Wadau, jana jioni nilenda kwenye makaburi ya Forest Hills hapa Boston kwenye Tamasha la Taa. Ni sherehe ya kukumbuka wafu. Watu wanaandika ujumbe kwenye karatasi maalum kwa wapendwa wao waliofariki na zinawekwa kwenye 'lantern' Ni mbao ambao inaweza kuelea kwenye maji. Katikati ya makaburi hayo kuna ziwa ndogo na 'park' sehemu ya kupumzika na kufanya sherehe.
Tuliburudishwa na wanamuziki wanaoimba nyimbo za injili na wacheza ngoma kutoka China na Japan. Giza ilivyoingia watu waliweka hizo 'lantern' taa kwenye maji ya Ziwa Hibiscus. Ilipendenza sana kuona mataa yanaelea juu ya maji, huko bata wanaogelea kwa mshangao kuna nini leo.
Bahati mbaya giza iliingia na sikuweza kupiga picha nzuri. Zingine zimetoka nyeusi kabisa!
*************************************************
The Lantern Festival
Once a year, Forest Hills hosts the Lantern Festival, an extraordinary community event attended by 3,000 people in 2000. Inspired by Buddhist traditions, this non-denominational ceremony offers a magical way to remember family and friends. After enjoying a program of music and dance, people inscribe the paper shades of simple wooden lanterns with greetings. At dusk, we light the lanterns and watch them float across Lake Hibiscus, bearing their messages to the world of the spirits.
Kwa habari zaidi za Forest Hills Cemetery Bofya hapa:
Kwa habari zaidi za Forest Hills Cemetery Bofya hapa:
No comments:
Post a Comment