Thursday, August 28, 2008

Afande Chemi!

Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.

Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba. Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.

Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room. Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.
Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.
Haya nitawapa updates.

Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

15 comments:

Unknown said...

Wow!!! That's so cool! Total Knockout crew yashiriki katika furaha yako. Congratulations dada Chemi. Na hizo uniform zimekupendeza kweli kweli!

Anonymous said...

Chemmi! You are really going places! Please Keep it up the good work so one day Bongoland will have a REAL Hollywood Star of its Own!
CONGRULATULATIONS!!!

Anonymous said...

so what the big deal?

Unknown said...

Hi Da Chemi,
Congrat. U look like realy cop, keep your dream alive Chemi and one day we gone have a Hollywood super star from Bongo.

We do hope so.

Anonymous said...

Hongera sana Chemi. Kwa kweli nimefurahi sana kuona maendeleo yako!!
kila la heri, ila chunga wasije-kuona na kamera (usije poteza unga bure!)

Anonymous said...

Well done, keep it up! Slowly but surely, you'll get there!

Anonymous said...

Habari chi??? Naona unafanya vizuri lakini uwe unajitahidi kuepuka kuweka picha kabla movie haijatoka ...

Go sister!!!!!!

Che Esha.

Anonymous said...

Hongera nyingi sana and wishing you all the best. Magwanda yanatisha lakini ni poa tu.

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wote.

Che Esha, mimi ni extra (background artist). Kazi yetu ni kufanya scene ionekane kama tukio ni kweli. Mfano huwezi kukuta stelingi anatembea barabarani peke yake. Lzima kutakuwa na watu wengine. Au akiingia ofisini haiko tupu, lazime kuna watu wengine mle. Hiyo ndo kazi yetu extras. Ni nafasi nzuri ya kujifunza kabla ya kuingia kwenye principal, yaani wale ambao unawaona wanaongea. Kuna utaratibu kwa kucheza sinema hapa Marekani.

Anonymous said...

Da Chemi utafika! Moyo unao na wanaanza kuona juhudi zako. Keep it up girl!

Anonymous said...

wabongo bwana,
sasa we huruhusiwi kupiga picha, halafu unajificha dressing room unapiga na kuibandika hapa online ili uchukue ujiko sindiyo?
sifa zinaua kumbe hujakua wewe?!
Play smart dont risk your career for unnecessary popularity
sasa wabongo nuksi wasiopenda maendeleo ya wenzao wakichukua hiyo picha wakamtumia Mel Gibson si kimeota na umevuruga career yako kwa tamaa ya sifa
Watch your back and be smart, sio lazima ujitangaze watajua tu kama ni kitu kikubwa unafanya otherwise it's a good start!
ni hayo tu

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:30PM, ngoja nikusahishe. Ninakushukuru kwa concerns.

Haturuhsiwi kupiga picha kwenye set, yaani pale wanaposhuti filamu na mastelingi walipo. Unaweza kupiga dressing room na sehemu ya kungojea. Ndo maana picha ambazo nabandika hutaniona kwenye action, hizo zitatoka kwenye publicity unit ya sinema wakitaka. Hiyo picha ya dressing room nimeshika camera mwenyewe kwa vile nilikua peke yangu mle. Nina picha zingine ambazo watu wengine walipiga lakini kwa sasa sibandiki.

Hizi picha siyo kuwa natafuta sifa, bali nawajulisha nafanya nini na pia kutoa moyo kwa waTanzania wenzangu kuwa inawezekana.

Anonymous said...

Dada Chemi uko juu.husikatishwe tamaa na wasio penda maendeleo ya wenzao.Mungu akusaidie uwe juu zaidi

Anonymous said...

Hongera sister,
lakini wanayosema hawa wadau wachache ni kweli na wanakutakia mema tu,wanataka wakuone uko mbali zaidi,na mimi nakushauri,usiwe unaweka picha hadi pale sinema inapotoka,hata kama ulikuwa peke yako,tayari umeshatuonyesha mavazi yao,ni sawa na kukiuka maadili,je kama walikuwa wanataka kusuprise watu kwenye movie kuwa kutakuwa na polisi mwanamke mnene wa kiTZ sasa wewe umeshatoa siri yao.mi pia nakushauri usiweke picha kwanza hadi mambo yawe tayari,kama hautaunekana,basi utatuwekea kuwa ulikuwepo na ulifanya haya lakini bahati mbaya sikutokea.

Pia kutujibu humu haipendezi kabisa wewe tulia tu wadau wabishane wenyewe,tutakuwa tunaogopa kuweka komenti zetu kwa kuhofu mwenye Blogu atatushushua,kama hauko au uko sawa wewe uchune tuu na ujirekebishe kimya kimya haina haja ya kutujibu au kujibishana,wewe ni mwandishi wa habari tena wa miaka mingi so haya utakuwa unayajua,
Ni hayo tuu,
Nakutakia kazi njema na Nakupenda

Anonymous said...

Sasa si unaona TK kakuweka kwenye matangazo Chemi ndani ya movie ya edge and nini nini sijui,sasa wenyewe labda hawajaanza kujitangaza wewe tayari unajitangazia,mimi sio kwamba nayamaindi hayo maatua yako lakini naona utajiharibia bure dada yangu na mimi nataka nikuone Holiwudi badae babakeee