Friday, May 11, 2007

Wanamlaumu Rubani - Kuanguka kwa Kenya Airways Flight 507


Bado uchunguzi unafanywa kuhusu kuanguka kwa ndege ya Kenya Airways huko Cameroon. Kwa sasa wanamlaumu Rubani hiyo, marehemu Capt. Francis Mbatia Wamwea. Wanasema huenda aliamua kuondoka kwa vile ilibidi abiria wawahi connections Nairobi. Marubani wa ndege zingine mbili zilizokuwa pale uwanjani wa Air Moroc, na Cameroon Airlines waliamua kusubiri.

Mimi sikuwepo lakini huenda aliamini kuwa kwa vile hiyo ndege ni ya kisasa kama wanavyoisifia 'Ultra-Modern' haiwezi kuanguka. Tusisahau kuwa meli ya Titanic ilizama 1912 wakati walisema haiwezi kuzama kwa vile ilikuwa 'Ultra-Modern' kwa wakati huo. Lakini siku yako ya kufa ikifika, imefika! Hakuna cha Ultra-modern wala nini. Kila ukipanda ndege au hata kuingia kwenye gari lako ni kuomba ufike salama.

Lakini bado hawajapata Black Box ya Cockpit ambayo itatoa habari zote na maneno ya hao rubani. Maskini ya Mungu msaidizi wake, Andrew Kiuru, alikuwa ana miaka 23 tu. Alikuwa amemaliza kusoma urubani Afrika Kusini mwaka jana.

Habari zinasikitisha kweli. Moja ya abiria waliokufa alikuwa Mtaalam wa UKIMWI, Dr. Albert Henn, wa Harvard University.

Kwa habari zaidi soma:

http://seattlepi.nwsource.com/local/6420AP_Cameroon_Planes_Last_Moments.html

http://allafrica.com/stories/200705110439.html

4 comments:

Anonymous said...

Wala hawajamlaumu rubani, uandishi wako unaonesha jinsi waandishi wa Tanzania walivyo na upeo mdogo, sasa kilikushinda nini kuelewa kwenye Kiingereza rahisi kile? Walichoeleza ni hali ilivyokuwa na maamuzi aliyochukua rubani. Kama rubani amelaumiwa, ni nani amemlaumu, hebu mtaje?

Pili, katika mazingira yaliyoelezwa na jinsi Boeing ile inavyosifiwa, na kuchelewa kulikotokea, kuna dalili kwamba rubani alifanya maamuzi ya haraka, pengine akidhani ubora wa ndege yake na uzoefu wake vinaweza kushindana na majanga ya asili kama mvua ya kimbunga.

Sitashangaa kusikia kuwa ni yeye aliyesababisha, kwa sababu kubwa tatu:
1. Ilishawahi kutokea mwaka 2000 rubani wa KQ alifanya makosa na ndege ikajitosa baharini. Kwa kufuata mwenendo wa kesi mahakamani, kama mtu au shirika lina historia ya kufanya kitu zaidi ya mara moja, inaweza kutumika kama kigezo cha kutoa hukumu kwa kuzingatia tabia.
2. Wakenya wana kiburi, ni wajuaji, mathalani wanadai eti wao ndiyo shirika kubwa Afrika la ndege, hivi Afrika Kusini na Ethiopia wako wapi? Kwanza wao wanamilikiwa pia na mashirika mawili ya Ulaya, wenzao ni wenyewe tu. Wamezidi Wakenya.
3. Kwa nini wenzake walikacha kuruka yeye akinyanyuka? Kitendo cha wengine kuminya si cha bure.

Jifunze kudadisi ukisoma.

Anonymous said...

Ahsante dada Chemi kwa kusikia kilio changu na kutuwekea tena hii habari. Kwa uandishi wa ile habari ya Seattlepi naona lawama zimeelekezwa kwa rubani wa ile ndege.Huu ni mtazamo wangu wa ripoti ya hiyo media.

Lakini nachelea kuhukumu sasa hivi kwani naona bado ni mapema mno. Kadri uchunguzi wa kitaalamu utakavyokuwa unaendlea kufanywa basi hapa kati kati mengi yatazuka; nasubiri nione!

Bravo Chemi!

Anonymous said...

Sio kwamba uandishi wa Tanzania ni mdogo ni kwamba yeye amejaribu kuelezea kilicho kwenye makala ile kwamba inavyoonekana kwa sasa Rubani ndie mtuhumiwa kwakuwa ni kwanini wenzake waligoma kwenda ila yeye akaamua kwenda?
hapa mwandishi kutumia kichwa cha habari "Rubani alaumiwa," isikuchanganye mzee ni aina ya uandishi wenye kuleta mvuto wakutaka kujua nini kiko ndani ya habari hiyo hasa.Bigup.from Ch,kessy

Anonymous said...

yeah, naona anonymous no. 1 umechemka kidogo kwa kumshambulia Chemi, nafikiri message yake imeeleweka kwa wengine. Ciao