Tuesday, May 08, 2007

Pole sana Mheshimiwa Dada Amina Chifupa






Natoa pole, tena pole sana kwa Dada Amina Chifupa (Mbunge Viti Maalum). Miaka mingi nimekuwa nikifuatilia habari zake. Lakini hii miaka ya ya karibuni maisha yake yameanikwa hadharani na kushabikiwa kama vile maisha ya hao stars wa Hollywood. Yaani maisha yake imekuwa kama Tanzanian Soap Opera. Ni kama vile papparazzi wanavyofuatilia maisha ya Paris Hilton hapa Marekani..oh sijui kavaa hivi, katembea na huyo, alionekana sijui wapi! Khaa! Na inaelekea watu hawatosheki na habari wanazaopata kuhusu Dada Amina, wanataka zaidi na zaidi.

Kwa kweli tangu jana nilisikitika sana nilivyosikia kuwa mume wake kampa TALAKA! Nilidhania wana ndoa safi sana. Lakini tena ndoa yao naona imekuwa kama hizi ndoa za Hollywood, hazidumu!

Nampongeza Baba yake Luteni Chifupa kwa kuzuia Amina kufanya Press Conference kuhusu yaliompata. Ni mapema mno. Ngojea apoe kidogo maana lazima atakuwa ameshutuka mno, anaweza kuwa na hasira na kusema maneno ya ajabu na baadaye kujuta.

Sijui kama habari nilizosikia juu ya kisa cha Dada Amina kuachika ni kweli. Lakini kama ni ya kweli basi ni aibu kwa huyo mwanaume. Je, alishindwa kumtosheleza mke wake kwenye mambo ya unyumba? Hatimaye ukweli utajulikana.
Dada Amina, kumbuka kuwa watu watasema na mwisho watachoka! Nyayua kichwa juu ukitembea barabarani wala usijali maneno ya watu. Unajua maisha yako mwenyewe. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia wanaume wako wengi katika dunia hii, na dunia ya leo si lazima uwe na mwanaume. Wakati mwingine mwanaume ni mzigo na mzuia maendeleo ya mwanamke. Samahani nimeingiza 'women's lib' hapa!

Na ambaye anatarajia kuolewa na huyo Bwana Mpakanija ajue kuwa atamtendea kama alivyomtendea Dada Amina. Kwa bahati mbaya ndivyo wanaume walivyo...wakimtendea mwanamke moja hivi na mwingine atatendewa vile vile.
Pamoja na kuwa nimemsema Bwana Mpakanija natoa pole kwake maana ni hatua kubwa aliyochukua na maisha yake pia yameanikwa hadharani. Jamani, mbona mlivyofunga ndoa mlionekana mna mapenzi mno.

Karibuni mtoe maoni.
Kwa habari zaidi ya Mheshimiwa Dada Amina Chifupa someni:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2787

32 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi,kumbe hukuwa na habari kwamba Mpakanjia alimtalaka mkewe kwanza ili afunge ndoa na huyo mtoto wa shule!!(manake ndio alikua anamaliza tu school na ankuja juu clouds0.Hivo hukukosea kwamba labda tayari kuna mwingine ataingiza timu karibuni.Anyway,yote maisha.

Chemi Che-Mponda said...

Duh! Hiyo habari sikuwa nazo. Kama hivyo basi lazima alijua kuwa atupwa na huyo jamaa. Wanaume sijui walivyo!

Lakini wazungu wana usemi WHAT GOES AROUND COMES AROUND!

Anonymous said...

chemi hizi habari za maisha binafsi ya amina hakuna anayezitafiti ni amina mwenyewe ndio anawapigia waandishi wenzake ili waziweke hewani.kwani wale wabunge wengine waliokaa kimya ndoa zao ziko stable?

Anonymous said...

NAONA CHEMI UNAMSAPAOTI HUYU MALAYA WA KIKE KWA UMALAYA WAKE MBOVU ULIOPITA MIPAKA BUNGENI NA NJE YA BUNGE. HIVI NANI ASIYEJUA KUWA ZITTO ANAMLA AMINAH? AU HAUFAHAMU HATA KESHAWAHI KUTWA HOTELINI DODOMA KAVAA KOTI LA ZITTO KISA ETI BARIDI?

PIA ELEWA KUWA KUNA "WAHESHIMIWA" WENGI TU PALE DODOMA WAMEMLA UCHI HUYU MTOTO WA KIKE.DR MATHAYO NI MMOJA WAPO.SASA ULITAKA MPAKA-ROAD AFANYE NINI? ACHA U-FEMINISM KTK MAMBO YA UMALAYA WEWE!

Anonymous said...

Mwanamke mwenye hurka ya umalaya lazima atajibanza kwenye upiginiaji haki za kijinga za wanawake kama wewe Chemi. Iwapo mtu anashindwa kutambua kuwa mwanaume na mwanamke wanapokuwa pamoja wana uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kuliko kila mmmoja akiwa peke yake, basi ameliwa. Amina ni changu tu, tunaojua habari zake hatushangai. Kabla hajaolewa na Mpakanjia, achilia mbali hiyo ya jamaa kumtosa mkewe, alikuwa anachukua mume wa mtu ambaye alikuwa hajatimiza hata mwaka na mkewe, kijana maarufu mjini hapo, simtaji kwa sasa. Halafu yule mke wa kwanza wa Mpakanjia hakuzaa mtoto nadhani, na Amina sikuwahi kusikia kazaa, kinaendelea nini hapo? Pia msisahau Bungeni ni shimo la umalaya.

Chemi Che-Mponda said...

Mbona mnaomsema Amina Chifupa hamtaji majina yenu? Anonymous, anonymous? Kama mmesema kweli si mgetaja majina?

Hizo habari za yeye kuwa mwingi ndo nasikia kutoka kwenu. Mwisho anajua mwenyewe alichotenda.

Nachosema ni nasikitika kuona maisha yake yameanikwa hadharani nadhani kuliko mwanamke yeyote wa kiTanzania. Yeye ndo Paris Hilton wetu. Lazima ana roho ngumu kuvumilia maneno na matusi yote hayo.

Unknown said...

Kweli da Chem lkn sijui nani alaumiwe?! najiuliza kwanini private life yake iwe hewani hivyo. Halafu haya mambo ya eti fulani katembea na mume/mke wa mtu si tuna yasikia kila siku tu sioni jipya.

Ukweli anaujua yeye mwenyewe Amina lkn why watu wamtukane? Maisha ni mstari kila mtu ana wake

Waridi

Anonymous said...

sasa da Chemi naona umechemsha. Kwa upande mwingine unasema kuwa hujui undani wa Amina, na hapo hapo unamtetea na kulaumu wanaume....

maoni yangu kuhusu hii mada
1) Amina Chifupa anastahili "publicity" kwa sababu yeye mwenyewe ni story-madisko sana, tuhuma kuwa mme wake ni zungu la unga n.k.
2) Huyo Amina, naye anakosea kukaa kimya-unapokataa kuongea na vyombo vya habari ndio unaongoza "juice" kwenye story kwa sababu waandishi wa habari wanaendelea kutengeneza habari zao wenyewe nyingi zikiwa za uongo.
3) kuna tuhuma kuwa Mheshimiwa Zitto naye alikuwa anapata. Lakini amekanusha vikali hayo madai, na amedai kuvishtaki vyombo vya habari.

Chemi Che-Mponda said...

mlalahoi,

Lazima nimtetee. Ujue Tanzania mwanamke akija juu lazima asemwe hata kama hana makosa. Ndo maana naamini kuwa kwa upande fulani kuna exaggerations.

Kuhusiana na hiyo habari ya Mheshimwa Zitto sijui, wanajua wenyewe.

Kwa upande wa Public Relations, ni kweli kuwa Amina angejitokeza sasa kuongea na waandishi wa habari ila kuzima huo moto.

Lakini kama ni kweli alitembea nje ya ndoa yake, lazima watu waulize sababu yake ni nini?

Anonymous said...

Kwanza Mpakanija si fundi kitandani navyosikia. Unene unamponza. Halafu ni risasi tupu blenki. Mbona kati ya wanawake wawili hakuna aliyezaa. Amina ni damu moto ilikuwa lazima atafute nje.

Anonymous said...

Da Chemi,mimi ndio niloanza toa comment hapo juu,pamoja na kujua kwamba Amina alioelewa baada ya kutoa shinikizo Meddy amwache mke wake kwanza,lakini sikubaliani na wote ambao wanadai kwamba binti huyu ni malaya isipokua yeye amebahatika kuwa"Star" na kuolewa na Meddy ambaye pia ni mtoto wa mjini kukamwongezea ujiko plus Ubunge wa viti maalum ndio kabisa.Kwa watu kama mie ambao tumewahi kuwa juu kidogo kwa namna moja ama nyingine kuitwa malaya ni kawaida sana kwani inapotokea ukawa beneti na mtu wa sex tofauti kwao "is an affair".Lakini sidhani kama binti huyu ni malaya kama ambavyo baadhi yetu tumediliki kumwita.

Anonymous said...

Unajua Chemi, sisi tunaosihi hapa Dar ndiyo tunamjua Amina tangu yupo Clouds. Huyu binti pamoja na kwamba ni super star lakini naye anajiharibia, maana anapenda sana sifa. Hivyo utakuta yeye anayaanika mambo yake kwa waandishi wa habari kwa kujidanganya kwamba anashirikiana na waandishi wa habari, which is wrong. Amina si malaya kama watu wanavyosema, ila amekuwa na uhusiano kadhaa wakati yupo shule, clouds hadi kumpata Meddy. Tatizo sifa zinamponza. Kama mke wa mtu hutakiwi kuropoka kila issue ya familia, lazima atofautishe kati ya ubunge na familia. Meddy ni mtoto wa mjini tunamjua sana, kilichofanyika hapa ni kumtumia binti hadi amechoka na amapigwa chini, kitoto kingine kinatinga muda wowote.

by Rajabu-Mtoto wa Sinza

Anonymous said...

Vigogo waingilia kati sakata la Chifupa

(http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=1559)

BAADHI ya viongozi wa ngazi za juu serikalini na CCM, wanadaiwa kumkataza katika dakika za mwisho, Mbunge wa Viti Maalum Amina Chifupa (CCM) asianike masuala ya familia yake na siasa kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa Amina alikatazwa kwa nyakati tofauti na viongozi kwa kile kinachodaiwa kingevuruga mambo hata ndani ya CCM.

Juzi Amina alijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari katika Idara ya Habari (Maelezo) Dar es Salaam, kuhusu mvurugano uliotokea kwenye ndoa na nia yake ya kuwania nafasi ya ju ya uongozi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM. Hata hivyo, katika mkutano huo hakutokea na badala yake alijitokeza baba yake mzazi Hamis Chifupa, hali ambayo ilifanya masuala nyeti ambayo angeyaibua Amina, kufichwa.

Baba yake Amina katika mkutano huo alionekana hakuweza kujibu maswali ya waandishi wa habari ilivyotakiwa. Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Amina alipanga kuanika ‘madudu’ yote yaliyotengenezwa na wapinzani wake ndani ya CCM baada ya kuhisi anaonyesha nia ya kuwania nafasi ya juu ndani ya UV-CCM.

Habari zinasema viogogo waliamua kujitosa kuepusha mvurugano ambao ungeweza kujitokeza ndani ya CCM na Serikali kwa ujumlakama angezungumza na vyombo vya habari. Kuvunjika kwa ndoa ya Amina na Mohammed Mpakanjia kunahusishwa moja kwa moja na masuala ya kinyang’anyiro cha uongozi ndani ya UV- CCM.

Moja ya ujumbe wa maandishi ambao unaonyesha kuwapo kwa mvutano unaotokana na kinyang’anyiro cha uongozi ndani ya CCM ni ule unaodaiwa kutumwa na Amina kwa mmoja wa vigogo wa CCM na kiongozi wa Serikali ambao ulisomeka: “Alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kukitenganisha.

Nakuheshimu sana kama kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu, Naibu Waziri, M-NEC, M-CC, mkubwa wangu kiumri, mbunge nakadhalika. Nimesikitishwa sana jitihada za kutaka kuvuruga ndoa yangu, nakutakia kila la heri, lakini usisahau malipo ni hapa hapa duniani na kila mwenye kufanyia wenzake mabaya na yeye hulipwa kwa ubaya.

Nampenda sana mume wangu na ntailinda ndoa yangu kwa gharama yoyote cko tayari kumpoteza, mi ni zaidi ya mwanamke. Asante sana, kila la heri na kazi yenye katika kulifanikisha hilo, wizara yako nyeti sana, ina mambo mengi sana. Bye.

Ujumbe huo unadaiwa kusambazwa Mei 3, mwaka huu kwa baadhi ya watu wa karibu wa Amina na kigogo aliyetumiwa ujumbe huo.

Mara nyingi wakati uchaguzi unapoingia ndani ya CCM, huibuka kashfa za kila aina, hali ambayo kuweza hata kuwaharibia sifa watu wanaowania nafasi mbalimbali. CCM imekwisha kuanza kufanya uchaguzi wa viongozi wake katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya mashina.

Anonymous said...

HAYA YOTE NI MAISHA.ASANTE DADA CHE!NINAJIFUNZA MENGI SANA YA KIMAISHA KATIKA HIZI BLOG !KWELI MAISHA NI DUARA!KABLA HALIJAKUFIKA UTAANDIKA NA KUSEMA MENGI LAKINI YAKIKUFIKA UTAJUA MCHELE NI UPI NA PUMBA NI ZIPI!MAISHA YA WANAWAKE HAYO!TULIAMBIWA KUWENI MUYAONE!NIMEYAONA BINAFSI NA NAZIDI KUYASOMA!POLE AMINA NA POLE MPAKANJIA!POLENI WANAWAKE WOTE DUNIANI!

Anonymous said...

Hivi humu ndani kuna watoto wangapi maana naona watu wameshikia kidedea kwa vijana wa wili tena vijana sana ukiachilia majukumu yao kisiasa kulalana kwa kweli sielewi ,ilmuradi kuna ridhaa na kuwa hakufanywa kinyume na matakwa yake wenye uchungu sana mbona sijasikia mnamhoji Mzee Kawawa au Malecela mbona na wao wameutandaza sana ududu wao enzi zao kama huko mbali haya na hawa Boyz to Men je, acheni zenu za kuleta mpisheni njia aende zake azeni mijadala ya Saccos, Mkurabita, Mkukuta na jinsi timu yenu ya taifa itakavyotairiwa tena huko Mwanza kwanza sijui kama huyo rais ataenda kufumania aibu tutakayoipata huko MWZ

Anonymous said...

Jamani mona mimi sioni uzuri wa Amina Chifupa. utasikia ooh.. mtoto mzuri hivyo. Mbona mashau kamaandazi acha mpaka njia ajitafutie mtoto mdogo Amina ashazeeka

Anonymous said...

'wanaume ni mzigo.....!' we chemi acha kututukana!
Ila kuna ukweli kitakwimu kuwa wanawake wengi wanaotetea sana haki za wamama ndoa zao zimeoza au hazina uhai ama wameshatalikiwa!!!!

Tengenezeni kwenu kwanza b'se charity begins at home!

Anonymous said...

Nakubaliana na Da Chemi wanaume ni mzigo na washenzi! Wana nyege za ajabu pia! Hebu tulia na mke moja basi!

Anonymous said...

hawa wote wanaoandika kuwa wanaume ni mizigo ni wanawake wenye matatizo kwenyemaisha yao ya mapenzi. Dada chemi ni mama mchungaji hii inaeleza yote. Na hao wengine ni wanawake wasio na mvuto wa kupata mwanaume wa kutulia nao

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 4:26am, ingekuwa vizuri ungejitaja kwa jina lako halisi badala ya kujificha nyuma ya jina Anonymous. Unalaumu akina mama wanaosema kuwa wanaume wana matitizo kwa nini. Tunajua kuwa wengi wanaojiita anonymous ni waongo na wenye matatizo pia.

Sawa, mimi ni Mama Mchungaji, una shida gani na mimi kuwa mama mchungaji? Akina Mama Wachungaji na Mama Sheikh wako wengi dunia hii. Au na wewe unataka kuwa Mama Mchungaji.

Kwanza wanaume wanajiona ni bora kuliko wanawake dunia hii. Lakini mbona wanawake wanaishi kwa muda mrefu ziadi ya wanaume? Na naona nitaandika mada juu ya Women's Lib hivi karibuni.

AKINA MAMA OYEE!

Chemi Che-Mponda said...

mathew,

Asante kwa kujipa jina. At least sina haja ya kukuita anonymous, maana anonymous wako wengi na ina confuse sana.

Kwa hiyo una maana kuwa mwanamke anayeshabikia Women's Lib hatosheki kitandani? Kama hivyo ni mawazo finyu. Na kuhusu wasagaji, mimi siingilii hapo, maana utasema nini kuhusu wanaume wanapenda kufanya wenyewe kwa wenyewe?

Mjue bila women's lib tusingekuwa na wanawake wengi kwenye fani kama engineering, sheria, uandishi wa habari, na megnineyo. Pia zamani shule za wasichana zilikuwa ni chache sana ukilinganisha na shule za wanaume, hata uzunguni ilikuwa hivyo.

Nasema ASANTE Women's Lib! Na siyo kuwa ilianza juzi juzi, hata miaka ya 1800' women's libbers walikuwepo. Akina Dada lazima waelewe kuwa nafasi walizo nazo leo ni kwa sababu ya jitihada za mabibi zetu!

Anonymous said...

kwanza kabisa napenda kuwafahamisha kuwa tusiwe wanafiki kabisa kwa sababu ngono inafanywa kila mahali iwe bungeni iwe mitaani watu wa madaraja yote,huu niunafiki mkubwa kumsema Amina chifupa.,Mbona yeye Mpakanjia tunasikia skendo zake nyingi tu mitaani au kwa sababu yeye ni mwanaume? mimi ni mwanaume sisi wanaume ndio wabaya sana sisi ndio tunaanza kuwa aprochi wanawake kwa mbinu zote hivi mnfikiri wanawake waO hawana hisIa za kimapenzi? au niwanume tu? .HIVi umalaya utatoka wapi kama wanaume hawahusiki?.wanaume wana matatizo mengi sana ya nguvu za kiume na wanawakinai wake zao haraka sana baada ya kuoana hii inasabaishwa na mambo mengi ikiwemo utumiaji wa vilevi mbalimblina vyakula kwa hiyo kurivive their potence wanakimbilia kwa machangudoa kwa sababu watapata mapenzi wanayoyataka kwa sababu machangu wanafanya kazi za ziada kuamsha hisia zao jambo ambalo mkeo halitegemei ikiwepo wanaopenda kulawiti hawawezi kuwaomba wake zao. kwa hiyo kila mtu ana maoni yakelakini mengine ni ya chuki na wivu wengine inawezekana walimtongoza Amina Chifupa akawakatalia ndio maana wanakuja na maoni ya kutukana haswa.Mimi ni mwanamume ,iam going to make some of my confession.NImefanya mapenzi na wanawake wa kabila tofauti na mimi ndio nilikuwa nawashawishI,nimeshafanya mapenzi na mke wa balozi ndani ya basi usikub ,nimeshafanya mapenzi kwenye mtaro ,kwenye baa,kwenye vichaka, sakafuni nk siyo kwamba sehemu mzuri ilikua hakuna la hasha ni utundu tu kiume na mimi ndiye nilikua nashawishi hayo.utakuta wanafiki wanaongelea mambo hayo huku wakitoa macho kama wamemeza panya. Mwanamke hata ajifunike manguo mpaka utosini sisi wanaume tunamdharau tu tunajua ni mnafiki anawadanganya wanawake wenzake kwa sababu hawezi kuepuka vishawishi vya wanaume sisi ndio initiata.TUACHE UNAFIKI.

Anonymous said...

Haya sasa Mpakanjia na wauza unga wenzio mmemuua Amina tegemeo la taifa letu. Wewe una faida gani kwa Tanzania? Nenda nchi za nje ukaongezewe uume wako uache kuchafua chafua watoto wa watu na uwezo huna! Amina amekufa shahidi wa mambo matatu: Mfumo Dume ulikithiri Tanzania, CCM ilivyochoka uongozi, na biashara ya madawa ya kulevya navyoendeshwa na viongozi wa CCM

Anonymous said...

Amina umekufa bado taifa linakuhitaji na vijana kwa ujumla tunasikitika. Umeteketea kama mshumaa kwenye upepo. ulikua mfano wa mwanamke jasiri mwenye upeo mkubwa mremba na kila kitu ambacho Mungu alipenda mwanamke awe nacho tulijua siku moja utakua kama Margareth Thatcher wa Tanzania au Arroyo lakini Mungu hakupenda. Nasikitika ulivuka majaribu mengi ulishindwaje kulivuka hili la media ccm na talaka? Mbona jay dee alitoa wimbo wakati muafaka kwamba siku hazigandi na kila mtu ana dhambi na siku hazigandi. Nadhani sasa shigongo atafurahi malaya mkubwa amevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani mbwa mwitu. Shigongo aliingia kwenye siasa akashindwa anatumina vyombo vyake kumchafua amina na pia yeye mwenyewe ngoneka na wafanyakazi wake mmoja wapo ni Mary Raphael anajiita anti liz ni demu wake toka wanaanza uwazi na ana mke wake achilia mbali mtaani na wewe Mungu atakuumbua utakufa ukimwi!!!!!!

AMINA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI NA Tunashukuru kwa muda aliotupatia tukaishi na wewe na kutoa mchango wa kwenye bongo flava wakati ukiwa bambataa, mpira wa miguu taifa stars, Bungeni na kwenye maskani ya vijana na watoto yatima na wale walio katika mazingira magumu.

MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI AMINA


ITS ME THE GREAT

Anonymous said...

POLENI NDUGU NA JAMAA WATE WA MAREHEMU AMINA CHIFUPA.

MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI, MUNGU AKUSAMEH MADHAMBI YAKO.

Anonymous said...

IT DOES NOT MAKE ANY SENSE TRYING TO ANALYSE SOMEBODY'S WEAKNESSESS (IF AT ALL THERE IS..) BECAUSE IN THE FIRST PLACE THERE IS NO ONE WHO IS PERFECT. SECONDLY, WEAKNESSESS OF OTHER PEOPLE SHOULD BE USED AS A TEACHING GROUND BUT NOT PUBLICISING THEM BECAUSE BY DOING SO WE ARE JUST CAUSING MORE HARM IN THEIR LIVES AND COMMUNITY AT LARGE.
MIMI NINGESHAURI KILA MTU AJICHUNGUZE YEYE MWENYEWE NA KUELEWA NINI UDHAIFU WAKE NA JINSI GANI ATAUTATUA MAANA KUONGEA YA WENGINE AMBAYO TUNAYAONA HAINA MAAN KWANI KILA MTU ANAYAJUA HAYO...JE YALE YA KWAKO AMBAYO HATUYAJUI...UNADHANI KUWA WEWE UNA NAFASI NZURI KULIKO WALE WALIOANIKWA...UNAJIDANGANYA NDUGU YANGU MAANA NDANI YAKO WAUJUA UDHAIFU WAKO.
MAMBO HAYO YAWE CHANGAMOTO YA KUTUFANYA TUTAFAKARI NINI KUSUDI LA MAISHA YETU ILI TUTUMIE VEMA KILA SEKUNDE YA MAISHA YETU VEMA...UNAJUA HATUJARIBU KUISHI...TUNAISHI MAISHA MARA MOJA TU
MUNGU AWABARIKI.

Anonymous said...

Nadhani sio wakati wa kulumbana huu.

Tumepoteza taa ya vijana ngome ya vijana, mtetezi na mfano wa mwanamke halisi wa kitanzania hayo matatizo mengine binafsi kila mtu hapo bungeni wanayo. Amina alikua jasiri mwenye kujiamini na asiyeyumbishwa na mtu yeyote, alifanya alichoamini na mara zote hakuwahi kukosea katika harakati zake za kufikia ndoto zake. Aliahidi kusomesha watoto yatima, nawaonea huruma walijua wamepata mama mlezi na ghafla ametoweka.


Haya na huyo shigongo naye tuliejua anapigana na maovu, kumbe ni wa kutoa boriti kabla ya kutoa kibanzi kwenye jicho la wenzake. Alimsakama amina toka sekondari hadi kifo chake. Haya Sinta nae alitaka kujiua kwa ajili ya kuandikwa na huyo shigongo.

Haya naye taarifa zake hizo zinaanikwa, akaziandike manake hata kama ni kashfa huwa anaandika.

AMINA TUNAMPENDA SANA ILA MUNGU AMEMPENDA ZAIDI.

MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI

Anonymous said...

Kifo chako dada amina ni moja ya hatua ya kupigana na mfumo dume. Dada Amina umetoka wakati bado taifa lilihitaji mchango wako kupambana na mtandao wa madawa ya kulevya. Hata kama utakuwa ulitaja majina yao, bado ushahidi hautakuwa na nguvu kwani mtoa habari muhimu umetutoka.
Mungu atufunulie mwingine jasiri kama wewe ili hao wana mtandao matumbo yao yasitulie, yaungurume kwenye kadamnasi.
MUNGU MWENYE REHEMA AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI, ULICHOKIANZISHA NA KUKIPIGANIA KITAENDELEZWA DAIMA.
JOHN,MAFINGA

Anonymous said...

Haya jamani pole ni kwa msiba uliotokea Watanzania wenzangu. Ukweli zaidi wa kifo cha AC tutaujua tu hata kama si leo. Inapotokea mtu anatoweka ghafla hivyo na unajua alikuwa anapambana, kidogo lazima utahisi "huenda kapigwa". Na kama kweli kosa lake ndio limesababisha mtu atumie "bush science" kummaliza AC, basi tukumbuke pia kwamba asiye na kosa tu ndio awe wa kwanza kutupa jiwe...otherwise kama kweli ni mtu kampiga AC, basi kuna malipo ya Mwenyezi Mungu yapo.

Anonymous said...

POLENI SANA FAMILIA YA MZEE CHIFUPA .KILICHOMUUA AMINA CHIFUPA wenyewe watu wa CCM WANAJUA,ALIKUWA AKIWATETEA wananchi Watanzania wameteseka sana NA MADAWA YA KULEVYA NA WAUZA UNGA (MADAWA) YA KULEVYA NA HAWA WATU KWA SABABU WAKO CCM WAMEAMUA KUMUUA AMINA CHIFUPA.MPAKA NJIA, ALIYEKUWA BWANA WAKE YEYE NDIYE ANAYEJUA KILIHOMPATA KWA SABABU HUENDA ALIKUWA ANAPOKEA AMRI KUTOKA KWA WAUZAJI WENZAKE ILI AMINA ASIWATAJE, NDIO MAANA MARA TU BAADA YA AMINA KUPEWA TALAKA NDIO MATATIZO YAKAANZA NA CHOKOCHOKO ZILIANZIA HUKO HUKO CCM .NA HUYO ALIYEKUWA ANAPELEKA UMBEA ILI KUVUNJA NDOA YA AMINA ANAJULIKANA ,NAOMBA WANANCHI WA TANZANIA WASIMCHAGUE HATA WAKIONA NYUMBA YAKE INAUNGUA MOTO WASIENDE .CCM INA BAADHI YA WABUNGE WAJINGA KUPITA MPAKA NDIO MAANA,TUNAPOFUATILIA VIKAO VYA BUNGE TUNAWONA WABUNGE AMBAO TUMEWACHAGUA WENYEWE WANASHANGILIA HOJA ZA KUWAUMIZA WATANZANIA.MFANO TUKIRUDI NYUMA KWENYE BUNGE LILILOPITA -- SPIKA WA BUNGE ALIJITAHIDI NA ANAZIDI KUJITAHIDI KULIWEKA BUNGE KATIKA MFUMO MZURI WA KIDEMOKRASIA YA UWAZI NA UKWELI LAKINI WAO HAWATAKI WANAMPIGA VITA NDIYO MAANA KAMATI YA BUNGE ILIYOKUWA IKICHUNGUZA MZOZO KATI YA MENGI NA MALIMA ILISEMA MALIMA ALILIONGOPEA BUNGE LAKINI BAADHI YA WABUNGE WAJINGA WALIKUWA WAKIMSHANGILIA MALIMA KILA ALIPOKUWA AKIJITAHIDI KUTETEA UJINGA WAKE MBELE YA WATANZANIA. SISI WNANCHI TUNA WAMAKI SANA WATU HAWA HA WAKATI MALIMA ANATOA ILE HOJA TULIJUA AMETUMWANA NA MTOTO MDOGO ,NA HUYO SIYO MWINGINE NI MANJI,AMBAYE KILA ANACHOFANYA NI UHUJUMU TU NA RUSHWA KWAKE NI NJE NJE,AKIAGIZA MCHELE LAZIMA UTAKUWA UMEOZA NA ANAWALISHA WATANZANIA NA SERIKALI INAMUANGALIA TU .AMEHUJUMU NSSF LAKINI SERIKALI IKO KIMYA,SIJUI RAISI ANASUBIRI NINI KUAMURU AKAMATWE. TUNAJUA MALIMA ALITUMWA NA MANJI PAMOJA NA MAKAMBA HUYU NDIYE ALIYEMSAIDIA MANJI KUNUNUA UWANJA WETU WA BAKWATA -- HUYU MAKAMBA NI KATIBU MKUU WA CCM NA MALIMA BAADA YA KUONA BUNGENI AMESHINDWA,AKAPELEKA MASHTTAKA YAKE KWA MAKAMBA!AIBU,AKAZIDI KUVUNJA TARATIBU ZA BUNGE AKAACHWA .TUNAJUA MANJI ANAUZA MADAWA YA KULEVYA TUNAJUA MANJI ALIWAHI KULETA MCHELE MBOVU,MKEMIA MKUU WA SERIKALI AKSSEMA UCHOMWE MOTO SUALA LIKAFIKISHWA MAHAKAMANI,KILICHOTOKEA NI KWAMBA MANJI ALIMUUA MKEMIA MKUU WA SERIKALI PAMOJA NA MASHAHIDI WOTE KUNA WAKATI WATANZANIA WATAMTIA RISASI AU KITANZI KWA UOVU WAKE HUU WATANZANIA WANAWEKA KUMBUKUMBU . CHA AJABU,SI KUWAHI KUFIKIRIA HATA SIKU MOJA KWAMBA MAKAMBA NI MLA RUSHWA KIASI HIKI, KWANZA NILIKUWA NAMUOMBEA KWA MUNGU SIKU MAJA AJE KUWA RAISI WA TANZANIA LAKINI AMEOZAA!HAFAI.SASA TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWAO?SISI WANANCHI TUNAWADHARAU VIBAYA SASA HIVI NDIO MAANA SIKU HIZI TUKIWAONA WANAONGEA KWENYE TV, TUNABADILISHA CHANNEL WANATUTIA KICHEFU CHEFU VIONGOZI WETU WAMEWEKA MBELE USANII WA KISIASA KULIKO KUWATUMIKIA WANANCHI MAISHA YAMEKUWA MAGUMU SANA WANAOTESEKA NI WALALAHOI,VIONGOZI WAO NI VICHEKO TU. MFANO MWINGINE WA KUTIA KICHEFU CHEFU NI PALE MBUNGE MMOJA MWANAMKE ALIPOMUULIZA SWALI WAZIRI HIVI:- NI MIKOA GANI INAYOJISHUGULISHA NA UKEKETAJI WA WANAWAKE HAPA TANZANIA? WAZIRI AKATAJA KWA MAKINI AKATAJA:- DODOMA,KLIMANJARO,MARA,ARUSHA NA SINGIDA. CHA KUSHANGAZA,MARA TU BAADA YA KUJIBIWA MBUNGE YULE ALIYEKUWA AMEJIFUNIKA MIGUO HAKUWEZA KUKWEPA KAMERA ILIYOKUWA MAKINI SANA ,MBUNGE YULE ALIANZA KUVUNJIKA MBAVU KWA KUCHEKA HUKU AKIINAMA KUCHUNGULIA,MACHO YAKE AKIYAELEKEZA UPANDE WA KULIA KWAKE ,KUMTAFUTA MTU AMBAYE SISI TULIMTAFSIRI NI WABUNGE KUTOKA MIKOA HIYO INAYOKEKETA WANAWAKE,KWA MANTIKI HIYO SWALI HILI ALILIULIZA KWA MZAHA NA INAONEKANA ALISIMAMA TU ILI WATU WAMUONE NA SISI WANANCHI TUONE UJINGA WAKE ,HATA SURA YAKE INAONYESHA NI MJINGA KWELIKWELI SASA MIZAHA KAMA HII ITAKWISHA LINI KWAYE BUNGE LETU? MISWADA MINGI INAYOPELEKWA BUNGENI INAKUWA YA KULINDA MSLAHI BINAFSI TU. JUZI MZINDIKAYA AMEANBIWA AMEFUJA PESA ZA SERIKALI WAKATI AKITOA HOJA ZA KUJITETEA ILI KULINDA UOVU WAKE WABUNGE WA CCM WAKAWA WANAMSHANGILIA ETI KULINDA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA KUFUJA NA KUIBA PESA ZA UMA .TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA HAWA WATU?.UTAFIKIRI NI KIKUNI CHA WAVUTA BANGI TU.HIVI RAIS WETU HUWA ANAFUATILIA VIKAO VYA BUNGE!KWA NINI SIKU HII AMEKUWA MUOGA KUPITA KIASI?AU NDIO ALAMA ZA NYAKATI ZIMEFIKA?WATU WANAIBA YEYE ANAKAA KIMYA TU,SASA HATA AKIONGEA KWENYE TV WATU HAWATAKI KUMSIKILIZA KWA SABABU ANA WAKUMBATIA SANA WAFANYABIASHARA HASA WA MAFUTA WATU WANASEMA HUENDA ALIWAKOPA PESA WAKATI WA KAMPENI KWA HIYO ANAWAFUMBIA MACHO ILI WATUTIE ADABU.KWA KUPANDISHA BEI ZA VITU HOLELA HOLEA HAKUNA ANAYEMTETA MWANANCHI.WANANCHI WAMEMUOMBA RAISI TPDC NDIO WAPEWE JUKUMU LA KUAGIZA MAFUE\TA LAKINI YEYE HATAKI.IKIJA WAKATI WA BAJETI KILA MWAKA WANAKIMBILA KUPANDISHA BEI BAI YA BIA ,MAFUTA ,SODA SIGARA NK,UTAFIKIRI HIZO BIA WANAKUNYWA WATU TOFAUI NA WLE WALIOWPIGIA KURA KWA HIYO WANAWAADHIBU WANYWAJI KWA KUFUATA MAWAZO YA YA WATU WA DINI AMBAO TUNAWAJUA NI WANAFIKI WAOVU WA KUPINDUKIA KAMA NDIVYO HIVYO BASI WAFUNGE VIWANDA.HALAFU HUYU WAZIRI WA FEDHA MEDJI ANTOKEA KWENYE GAZETI NA MKOBA WAKE HUKU AKITOA TABASMU LISILO NA MVUTO WOWOTE BILA HATA HAYA AIBU UTAFIKIRI KWEHYE MKOBA HUO KUNA BAJETI YA KUWASAIDIA WALALAHOI SIJUI KAMA AMESOMA,HATUTAKI HATA KUONA USO WAKE.VIONGOZI WETU WANATAKIWA KUJUA KUWA KUNA WATU NDANI YA CCM AMBAO HAWATAKI HAYA MAMBO WANAYOWAFANYIA WANANCHI WATAKUJA KUWAHUKUMU. NAOMBA MKUSANYE DATA TU,TUKO NYUMA YENU.ACHENI WIZI NINYI VIONGOZI WA WATANZANIA MNATAFUTA SIFA NJE WAKATI KWENU KUNAOZA,MBONA RWANDA NA BURUNDI BEI YA PETROLI NI RAHISI KULIKO HAPA NA WAKATI HAWANA HATA BANDARI.HAPA TANZANIA KILA KITU NI LUXURY HATA MCHICHA.SASA WENYE MABASI WANAJIANDAA KUPANDISHA NAULI ZA USAFIRI ,ETI NEDJI ANASENA ETI ATAFUATILIA WATU WASIPANDISHE BEI HOVYO! WEWE HUYO HUYO TUNAYEKUJUA AU MWINGINE?.KIONGOZI GANI HAPA TANZANIA AKITOA AMRI INATEKELEZWA? HII NI KWASABABU MNADHARAULIWA KWA VITENDO VYENU WAKATI WA MWALIMU KIBAO KIKIWEKWA KUKATAZA JAMBO FULANI WATU WALITII.KILA JAMBO HAPA UTASIKIA TUNAFANYA UCHUNGUZI HATA MAMBO YA WWAZI.MACHINGA BADO WAPO,WAPIGA DEBE BADO WANAWABUGUDHI WANANCHI.WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA NDIO WANAOWAFUGA WAHALIFU VIBANDA BADO VINAJENGWA,WATU WANAKABWA HAKUNA WA KUTUTETEA WAO WENYEVITI NA MADIWANI KAZI YAO KUFUATILIA RUSHWA TU KILA SIKU ,MICHANGO YA OFISI HAIISHI HAWA WENYEVITI WA S.ZA MITAA NI VIZURI WAONDOLEWE KUTOKA KATIKA NAFASI ZAO BADALA YAKE WALETWE MAASKARI WAAJIRIWA WAO WAWE WSAIDIZI MAASKARI WATAKUWA NA NIDHAMU YA KAZI NA WAEAWAJIBIKA. SIASA ZINAHARIBU NCHI HII HAKUNA KAZI WANAYOIFANYA WAONDOENI HAWA VIONGOZI TUTATESEKA MPAKA LINI? .SI BORA TUNGEPATA UHURU KUTOKA KWA WA WAKOLONI LEO HII TUNGEKUWA NA MAENDELEO MAZURI VIONGOZI WETU HAWAJIAMINI KABISA HALAFU NI WABINAFSI KABSA .HEBU FIKIRI WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 46 YA UHURU WA TANGANYIKA ,RAISI ALIPIGIWA WIMBO WA TAIFA LAKINI YEYE HAKUWA ANAFUATILIA, WIMBO HUU AMBAO NDICHO KIELELEZO KILICHOMWEKA MADARAKANI YEYE ALIKUWA AKIIMBA VITU VINIGNE TOFAUTI KABISA HII NI AIBU KWA TAIFA KAMA MIMI MUONGO ANGALIENI KANDA .TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA HUYU MTU .TUNAOMBA WOTE MUACHIE MADARAKA UONGOZI,UMEWASHINDA NIUNGENI MKONI TUANDAE MGOM0 WA NCHI NZAMA. NAOMBA MWENYE UWO AMPELEKEE KIKWETE UJUMBE HUU

Anonymous said...

amina mwanamke shujaa! mungu akurehemu

namlaumu mpakanjia sana, sasa ndo atajua chuya na pumba, analia nini kama si unafiki? wewe mke wako uliempenda unadiriki kumpa talaka 3 tena kwa kujivuna? utajutia hili katika maisha yako yote, pamoja na kuwa alipatwa na tuhuma kuwa ana mahusiano nje mngeyamaliza ndani but sasa nadhani umeamini japo ni too late amina alikuwa anakupenda kuliko maelezo, mkeo ameintroduce issue nzito bungeni mpaka kufikia akatishiwa uhai wake, kama mume ulikuwa ni muda mzuri wa kumtia ujasiri mkeo, lakini ndo kwanza unajidai kidume kwa vile sasa amina anakuzidi kipato, ok now kula jeuri yako, leo wapambe wamekufikisha wapi? utajutia siku zote za uhai wako, ninaamini mbali na matatizo mengine you ar the courser of this.

awaze mangapi? bungeni, kila kukicha ktk magazeti, still na wewe unakandamiza, she is a human being amejitahid kujikaza at last yamemletea magonjwa na amekufa, nadhani ni muda mzuri wewe ku-enjoy na mkeo huyo wa kigamboni.

Anonymous said...

sara says:

ndugu zangu wake kwa waume mnaotoa mawazo yenu humu, nadhani ingekuwa vyema kujitambua, nikimaanisha personal recognition maana inaonekana wengi mmeandika hapo maoni yenu ila kwa matusi, na dhihaka sasa sioni kama kweli kuna la faida sana katika amjidiliano hayo ya namna chafu. nawashauri ni vema kujadili mambo ya maisha katika mitazamo adilifu na yenye kuleta mabadiliko zaidiya kupoteza muda mwingi sana kuandika matusi na dhihaka ambazo kwa kweli kama sote tunaishi ni lazima tunakutana nazo.... jaribuni kutumia muda wenu vizuri kuelimishana na kureekebishana kiadilifu na kiheshima zaidi: itasaidia sana besides waliosema nobody is perfect hawakukosea hata kidogo. tunzeni muda