Monday, May 28, 2007

Flaviana afika Top Ten - Miss Japan ashinda!






Kwanza nampongeza Miss Tanzania, Flaviana, Matata kwa kufika katika Top Ten (kumi bora) ya mashindano ya Miss Universe. Ingawa hakufika katika Top 5 atafika mbali maana mabilioni ya watu wamemwona. Pole zake Miss USA, alianguka jukwaani kwenye evening gown segment.

Nilijua Miss Japan atashinda. Alivyopita na swimsuit yake alivyokuwa anatingisha matako, kwa swing, macho yote yalikuwa kwake. Flaviana alivyovaa ili bikini niliona kama ana aibu fulani, bora angetembea kama anacheza ngoma watu wangemshangilia. Flaviana alijitahidi sana lakini kuna wakati niliona kama alikuwa nervous hasa pale kwenye Evening gown, na hata mwanzo walivyokuwa 77 na alikuwa jukwaani.

Lakini kunyoa kipara kilimsaidia kwa kiasi fulani, ila ingekuwa vigumu ashinde awe Miss universe maana moja wa wadhamini wakuu ni kampuni inayotengeneza manukato ya nywele. Miss Jamaica naye alishindana na nywele za rasta.

Lakini leo jioni waTanzania tuliweza kujivunia si mchezo, maana ni mara ya kwanza kuona Miss Tanzani anafika mbali kiasi hicho katika hayo mashindano. Naomba Flaviana akirudi Tanzania afundishe na atoe ushauri kwa wasichana wengine kuhusu jinsi ya kushiriki katika hayo mashindao na kushinda.

Natumaini Trump Model Agency watampa contract.

8 comments:

ngono said...

Hongera sana flaviana kwa kufika mbali!

Anonymous said...

Naungana na Ngono hapo juu pamoja na wabongo wengine kumpa hongera Flaviana.

Mie nafikiri kunyoa nywele kuliondoa alama, wengine mnasemaje??

Anonymous said...

mlalahoi, definitely kipara kilisaidia. Ili ile gauni ilimponza! Angekuwa katika Top 5!

Anonymous said...

Kwa kweli nimefurahi sana kwa bi Flaviana kufikia hatua ya juu kiasi kile. I got tearly watching. Mlalahoi,
ni kweli Kunyoa nywele ilikuwa ni mbinu nzuri sana ilifanya adraw attention!Sasa achukue contract yake ya nguvu aanze kujilia nchi.Ana ngozi nzuri , smooth, Mungu amjalie tuje tumuone kwa kina Revlon na Cover girl.
Subira.

Unknown said...

Nakupongeya sana Dada Chemi kwa blog zako hii, pia nampongeya Dada zetu Flaviana kwa kufika hatua hii kumbuka ni mara za kwanya kwa TZ kuingia ktk mashindano haya makubwa za urembo kumi bora si padogo hongera sana Flaviana. nimekuwa nikifuatilia kwa karibu ushiriki wake na kuweka ktk blog ya www.bernardrwebangira.bolgspot.com waweza kuivinjali. nisalimie USA: CIAO

Anonymous said...

Chemi unasema miss Japan ulijua atashinda kwa sababu alitingisha matako. Flaviana naye angetingisha yake tena ya kibongo.

Wazee wa matako makubwa mnasemaje?????? mpo

FC

Anonymous said...

tako na nywele bwana!!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 12:15, ukipata nafasi utazame tena mwondoko wa Miss Japan. Yeye ni professional Model na alionyesha wazi kuwa anajua jinsi ya kumudu ile Catwalk.