Saturday, May 12, 2007

Miss Universe 2007 - Je, atakuwa Flaviana Matata wa Tanzania?




Kwa kweli mwaka huu nangojea kwa hamu siku ya May 28th. Siku hiyo NBC itonyesha Live mashindano ya Miss Universe itakayofanyika huko Mexico City.

Mwakilishi wa Tanzania, Flaviana Matata yumo. Kwa kweli weusi kutoka nchi zingine wana weave na wigi kichwani, lakini yeye kanyoa upara! Kama vile kusema, napenda uafrika wangu! Naomba afike mbali katika hayo mashindano.

Na hata kama hata pita msishangae mkisikia kuwa amepata modelling contract, au yuko kwenye matangazo ya magazeti na TV. Sasa hivi hao models weusi wa kiafrika ni mali kweli hapa. Washukuru akini Alek Wek, na Iman kwa kupendwa waafrika katika u-model hapa USA. Zamani ilikuwa model mweusi lazima awe mweupe karibia ya mzungu na awe na nywele ndefu!

Black Beauty juu! Waafrika tujipende!

6 comments:

Anonymous said...

namtakia kila heri huyu Binti. Ushindi wake ni kitu kizuri kwa nchi yetu.

Anonymous said...

Flaviana ni mzuri kuliko Cynthia Masasi! Naweza kununua kalenda ya Flaviana.

Anonymous said...

Grace.
binti ni mrembo mno, tumuombee tu afikie malengo.

Anonymous said...

Chemi kuna haja ya kujifunza kutoa heshima kwa huko ulikochota picha, ni ustaarabu mdogo unahitajika.

Huyu mrembo kiboko, ana mambo ambayo warembo wengi wa Tanzania hawana. Yeye ukimuona tu unahisi umeona model wa nguvu, tofauti na wengine hasa wale wa Hashim Lundenga ambao ukimuona unahisi umeomuona Maimuna.

Wamenikera kwenye website ya Miss Universe ulikoiba picha, wamekata kalio lake, nina hakika ndilo lililompa ushindi wa tano pamoja na kwamba pozi lake halijawahi kutumiwa popote duniani.

Huyu demu bomba.

Anonymous said...

kutokana na hilo vazi alolivaa mi naona bora angeingia jukwaani kama alivyozaliwa ili apendeze zaidi

Anonymous said...

Sijui hata lakusema ila kusema ukweli binti huyu ni mzuri kweli kweli yaani anavyote na yuko natural so i hope all the best atashinda.