Monday, July 21, 2008

Survival Sisters aka. Choka Mbaya Sisters

Kutoka Haki Ngowi Blog:

Walipokuwa wanaingia kwenye‘game’walikuwa wanajiita ‘Choka Mbaya Sisters’,wakafanikiwa kutoka na albamu yao ya kwanza iliyokuwa na jina la ‘Yatima’, lakini kunako mauzo wakala za uso na kuambulia jina kidogo tu, Mariam Mndeme anashuka nayo zaidi.

Sasa wanajiita ‘Survival Sisters’,huku mkononi wakiwa na albamu ya pili waliyoipa jina la ‘Tukiwezeshwa Tunaweza’.Nawazungumzia mabinti watatu, Irene Malekela, Lucy Samsoni na Latifah Abdallah wanaoonekana pichani ambao wamesema na ShowBiz kwamba,sasa wako tayari kwa utambulisho wa albamu hiyo utakaofanyika Agosti 26,ndani ya ukumbi wa Dar West Park,uliyopo Tabata,Dar es Salaam.

Zaidi wasanii hao wenye ulemavu wa viuongo ambao hivi sasa wanafanya vyema kupitia ngoma yao yenye jina la ‘Siyo siri’,iliyomshirikisha Dully Sykes,walisema kwamba mastaa kibao wa Bongo Flava wamejitolea kuwapiga tafu siku hiyo,wakiwemo Profesa Jay,Fid Q,Dully na Mr.Blu na wengine kibao.”Siyo wasanii hao tu, pia makampuni na watu binafsi wamejitolea kutusaidia kama Global Publishers,Morgan Sound,Dotnata Decorations, Screen Masters na Times FM.Habari hii na Mdau Abdallah Mrisho Salawi.

7 comments:

Anonymous said...

Wasichana wazuri kweli hao!

Anonymous said...

Nimempenda yule wa nyuma!

Anonymous said...

yule msichana wa nyuma pale anafanana na Chemi...yaani ka photocopy. duh...kweli duniani zaidi ya wawili wawili...

Anonymous said...

Yule wa nyuma mbona anafanana na da Chemi? We anony hapo juu kama umempenda yule wa nyuma basi nimekuelewa kwa da Chemi....

Anonymous said...

Jamani yule wa nyuma mbona kafanana sana na wewe dada Chemi ni ndugu yako? au ni macho yangu tu.

Chemi Che-Mponda said...

LOL! Labda ni ndugu yangu.

Anonymous said...

Mungu na awajaalie katika safari yao ya muziki. Ni vijana wazuri wanaojituma bila kujali hali yao. Je ni wangapi tulio wazima lakini tumebweteka tu? Wanastahili recognition kubwa kwani wanawazidi hata vyangudoa wanaodai hakuna ajira ndo mana wanajiuza.

Big up sana Survival Gals.. Tuko Pamoja