Thursday, May 03, 2007

Barack Obama yuko chini ya ulinzi wa Secret Service


Mgombea wa raisi wa Marekani katika uchaguzi ujao, Senator Barack Obama wa Illinois, amewekwa chini ya ulinzi ya Secret Service. Kazi ya Secret Service ni kulinda watu wazito katika serikali ya Marekani kama Raisi na familia yake na makamu wake, na pia wagombea raisi lakini walioteuliwa na vyama vyao.

Obama bado hajateuliwa, hivyo ina maana kuwa lazima Secret Service wamepata habari kuwa maisha yake iko hatarini. Kama tunavyojua Obama ni mweusi na bado kuna wabaguzi hapa Marekani amabao wasingependa kuona mtu mweusi anashika uraisi. Ametokea kupendwa na watu wa kila rangi na kuna watu ambao hawafurahii kabisa! Tusisahau viongozi weusi waliouliwa na hao wabaguzi kama Martin Luther King Jr., na Medgar Evers.

Mungu amlinde na abariki Barack Obama!


********************************************************************

Thursday, May 03, 2007


(CNN) Democratic presidential hopeful Barack Obama has been placed under secret service detail, according to a statement from the U.S. Secret Service."Secretary Chertoff has, after consultation with the congressional advisory committee, authorized the United States Secret Service, to protect presidential candidate Senate Barack Obama. "As a matter of procedure, we will not release any details of the deliberations or assessments that led to protection being initiated. For security reasons we will not release the timing, scope or details of any protective operations."

12 comments:

Anonymous said...

jamani Obama sio mweus. jamani kwa nini waafrica tunawang'ang'ania maafkasti kuwa weusi. Huy ni mchanganyiko wa mtu mweusi na mweupe na sio mweusi period!

Chemi Che-Mponda said...

Kwa Marekani kama una tone ya damu ya Kiaafrika wewe ni mweusi. Ndo maana unakuta mtu kafanana na mzungu lakini wanamhesabu kama Mweusi. Enzi za utumwa ilikuwa balaa, watu walikuwa wanakimbiklia sehemu ambazo walijua watu hawatajua asili yao halafu wanajaribu kuishi kama wazungu.

Anonymous said...

Dada Chemi kule kwa Michuzi nimeshidwa kuiweka hii naomba Hoja ii ijadiliwe hapa kwako au uniwekee kwenye comment kwa kaka Michuzi. Inaenda namna hii:-

Michuzi twashukuru kwa kazi nzuri(narejea picha aliyoweka tarehe 3 may 2007 ya ufunguzi wa kikao kujadili ripoti ya CAG).

Naomba kutoa hoja sasa kijiwe chako kikae kama KAMATI na kujadili ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali. Juzi kupitia BBC nilisikia wakiiongelea. Kisha nikasikia wakiongelea na ripoti ya mkaguzi mkuu kule Uganda. Tofauti ya hii yetu na ile ya Uganda ni kuwa yule mkaguzi mkuu wa Uganda alitoa mapendekezo nini kifanyike kwa waliofuja hela ya umma.Raisi Museven (M7)amekubali.Pamoja na wengine wapo mawaziri watatu waliotumia vibaya fedha za global fund, na sasa watakabiliana na mkono wa sheria.Hapa kwetu kuna udhaufu wa aina mbili:
Kwanza, Ripoti yenyewe haikusema hawa wezi waliotumia kalamu zao kutuibia hela zetu wafanywe nini. Haikuwataja specificallty kama ile ya Uganda.
Pili, Mwitikio wa viongozi wetu umekuwa dhaifu mno kiasi cha kutiliwa shaka.Eti hawa wezi wameambiwa wajirekebishe. Ebo!. Kule walikopata hati chafu si wanajulikana kwa nini wasingekamatwa na polisi washitakiwe.Are we really serious?.Mheshimiwa rais hivyo vikao vinazidi kuendeleza upotevu wa pesa chukua hatua, kumbuka mheshimiwa rais, vitendo huongea kwa sauti zaidi kuliko maneno.Toa amri tu, wote waliofanya usanii na hela yetu sisi wananchi ambao ni waajiri wako, wezi hao wastaafishwe kwa manufaa ya umma, washitakiwe na wafilisiwe. Ukifanya matendo haya yataongea kuliko vikao mia.
Hivi ndugu wananchi, mbona wezi mitaani tunawachoma moto( siungi mkono uchomaji moto) lakini hawa jamaa tunawaacha wanaendelea kutanua?. Kwanini tusimshinikize rais ambaye sisis kwa kura zetu tumemuajiri. Ili atoe amri washitakiwe. Akumbuke alpokuwa pale wizara ya Ardhi alisema yuko tayari kuanza moja.Kuna vijana wengi tu hapa nchini , graduates wanaweza kulisaidia hili taifa. Mheshimiwa waondoe hao wezi. Au ule muda uliosema unawaopa wajirekebishe bado haujatimia?.Wakati wa kujirekebisha umekwisha .Wezi hawa wafikishwe mahakamani wakajitetee kama hawakuhusika.
Wanasema hakuna hela ya kuongezea ile 40% kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wakati wao wanazila bila aibu, wakiongeza ukubwa wa matumbo yao.
Tatu, kule Uganda tunaambiwa mkaguzi mkuu wa serikali ana hadhi kama ya jaji mkuu. Hapa kwetu hali ikoje?. Huyu mheshimiwa anahitaji mamlaka ya kudhibiti na kupendekeza hatua za kuwachukulia hawa wezi, anahitaji ulinzi wa hali ya juu,asituambie tu matumizi mabaya, atueleze wahusika kwa nyadhifa zao na hata kwa majina.Kwa kuwa hela hizo ni zetu sisi walipa kodi tunapaswa kujua kila kitu.Kifupi huyu bwana ACG apate meno makali zaidi.
Hatuwezi kuendelea kama tutaendelea kuoneana aibu. Kwa kuwa tu ni wa chama chetu basi tunamuacha. Kwa kuwa tu anajuana na waziri fulani na huwa wanapata nyama chma pamoja basi asiguswe.Haiwezekani.Ni lazima tujenge uwajibikaji wenye maadili mema.Lazima tujenge mifumo itakayowafanya mafisadi wakome kutenda wanavyotenda. Lazima tuonyeshe kuwa nchi hii ina wenyewe na wenyewe ndio sisi. Yaani mimi, Michuzi na wewe unayesoma.
Baada ya kusema hayo machache, sasa kwa heshima kubwa naomba kijiwe cha ndugu Michuzi kikae kama kamati na kuijadili ripoti ya ACG.
Naomba kuwasilisha.
Ni mimi Mtumzima

Anonymous said...

Dada Chemi HOJA hii imewasilishwa na Mtumzima, potokaz@yahoo.com

Anonymous said...

anonymous wa 2.26
mbona unabandika vitu ambavyo ni off topic??

KUHUSU OBAMA
1)mie ningekuwa Mmarekani ningempa kura yangu. Nimesoma kitabu chake cha "Audacity of Hope"-jamaa anafaa kuwa rais.
2)kwa anonymous wa 2:49-kwa wazungu: black + white=black, hilo swala la afkasti halipo kwenye msamiati wa wazungu.

Anonymous said...

Da Chemi, sasa Al Sharpton nae abadilike kwa maana ndie mweusi anaempinga waziwazi Obama mie kwa upande wangu namwona huyu mzee ana tabia za kiswahli/weusi anapenda ujiko na kutambulisha familia yake ili kujipa misifa tu.Kuhusu huyo anaedai kwamba Obama sio mweusi inabidi tumshangae yaani baba yako awe Mjaluo afu wewe uwe Mzungu kwa vile tu mama yako Mzungu!?Nadhani mtoa hoja sio mwafrika I mean weusi wote wa hapa Amerika wanaitwa waafrika wa amerika na sio chinese or what Americans.

Chemi Che-Mponda said...

Al Sharpton asisahau kuwa babu yake alikuwa mzungu! Loh, lakini ubaguzi ya weusi kwa weusi unatia kinyaa.

Hapa Marekani utasikia weusi wanasema Obama siyo mweusi kwa vile baba yake ni Mkenya. Hao weusi wa hapa wana asili ya utumwa, na wanasema Obama hana na pia Kenya iko Eastt Africa na watumwa wote walitoka West Africa. Lakini mbona maisha yake yote hapa USA Obama ameishi kama mtu mweusi? Hawajasema, oh baba yako ni Mkenya hivyo wewe siyo mweusi na hatutakuhesabu kama mweusi. Siasa za Marekani bwana.

Nawaambia mlioko Bongo, hapa USA kila kitu ni white na black. Na usifikirie kuwa wiki itapita na hujakumbushwa wewe ni mtu mweusi!

Anonymous said...

Wamarekani weusi ni wapumbavu kwa sababu wana asili ya utumwa, mtumwa yeyote ni mshenzi tu kama hataki kujitambua na kubadilika na ndivyo walivyo hawa kenge. Wanambagua Obama wakati wenyewe wanabaguliwa na Wazungu na wanaonwa kama mavi... mishenzi sana hii na itabaki kuwatumikia Wazungu mpaka kesho. Mtu yeyote mwenye damu ya Mwafrika ni mweusi, kwisha. Wapo wehu kama yule wa gofu ambao hawataki kujitambulisha na Uafrika, lakini ni wapuuzi. Mwafrika ni mtu pia.

Anonymous said...

Jamani da chemi na hao watu msemao Obama ni mweusi sikubaliani na nyie kabisa. Obama ni half cast huwezi ita mchanganyiko wa punda na farasi, farasi au punda bali ni mule. Obama achukuliwe kama mchanganyiko. Pundamilia ni weusi au weupe??
Kuhusu hilo swala la wamarekani weusiwao ni wapumbavu toka enzi kwa hiyo msiumize kichwa kuwajadili.

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe hapo juu kabisa.kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri huwezi muita Obama mweusi. Hawa wazungu or waafrika koko wanaitwa wusi na wazungu kutokana na historia. Wazungu waliwaita hawa watu mchanganyiko weusi kwa sababu walionekana kama aibu kwa jamii ya wazungu.
Obamasi mweusi kabisssaaaaa

Anonymous said...

Wajameni msomeni na Mtumzima basi hapo anony 2:26. Muidiskas.Nchi ya bongo inaliwa na wenye meno.
Nakubali kuwa niko off topic kama mlalahoi anavyosema. Nimesukumwa na uzalendo.

Anonymous said...

very good read
dreams of my father
- a story of race and inheritance
Barack Obama.
people should not be defined by the color of their skin or their origin of birth
but their contribution to society and human mankind
in the eyes of God we are all souls of his own making.