Nimeona hizi picha kwa Michuzi Jr. (Jiachie Blog). Huyo mshiriki wa Miss Utalii alikuwa kwenye ziara. Ghafla alianguka. Wanasema kuwa harufu ya dawa wanazotumia kiwandani zilimwangusha. Inawezekana. Ila navyofahamu hizi pageant za urembo, mara nyingi mtu akianguka hivyo ni shauri ya njaa. Hao wagombea wanakula kidogo sana au hawali kabisa kusudi wakonde au wabakie wembamba. Wakati mwingine wanapata dehydration (ukosefu wa maji mwilini) na utapiamlo. Inatokea sana kwenye pageant za Marekani. Lakini kwa Bongo huenda ana malaria. Pole sana Sara Salum.
Mshiriki wa miss utalii 2008 Sara Salum kutoka Dodoma akipewa sapoti ya kutembea na baadhi ya wasimamizi wa walimbwende hao waliofika kushuhudia kazi za uchapaji ndani ya kiwanda cha Image Printer,kilichopo Nyerere road jijini dar. Moja ya washiriki wa miss Utalii Tanzania 2008, Sara Salum 25, Dodoma alidondoka katika ziara ya kutembelea kiwanda cha Image Printer leo mchana baada ya kuzidiwa na kemikali zinazotumika katika masuala ya uchapaji kiwandani hapo. (Picha kutoka Michuzi Jr. Blog)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
8 comments:
Maskini! Mwembamba mno huyo. Mbona huyo mnene anayesaidia anaonekana kama anafuraha na afya? Acheni kujikondesha kama mgonjwa wa UKIMWI jamani.
Anon wa August 30, 2008 3:27 PM, asante sana kwa ONYO hilo kali!
Acheni kuiga wazungu jamani akina dada. SIsis waafrika tunapenda akina dada waliojaa. Kati ya huyo Sarah na huyo mnene mimi namchagua mnene kama mzuri!
Mrefu,hips kidogo,nyuma kumejaa jaa sio kapigwa pasi,kiuno dondola,guu guu kweli sio fito.....popote pale wasichana wa bongo inasemekana ni vyuma hasa!
Hako katoto njaa tu, wakimpa chai kikombe hamalizi, atazinduka tu.
Njaa hiyo!
Mungu wangu! Au ana mimba huyo! Huenda kweli njaa ndo ilimwangusha.
wabongo kwa kupondana hatujambo. Haya, mi yangu macho! Pole dada
Post a Comment