Jamani dunia inaenda wapi? Nawauliza tena mwanaume anakuwa na nyege kiasi gani mpaka kutaka kumbaka mtoto mdogo ambaye nyeti zake hazijakomaa kumudu tendo! Na hata kama ni mkubwa na hajakubali anaweza kuchanwa uke! Si uwongo! Kateni boro za hao wanaume wahalifu maana hawastahili kuwa nazo! Na wanyongwe hadharani!Na mtasoma chini, wananchi wenye hasira hawakusubiri mkondo wa sheria na hii kesi!********************************************************************************
Kutoka Freemedia.comWanafunzi wawili wafa kwa kubakwana Jumbe Ismailly, Singida
MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mrama, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida na mdogo wake aliyekuwa akisoma shule ya awali katika shule hiyo, wamefariki dunia baada ya kubakwa na kulawitiwa na watu wasiojulikana.
Wanafunzi hao wametajwa kuwa ni Twaiba Athumani (13) anayesoma darasa la sita na Zulfa Athumani (7), aliyekuwa akisoma shule ya awali.
Akizungumzia tukio hilo jana, baba wa watoto hao, Athumani Jumanne, alisema tukio hilo lilitokea juzi, kati ya saa 12 jioni na 2 usiku, umbali wa kilomita takriban mbili kutoka nyumbani kwake, kwenye eneo la shamba la viazi la mkazi mmoja wa kijiji hicho.
Alisema kabla ya tukio hilo watoto hao walitoka nyumbani majira ya saa 10:30 jioni kwenda kisimani kuchota maji kwa ajili ya kufulia nguo na kwamba mpaka inafika saa 2 usiku walikuwa hawajarudi.
Alisema, baada ya kuona hali hiyo waliamua kuwafuatilia, lakini hawakuwaona, hali iliyosababisha kwenda kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na baadaye Kituo Kidogo cha Polisi Ilongero.
“Mpaka saa mbili asubuhi walikuwa hawajarudi...ilibidi tuwafuatilie hadi kwenye eneo lililokuwa na korongo na ndipo tulipookota kiatu cha tairi cha mtuhumiwa mmoja na tulipoendelea kufuatilia hadi kwenye shamba la viazi ndipo tulipoikuta miili ya marehemu ikiwa imetapakaa vinyesi na damu.
“Tuliweza kutambua viatu vya mmoja wa watuhumiwa baada ya kufuatilia nyayo na tulipofuatilia hadi kwa mmoja wa watuhumiwa, Hamisi Msaghaa, mkazi wa Kijiji cha Mrama tulimkuta akifyatua matofali na kumchukua hadi kituo kidogo cha polisi Ilongero,” alifafanua baba wa watoto hao.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji, Issah Swedi, alisema mtuhumiwa Mile aliyetoroka inasemekana alitoka gerezani hivi karibuni baada ya kumaliza kutumikia kifungo kwa makosa ya ubakaji na kwamba amekuwa na uzoefu wa kuishi gerezani kuliko uraiani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ilongero, Greace Kishindo, alithibitisha kupokea maiti hizo huku zikiwa zimetapaa damu na vinyesi.
Polisi mkoani Singida wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba inamshikilia Msaghaa kwa tuhuma hizo na bado wanamtafuta mtuhumiwa mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Mile aliyetoroka baada ya kufanya tukio hilo.
Kwa habari zaidi someni:
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/17/habari31.php********************************************************************************
From Ippmedia.comWavamia polisi na kuua mtuhumiwa 2007-10-22 08:47:45Na Elisante John, PST, Singida
Mamia ya wananchi wenye ghadhabu wamevunja mahabusu ya kituo cha polisi cha Ilongero kilichoko wilayani Singida Vijijini, wakamtoa nje na kumpiga hadi kufa mtuhumiwa wa mauaji ya watoto wawili wa familia moja.
Aliyeuawa usiku wa kuamkia juzi ni Mile Nkindwa (20), mkazi wa Ilongelo wilayani hapo, aliyekuwa ametorokea kijiji jirani baada ya kufanya mauaji. Mtuhumiwa huyo alifikishwa kituoni kwa tuhuma za mauaji ya watoto wawili wa kike kwa kuwabaka, kuwalawiti na kuwanyonga kisha kuwatumbukiza ndani ya korongo na miili yao kugundulika ikiwa imetapakaa kinyesi na damu.
Habari kutoka kituo hicho zilisema Nkindwa baada ya mauaji hayo alitoroka na kujificha katika kijiji cha Mughamu. Hata hivyo, mtuhumiwa mwenzake Hamisi Juma Msaghaa (33) amefikishwa mahakamani mjini Singida kujibu mashtaka ya mauaji.
Akielezea tukio hilo, diwani wa Kata ya Ilongelo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Singida, Bw. Ramadhan Samwi, alisema mauaji dhidi ya mtuhumiwa huyo yalifanyika juzi saa 4:00 usiku nje ya kituo hicho. Alisema pamoja na kuwepo askari wa kutosha kutoka Singida mjini waliokwenda kituoni hapo kumchukua, wananchi walivamia kituo hicho kuanzia saa 3:00 usiku na kuwataka askari wamtoe mtuhumiwa aliyehusika na mauaji ya watoto hao.Bw. Samwi aliongeza kuwa pamoja na askari kugoma kumtoa mtuhumiwa, wananchi walishinikiza atolewe hatua iliyosababisha wapige risasi hewani ili kuwatawanya lakini wananchi waliwazidi nguvu polisi na kuvunja milango na kumburuza nje mtuhumiwa na kumpiga hadi alipokata roho. Aliongeza kuwa wanakijiji hao walimshambulia kwa mawe, marungu, fimbo na kila silaha waliyoiona hadi akaaga dunia.
Akifafanua zaidi, diwani alisema marehemu Mile alikamatwa baada ya baba yake akiongozana na mwenyekiti wa Kijiji cha Itamka Bw. Mamu Mloya, kwenda katika kijiji cha Mughamu ambako mtuhumiwa alijificha kwa jamaa zake baada mauaji hayo. Alieleza kuwa walimnasa na kumfikisha kituo cha polisi cha Ilongelo ambako jioni yake ndipo alipouawa na wananchi hao waliokerwa na mauaji hayo ya kikatili.
Waliokufa katika mkasa huo ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mrama iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida pamoja na mdogo wake aliyekuwa akisoma masomo ya awali shuleni hapo. Watoto hao ni Twaiba Athumani (13) na Zulfa Athumani (7).
Watoto hao wa Bw. Athumani Jumanne, walikumbwa na vifo hivyo vya kikatili Jumatatu iliyopita kati ya saa 12:00 jioni na 2:00 usiku katika shamba la viazi la mwanakijiji mmoja, umbali wa kilomita mbili kutoka nyumbani kwao, wakati walipokwenda kisimani kuchota maji.
Hili ni tukio la tatu katika mwezi huu la wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kuvamia vituo walimowekwa watuhumiwa wa mauaji kwa lengo la kuwaua. Mwanzoni mwa mwezi huu, wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Kagera walivamia makao makuu ya polisi na kuchoma moto kituo kwa lengo la kumuua mtuhumiwa.
Katika tukio hilo, kulikuwa na uvumi kwamba kuna mwanamke kituoni hapo anashikiliwa na polisi baada ya kukutwa akiwa na ngozi ya binadamu. Hata hivyo, habari za kipolisi zinaonyesha kuwa uvumi huo haukuwa wa kweli. Wiki iliyopita, tukio kama hilo lilijiri mkoani Tanga ambapo watu wasiofahamika walivunja ofisi ya kijiji cha Nkogoi wilayani Lushoto na kumuua mtuhumiwa wa mauaji aliyekuwa amefungiwa ofisini humo.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisubiri kupelekwa polisi ni kijana wa miaka 22, Yahaya Omari. Yeye anadaiwa kumuua kwa kumpiga rungu kichwani Muhsin Rashid (15). Marehemu Muhsin alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mavumbi.