Thursday, May 24, 2007

Mshindi wa American Idol 6 ni Jordin


Natoa pongezi kwa Jordin Sparks aliyeshinda American Idol 6 jana. Ana miaka 17 tu na anasoma darasa la 11 (Form 3). Ni mshindi mwenye umri mdogo kuliko wote waliowahi kushinda.

Baba yake ni mcheza footbal (American style) mweusi, na mama ya ni mzungu. Huyo Jordin ni mrefu na ana mwili. Alifmfanya Ryan Seacrest aonekane kama pygmy kwake.

Kwa uimbaji, sijamfurahia sana. Ila aliimba vizuri kuliko aliyebaki, Blake, kijana wa kizungu aliyependa kutia ma beatbox kwenye nyimbo zake.

Wenye sauti nzuri Melinda na Lakisha walitolewa wiki kadhaa zilizopita. Wanasema watazamaji wa America Idol walipungua kwa vile show mwak huu haikuwa nzuri. Nsiyohaikuwa nzuri, maana walitoa waliojua kuimba mapema. Wengi walikuwa wanaume weusi. Tungojea January 2008, kuona American Idol y itakuaje.

8 comments:

Anonymous said...

Da chemi nilidhani ulisema hauta kaa uangalie american idol tena baada ya Melinda kutolewa. Imekuwaje au ilikuwa mkwara tuu

ngono said...

Hongera sana kwa jordin! Check out this blog - http://pichazangono.blogspot.com

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 12:36Am, niliangalia dakika kumi za mwisho. Ila nilisikitika sana kutoiangalia maana nasikia Lakisha na Melinda waliimba na Gladys Knight! Watu wanasema hiyo sehemu ndo ilikuwa show. Lakini ukweli Season 6 haikuwa nzuri na huyo Jordin bado sijaona ana nini zaidi kwenye kuimba.

Anonymous wa 11:39Pm asante nitakaribia. Yeah, hata mimi nilifyatilia habari za hiyo Catfight. Na Rosie hajarudi bado!

Anonymous said...

Huku UK tumeona fainali hii jana usiku itv2!!! Thanks chemi, maana nilikuwa tayari nimeshamjua mshindi kupitia swahili time!!

Sheria Ngowi. said...

Da chemi Jordin anasauti sana na ni mdogo na anapersonality na najiamini sana akiwa anaimba mi naona ni sawa tu alivoshinda nimefurahi sana

Anonymous said...

hata mimi nimefurahia Jordin kushinda badala ya Blake. Najua ana-uchangamfu ambao utamsaidia kuuza santuri (record) nyingi. Hata sauti yake sio mbaya sana.
Natumaini Melinda, Lakisha na Stephanie Edwards watabahatika kupata mikataba kutoka kwingine. Cheers Chemi.

Anonymous said...

jinsi gani inaonyesha sisi watu weusi pia tuna kaubaguzi. Kwa kushindilia kimaoni kuwa wale weusi wawili walioshindwa ndio wanaostaili kushinda. It just shows how bigots some of us are, the girl just handled the rest of 'em all fair and square. You gotta swallow it n' move on. Stop whining about 'em two loser black girls. They lost, yeah, we know it, if they 're good still they're gonna get contracts, like uh Jeniffer Hudson - The dream girl.
Jordin is young , beautiful,talented and biracial what's wrong with that che-mponda? . Y'know entertaiment industry is all about a completed package n' there they got it.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 1:09PM, I have nothing against Jordin winning. She was the better of the remaining two by far. But I do think that she was not the best singer overall.