Wednesday, July 09, 2008

Siti Binti Saad 1880-1950 - Kumbukumbu


Bibi Siti Binti Saad ni mmoja wa waanzilishi wa Taarab nchini. Alitokea Zanzibar, na aliweza kuimba katika lugha za kiarabu, kihindi na Kiswahili. Alikuwa mwimbaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutengeza santuri za nyimbo zake. Studio ilijengwa Zanzibar kwa ajili yake.

Alitengeneza santuri 150 (78 rpm). Si rahisi kupata nyimbo zake siku hizi.
Siti alikuwa mtoto wa watumwa. Alizaliwa huko Fumba, Zanzibar 1880 na alikuwa na maisha magumu hapo mwanzoni kabla ya kuwa mwimbaji maarufu. Alifariki dunia siku ya Julai 8, 1950 na kuzikwa kesho yake huko Zanzibar. Bi Kidude ni mwanafunzi wake.

Karibuni mtembelee website niliyotengeneza siku nyingi kuhusu historia na maisha ya Bibi Siti Binti Saad.

No comments: