Thursday, May 10, 2007

Kwa Heri Lakisha!


Jana kwenye American Idol, Lakisha Jones alitolewa kwenye mashindano. Kwanza nashukuru kuwa aliweza kufika mpaka kuwa namba 4! Nilikuwa na wasiwasi angetolewa mapema maana wtau walikuwa wanamwita 'Fantasia Part 2' kwa vile ana mtoto. Na kwa kweli sikufurahi kuona Simon Cowell anampiga busu kwenye mdomo wiki iliyopita. Nilijua wazungu watachukia kuona hivyo. Wengi hawajui kuwa mchumba wa Simon Cowell ni mweusi.

Watu wanasema kuwa Show siyo nzuri mwaka huu, kwa vile waimbaji wengi hawana sauti za kuvutia mno kama za mastaa. Nalaumu majaji wa American Idol kwa sababu kulikuwa na waimbaji wzuri lakini hawakuchaguliwa. Kulikuwa na vijana wengi wa kiume wenye sauti za ajabu, lakini hata hatukuwaona kwenye finals! Badala yake walichagua wahuni kama yule malaya Antonella, na Sanjaya asiyeweza kuimba kusudi ratings ziwe juu. Watu wamechukia na ratings zimeshuka! Wameahidi mwaka kesho watakarabati jinsi wanavyochaga waimbaji.
Kwa kweli Lakisha ana suaiti nzuri, anaweza kushindana na Jennifer Hudson. Nina imani kuwa atenda mbali. Tutasikia ana contract hivi karibuni.

Bado wiki mbili za mashindano. Je, mshindi atakuwa Blake, Melinda au Jordin?

Ningependa kuona Melinda akishinda. Kwa kweli ana sauti nzuri mno na hakuna wiki aliimba vibaya.

6 comments:

Anonymous said...

Da Chemi hebu nawe sasa anza kumpigia debe miss Universe wetu Flaviana nasikia kila mtanzania anaweza kumpigia kura ili kumweka katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi.Nyumbani ni nyumbani hata kama si kuzuri ni TMK hao.

Anonymous said...

Nitammiss Lakisha, lakini sorry sidhani kumwita Antonella malaya ni Fasida nzuri na sidhani kama ni kitu cha uhakika, kuna vitu vilikuzwa juu yake.

Anonymous said...

Antonella ni malaya! Umeona ile picha aliyopiga uchi na wasichana wengine akiwa Spring Break? Anasema oh, I was young! Ndo kisingizio cha kufanya umalaya.

Anonymous said...

Mumu acha ushamba,kupiga picha uchi kwetu waafrica ni mbaya kimaaadili yetu ila watu wa magharibu ndo mambo yao mi siwalaumu.

Anonymous said...

Chifupa sasa ataanza kumsakama Mpakanjia na habari za madawa ya kulevya,maana si inasadikika huyu ndugu at some point in life ndiyo ilikuaga issue yake

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 8:32am, nimekusikia, ila tatizo sina access ya website yao. Kesho naona nitakuwa nayo.