Tuesday, January 13, 2009

Bikira wa Miaka 107 Anataka kuolewa huko China!!

Leo ni siku ya mabikira!

Huko China, Bi Kizee Wang Guiying (107) anasema anataka kuolewa kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Anasema pia bado ni bikira.

Bi Wang, anasema kuwa alikuwa mwoga wa kuolewa kwa vile aliona wanawake walioolewa wakipigwa na waume zao. Alisema hakutaka maisha ya hivyo, hivyo alikuwa na shamba na aliamua maisha yake itakuwa ni ya kulima.

Ila sasa anakaribia kuwa na miaka 108 na amekuwa mpweke. Anasema kuwa sasa anataka mwanaume wa kukaa naye. Yuko tayari kumkubali kijana wa miaka 90 au hata 100! Huko China wasamaria wema wanamtafutia mume huko kwenye nyumba za wazee.

Na kuna watu wamesema itakuwa vigumu kwa Bi Wang kupata mume maana hao wazee wenye miaka 90 wanatafuta maspring chicken wenye miaka 70!

Kwa habari zaidi someni:

http://chattahbox.com/curiosity/2009/01/12/107-year-old-woman-seeks-husband/

http://www.telegraph.co.uk/news/worldnews/asia/china/4222884/Woman-107-seeks-husband.html

http://newsblaze.com/story/20090112100351reye.nb/topstory.html

No comments: