Wednesday, July 23, 2008

Msiba wa Mzee Kizigha

Mwandishi Mwandamizi wa Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) wachapishaji wa gazeti la Daily News na HabariLeo, Charles Kizigha, akiwa amebeba msalaba baada ya Ibada maalum ya kumuombea Marehemu Baba yake mzazi, Mzee Thomas Marijani Kizigha ambaye anatarajiwa kuzikwa wiki hii nyumbani kwao Usangi mkoani Kilimanjaro. Imepangwa asafirishwe kesho kwa ndege. Kwa picha zaisi tembelea Michuzi Blog.

*************************************************************

Nimeona hii habari ya mziba wa Mzee Kizigha kwenye Michuzi blog. Nilifanya kazi na mwanae Charles Kizigha, miaka mingi Daily News. Kwa kweli lazima nimpe pole Kaka Charles maana ni majuzi tu alifiwa na mama yake mzazi. Msiba ni msiba lakini kufiwa na wazazi wote wawili katika kipindi kifupi duuh. Poleni familia.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema mbinguni. AMEN.

2 comments:

Anonymous said...

Pole sana familia ya Kizigha. Mungu amlaze mahala pema mbinguni. Amen.

Anonymous said...

nimesoma habari za msiba wa mzee wetu Kizigha kwenye blog ya Michuzi roho imeniuma sana kwa sababu ni juzi juzi tu tumemzika mama yetu mama kizigha pale usangi jamani familia poleni sana. tunaambiwa tumshukuru Mungu kwa kila jambo. poleni sana sana na Mungu awatie nguvu. mimi ni jirani yenu pale Majengo moshi