Thursday, July 03, 2008

Mandela au Mandingo?

Cheki CNN walivyomtusi Mzee Mandela wiki iliyopita. Kwa hapa Marekani 'Mandingo' ni mwanaume mweusi anayetembea na wanawake wa kizungu. Wanawake wa kizungu wanapenda akina mandingo kwa vile eti wamejaliwa chombo/ume 'kikubwa'.

Asante Da Subi kwa kunistua na habari hii:

Inaelekea kuna mtu alifanya uandishi kutumia 'auto complete' wakati wa kazi halafu akalibandika tu alimradi...Afadhali CNN wameondoa na kurekebisha maana ingekuwa si njema.Dah, akikosewa jina Mandela sisi akina Chipiliro wa Akapungwamchanye sijui itakuwaje.Tizama kipande cha picha nimekiambatanisha hapa.


2 comments:

Anonymous said...

Nakumbuka hata Sen. Obama walishawahi kumwita O's'ama tena mbele yake. Kuna mtu alikuwa akimkaribisha kuongea!
Ila Obama alisema palepale kuwa huwa inatokea mara kwa mara tena kwa makusudi ili kumchafulia jina!
(Nadhana Chemi uliiona hiyo ktk tv)
-Mosonga

Anonymous said...

yeah ni kweli siku hio na mimi niliona kwenye taarifa ya habari jamaa mwandishi akajitia kuomba msamaha kufanya kama vile ulimi uliteleza vile pambaf hawa!!