Thursday, May 17, 2007

Kwa Heri Melinda! American Idol IMEOZA!

American Idol imepoteza watazamaji wengi baada ya kutolewa kwa Melinda Doolittle (29) jana.
Waliobaki sasa ni kijana wa kizungu Blake na shombe Jordin. Blake sijapenda staili yake maana anaimba huko anafanya ma beat box, halafu Jordin basi tu ndo wiki hizi za mwaisho ndo kajitahidi sana lakini sijaona kama anasthahili kushinda.

Nimechukia sana kwa sababu hakuna wiki tangu walivyoanza kuonyesha msimu huu kuwa Melinda alikosea wimbo. Ana sauti nzuri ajabu na majaji wote walikubali hivyo. Yeye kati wa wote waliochaguliwa katika Top 24, ndiye alishahili kushinda.

Lakini mshndi anachaguliwa na watazamaji. Na tunajua kuwa bado kuna ubaguzi Marekani. Ukiingia kwenye bodi ya American Idol utaona wanavyotukana waimbaji weusi. Insikitisha kweli kweli.

Haya tuone nani atashinda wiki ijayo, lakini mimi sitazami. Nitaona matokeo kwenye taarifa ya habari. Kwa nini nipoteze muda kuangalia watu wasiostahili kuwa Idol wawe pale? No nitangalia Sopranos reruns! Huenda Tony ataweza kuwawahack hao producers wa show!

Msimu wa sita wa American Idol umeoza kweli kweli.

For the benefit of non Swahili speaking readers, I say that American Idol is rotten and stinks! Is it a talent contest or a popularity contest?

6 comments:

Anonymous said...

Unajua da chemi kwa huyu msichana ndipo nimeamini kuwa mwanamke ni uzuri wa tabia au moyoni. Huyu mwanamke si mzuri sana ila kwa moyo aliouonyesha idol au sijui ni mimi pekee ila namzimia. Kuna mvuto tuu anao kuzidi hata hao waitwao wazuri

Anonymous said...

hii show haina maana kabisa, wanaojua kuimba wote walitolewa (Lakisha, Melinda, Stephanie Edwards), bahati mbaya wote ni weusi. Nafikiri wangebadilisha ikawa kama Dancing with the Stars ambao watu watatu wanaingia finali-hii ingesaidia kutoua morale wa watu kama Melinda!! Angalau Jordin anajua kuimba, ila sitashangaa kama Blake atashinda-watchout!!

Anonymous said...

Blake anaweza kushinda kwa sababu kuna VOTE WHITE bloc. Hawataki mweusi ashinde hebu fnaya sechi kwenye neti.

Anonymous said...

why waste your time watchin' this non-sense and get all fired up?

Anonymous said...

hili dada chemi alikuwa akilizungumzia kama kuna weusi na weupe mkawa mnamwambia aaa hay0o mambo yamepitwa na wakati, sasa si mnaona.mwacheni aelezee anachokijua msiwe mnamkera mara kwa mara eti aaa huo ushamba mara vile mara hivi mwisho wenyewe mnaingia kichwa kichwa.

Anonymous said...

ubaguzi upo

uko sahihi che mponda.