Sunday, August 10, 2008

Isaac Hayes Afariki Dunia!

Mwanamuziki maarufu, Isaac Hayes, amefariki nyumbani kwake leo huko Memphis Tennessee. Alikuwa na miaka 65. Habari zinasema walimkuta amekishakufa pembeni mwa treadmill nyumbani kwake. Huenda alikuwa ametoka kufanya mazoezi.

Yaani ni jana tu Bernie Mac alitutoka. Leo kaondoka Isaac Hayes.

Isaac Hayes atakumbukwa hasa kwa kutunga ule wimbo wa 'SHAFT' (Shut your mouth). Wimbo wa Shaft uylimpatia Oscar pamoja na Grammy. Miaka ya 70 wimbo wa Shaft na sinema za Shaft ziliwapa nguvu weusi wa Marekani. Kwanza Shaft alikuwa ni mpelelezi mweusi, na huo wimbo ulikuwa staili aina yake.

Kwa habari zaidi someni:

http://ap.google.com/article/ALeqM5gsCUwiqAHCNIbxD6oePjCg1RToZQD92FOTRO0

REST IN PEACE!

2 comments:

Anonymous said...

Ninavyopenda wimbo wake wa Shaft. Huyo alikuwa na kipaji cha aina yake. Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. AMIN.

Anonymous said...

Eh bwana! Who is next? Hivi vofo vinakuja tatu tatu.

Rest in Peace Soul Man!