizi hata majina huwajui walivyo wengi

Anonymous said...

Duh, anony hapo juu hivi mapisto bado yupo hai? Mbona kejeli umemsahau?

Anonymous said...

Chemi kwanini umeweka picha ya Tupac hata sielewi imeingiliana vipi na mada hiyo.