Sunday, July 27, 2008

Ubatizo Revere Beach - IGC

Leo, waumini wawili wa International Gospel Church walibatizwa na kuazaliwa upya katika jina la Bwana Yesu huko Revere Beach.Iko karibu na uwanja wa ndege wa Logan hapa Boston . Waumini Lillian na Faith, walibatizwa leo mbele ya umati na waumini wa kanisa. Bahati mbaya kulikuwa hakuna jua hivyo picha hazijatoka vizuri.
Waumini Lillian na Faith (Morine) wakiwa na wasimamizi wao kwenye ibada. Walitambulishwa mbele ya kanisa kabla ya kwenda baharini kubatizwa

Waumini wa IGC wakifika Revere Beach Lillian na Faith wakiwa na Pastor Jared, wakiombewa kabla ya kuingia kwenye maji



Baadhi ya waumini wa IGC kwenye ibada ya ubatizo

Pastor Jared ndani ya maji akingojea wanaobatizwa

Lillian akjiandaaa kubatizwa

Lillian alisema maji ni ya baridi

Faith akiomba kabla ya kubatizwa
Faith akibatizwa

Tulivyokuwa tunabatiza wazungu waliangalia kwa mshangao wengine walichangia katika kusema, 'Amen' na Halleluyah!
Baada ya Kubatizwa

2 comments:

Anonymous said...

Bwana asifiwe sana, aaminiye na kubatizwa ataokoka. wamechagua fungu lililo jema
Ms Bennett

Anonymous said...

Bwana asifiwe. Ni visuri kuna hao mabinti wazuri wamepokea bwana Yesu kama mwokozi wao. halleluyah!