Wednesday, May 09, 2007

Mpakanjia sasa yuko Hoi!

Duh, ni majuto, maneno ya watu, mapenzi, au nini kinachomsumbua Bwana Mpakanjia?
Hivi majuzi kampa mke wake, Mheshimiwa Amina Chifupa, talaka na leo tunasikia yuko hoi kitandani! Mungu ampe nguvu maana mambo ya ndani yakianikwa hadharani yanaweza kuleta presha!



********************************************

From: http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/05/09/90143.html



Mumewe Amina hoi!



2007-05-09 Na Badru Kimwaga, Jijini

Siku chache tu baada ya `kumlima` talaka mkewe kwa tuhuma za kutokuwa muaminifu, katika ndoa, mfanyabiashara maarufu nchini, Bwana Mohammed Mpakanjia almaarufu kama `Meddy` imedaiwa kuwa hivi sasa yuko hoi bin taaban kitandani.


Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu mapema leo asubuhi, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mkandarasi wa kutengeneza barabara, amesema hivi sasa yu hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hakuweza kuyafichua.

19 comments:

Anonymous said...

So sad to see so many people discussing things which to say the truth there not in national interest does anybody discuss about president kikwete trips abroad and how much there have cost tax payers ,lately the goverment lost 242 tsh billions (20 Millions USD)that the auditor General discovered and send report to the parliament , now dont you people figure this to be more important than want Amina & Zitto did

Anonymous said...

Andikeni mambo ya kimsingi nyie bloggers sio ishu za amina chifupa!.Chemi andika vitu vya kusaidia taifa kuondokona na umasikini.Tumechoka na habari hizi.Badilika!

Anonymous said...

Jamani msiwahukumu hawa kina Chemi. Hawawezi kuandika mambo wasiyo na ufahamu na maslahi nayo. Wao wanachojua ni Chifupa, Mpakanjia, American Idol, Big Brother, n.k.

Tuwasamehe tu ila ndio upeo wao ulipofikia hapo. You can't get blood from a stone!

Anonymous said...

Mpakanjia amsihi Chifupa ajitokeze

HabariLeo; Thursday,May 10, 2007 @00:02

(http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=1566)


ALIYEKUWA mume wa Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), Mohammed Mpakanjia amesema kupeana kwao talaka isiwe sababu ya kumfanya mbunge huyo ajifiche na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya siasa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na HabariLeo Dar es Salaam jana, Mpakanjia alisema kupeana talaka ni jambo la kawaida katika maisha hivyo Amina awe huru kufanya shughuli zake za siasa.

Mpakanjia na Amina ambao wamedumu katika ndoa kwa miaka mitano na wana mtoto mmoja wa kiume wa miaka minne, walitalakiana Alhamisi iliyopita kwa sababu ambazo hazijabainishwa rasmi ingawa kuna madai yasiyothibitishwa kwamba ni saa chache baada ya Mpakanjia kudokezwa na Naibu Waziri mmoja madai juu ya mwenendo usiofaa wa mkewe.

“Anaweza kushindwa kufanya kazi zake nyingine na kujikuta anapoteza muda wake mwingi kujificha ama kutopatikana katika simu zake na sehemu muhimu anakotakiwa bila sababu za msingi,” alisema Mpakanjia ambaye kwa sasa anauguza majeraha aliyoyapata katika ajali ya gari iliyotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro.

Alisema anajisikia vibaya kusoma katika magazeti kuwa Amina anajificha ama haonekani mitaani, kutokana na tukio hilo, jambo ambalo anadai limekuzwa kupita kiasi.

Alisema kuwa suala la mtalaka wake ni la kijamii na kuwataka watu waliolirukia, kuliacha na kumuacha Amina, awe huru katika kufanya kazi zake. “Nisingependa kuendelea kuzungumzia suala hili, napenda kulifunga rasmi na Amina awe huru kufanya mambo yake ya kisiasa.

Mpakanjia ambaye alifanya mahojiano na HabariLeo katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo, Dar es Salaam, alisema licha ya talaka bado ana ushirikiano mzuri na familia ya akina Chifupa akiwamo baba na babu yake.

“Niko hapa kumpokea babu yake Amina. Nimelazimika kuja licha ya kuwa naumwa kwa heshima na mapenzi makubwa ya familia. Ningekuwa na kinyongo nisingekuja,” alisema. Wiki mbili zilizopita, Mpakanjia alijeruhiwa kwa kuungua sehemu kadhaa za mwili, baada ya gari lake kuwaka moto ghafla. Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser , liliteketea katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Mpakanjia, hakupenda kuzungumzia suala la kuwapo kwa barua aliyoiandika kwenda kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na kama alitaka lizungumziwe katika chama.

“Kama kutakuwa na suala la nidhamu kichama, litashughulikiwa kichama na vikao vyake. Tatizo ni dogo sana lisikuzwe na kuharibu ‘CV’ ya Amina. Nataka awe huru na shughuli zake za kila siku,” alisema. Pia hakupenda kuzungumzia zaidi suala la talaka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za ndoa ya Kiislamu ana nafasi ya kumrudia Amina endapo ametoa talaka moja.

Sheria ya ndoa ya Kiislamu, kuachwa kwa mke kwa talaka tatu ni ngumu kurudiana. Lakini mke huyo akiolewa na mume mwingine, kisha akaachika tena, mume wa kwanza anaweza kupeleka maombi yake tena na kumuoa upya. Lakini, endapo talaka moja itatolewa kwa mke na kuishi zaidi ya miezi, mwaka ama miaka bila kuolewa ama bila kupewa talaka nyingine mbili zilizosalia, inahesabika kuwa mwanamke huyo ameachika rasmi kisheria.

Kwa suala la matunzo ya watoto, sheria hiyo inamlazimisha mwanaume kumtunza mtoto/watoto. Ikiwezekana mke naye anastahili kutunzwa kama ana talaka moja ndani ya miezi kadhaa.

Katika moja ya vipengele vya kisheria, mume ataruhusiwa kuwachukua mtoto/watoto, endapo watatimiza miaka minane. Pia, haimzuii kuchukua mtoto/watoto kutoka kwa mwanamke, endapo itabainika kuwa hali ya mwanamke huyo kwa fedha ama maisha siyo nzuri.

Anonymous said...

Kuna habari zaidi ya American Idol,, na Chifupa wewe Anonymous mshamba wa 5:23am.

Anonymous said...

naungana na wadau hapo juu. Da Chemi, lete vitu vingine-hivi kweli huyu AMina CHIFUPA anastahili postings 2 katika siku tatu??

Anonymous said...

"Kuna habari zaidi ya American Idol,, na Chifupa wewe Anonymous mshamba wa 5:23am".

ZIKO WAPI HIZO HABARI MUMU? ALIFANYA JAMBO LA MAANA KUTUJUZA YANAYOJIRI HUKO CAMEROON KWA MAREHEMU WETU WA AJALI, ILA CHIFUPA KAIBUKA TENA(FRONT PAGE).

VP AMERICAN IDOL INAENDELEAJE? BIG BROTHER AFRICA INAANZA LINI TENA?

Anonymous said...

Anonymous wa 8:59am, hebu bonyeza kushoto kuna habari kibao. Acha USHAMBA wewe. Unaonekana MSHAMBA NAMBA WANI!

Anonymous said...

Mpakanjia sio Mpakanija kwenye kichwa cha habari.

Anonymous said...

Kuna uhuru wa kuandika kitu unachotaka, jamani anzisheni blog zenu za kisiasa na maendeleo,au topic mnazotaka sidhani mtamforce mtu aandike, hayo yawe maoni tu jamani

Anonymous said...

WATU MNAPENDA SANA KUJADILI KUHUSU WATU WENGINE NA VITU VYAO NA SIO NYIE NA VITU VYENU NDIO MAANA HATA MAJINA HALISI MNAFICHA MNAJIITA MARA TUPLIONYU, MUMU, N.K

WEKENI HABARI ZENU BASI ZIJADILIWE. HATA KAMA KILA MTU ANA UHURU WA KUANDIKA ATAKACHO LKN KWANINI ASIWE MAISHA YAKE MWENYEWE HAPA HADI ANASHILIA BANGO MAISHA YA WENGINE?

Anonymous said...

Wabongo wapo tayari kutukana wenzao na kuwaita majina ya ajabu ili mradi tu waandelee kuwasakama na kuwajidili wenzao huku wao wameficha sura zao. Kila umtukanae ujue nae pia anaweza kukutukana kama hivyo au hata zaidi.

Amina/Mpakania/Zitto/Nchimbi ni mambo ya umbea tu ambayo hayamsaidii mtu asiyehusika nayo kitu chochote!

Anonymous said...

Na wewe anonymos wa 4;45pm kwa nini kuhutumia jina lako??? Hebu jibu! Unasema maanonymous kumbe na wewe mwenyewe umo. Hata haya huna! Hebu nyamaza!
Bora ya mumu, mlalahoi, tuplionyo, etc. wamejipa majina!

Anonymous said...

Nikitumia jina au nispotumia siwezi kuja kumtukana mtu hapa. Naweza kuwatukana watu ovyo tu ila sio mila na desturi yangu. Nashangaa anaejibu hizi hoja sio Chemi. Tangu mwanzo mimi namsakama Dada Chemi ila watu wengine wamejifanya wao Chemi wanajibu; haya "kina Chemi" endeleeni kujibu.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 5:47PM, you are right, people should be discussing things that are more important like government financial losses. However, as you can see people love gossip. That is just human nature unfortunately. Why are government and parliament officials even commenting on this?

Na kwa wengine, naomba tuwe waungwana katika majibu hapa kwenye blogu yangu. Asanteni.

Anonymous said...

Jamani welcome to the planet Earth!!

Anonymous said...

Ahsante Chemi kwa majibu mazuri. Umeonesha ustaarabu na ukomavu mkubwa; sijaona umemtusi mtu wala kujibu kwa jeuri/dharau kama wachangiaji wengine. Lakini wao mbona hawajifunzi toka kwako? Waelimishe zaidi na ikiwezekana weka hoja kuhusu watu wanaoandika matusi/kejeli/dharau ktk blogs!

Lk dada Chemi sakata la ndege ya KQ linaendeleaje? Najaribu kutafuta sana ila media nyingi hazilizungumzii tena naona!

Wikiendi njema kwa kila mtu!

Cheers!

Anonymous said...

Hivi ndugu zangu wananchi lile sakata la Rada limeishia wapi? nihabarisheni mana nimeachwa nyuma kidogo.

Pia mikataba ya madini kwa makaburu kuingia nchini mwetu imekaaje? swali kwa Rais

maryam K

Anonymous said...

kila mtu binafsi anaweza kufungua blogs yake kwa malengo maalu. ikiwa mtu amejipangia blogs yake iwe kwa ajili ya starehe au elimu au siasa au mazingira au chengine chochote basi musimlazimishe kuingia katika sehemu ambayo hajajipangia ila mnaweza kumpa maoni. mnajua baadhi ya maoni niliyosoma ambayo yanamkandia dada Chemi yanaweza kumvunja moyo. sisi wengine tunatembelea blogs yake ikiwa topic tunapenda tunasoma na ikiwa hatukuipend tunairuka. nanyi mngejifunza kufanya hivyo.
mbona hamjaizungumzia blogs ya mikundu na matusi kwa kuweka hadharani mambo ambayo hayastahiki kidini kadhalika kijamii. kwa kuwa aingiae kapenda mwenyewe basi naye mungemwacha afanye apendacho ila tu mwaweza kutoa ushauri.
ah bora ungefanya hivi kuliko hivi itapendeza zaidi? au mnasemaje wenzangu? tuweni wastaarabu sio.