Saturday, July 12, 2008

Mboga za Majani huko Chang'ombe

Bustani za Mboga za Majani Chang'ombe
Wanamwagilia kwa 'can'

Maji Machafu huko Chang'ombe karibu na hiyo bustani...ndo wanachotea maji ya kumwagilia

Bustani ya mboga za majani Chang'ombe


Mdau wa Joseph N. Kutoka Dar es Salaam kaniletea picha hizi za mboga zinazomwagliwa na maji machafu huko Chang'ombe, Dar es Salaam. Kitu gani kinaelea juu ya hayo maji? Na hao wanaotumia kumwagilia wanadhani mchanga unatosha kuwa 'filtration system'?

"Rejea makala uliyo post 'Mboga za majani zaua Dar" kuhusu mboga za majani. Nimeamua kukutumia pix za moja ya sehemu dar eneo la chang`ombe jirani na uwanja mpya wa taifa. Sijajua hasa nini kinapita kwenye mtaro huo sijui mazagazaga ya kiwanda cha serengeti bia au vinyesi ndio wana palilia mboga then watu wanakula, duhh hii ni sumu tena kali sana ina ku kill soft taratibu." - Joseph N.

5 comments:

Anonymous said...

Doh hizo kemikali kwenye maji zinachemka. Kweli kungefaa kuwe nawakaguzi wa mashamba huko Dar. Tunalishwa sumu si uongo!

Anonymous said...

Ungeyaona kwa macho hayo maji yanayomwagia hizo mboga, somo wala usingezila hizo mboga.
Sijui yanatoka kwenye hicho kiwanda cha bia hapo karibu, au ni maji ya kwenye vyoo?
Walimaji wenyewe wanaingia ndani ya hayo maji mwili mzima na wanayachota kwa keni, hawana hata wasiwasi.
Sijui hatima yao itakuwaje?

Anonymous said...

Hao wanaomwgili wako hatarini kupata kansa ya ngozi na kansa zingine. Kweli hayo maji hayafai.

Anonymous said...

Maji kuwa machafu aimaanishi ya kuwa ni mabaya . Bila ya kufanya laboratory analysis nakujua composition ya hayo maji it will be totally unfair to say those mbogas are not fit for human composition.

It is not the color that one should be skeptical about but rather the chemical compostion .

Anonymous said...

Kutazama kwa macho tu inatoahs akujua haya maji hayafai. Rangi hiyo ya ajabu hatokei natural.