Sunday, January 25, 2009

Mwizi Ageuka Mbuzi Nigeria


Wadau, huko Nigeria mbuzi kashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuiba gari. Watu walioshuhudia tukio wanasema kuwa eti mwizi alitumia uchawi kusudi ageuke mbuzi wakati anakimbia kutoka kwenye eneo la tukio.

Nilidhani kuwa Tanzania tuna imani kubwa na uchawi kumbe hata huko Afrika Magahribi wamo!

Ujumbe kwa polisi huko. Na nasema hebu lete huyo mbuzi tumgeuze nyama choma! LOL!

*******************************************************

Goat Detained over Armed Robbery

LAGOS (Reuters) – Police in Nigeria are holding a goat on suspicion of attempted armed robbery.

Vigilantes took the black and white beast to the police saying it was an armed robber who had used black magic to transform himself into a goat to escape arrest after trying to steal a Mazda 323.

"The group of vigilante men came to report that while they were on patrol they saw some hoodlums attempting to rob a car. They pursued them. However one of them escaped while the other turned into a goat," Kwara state police spokesman Tunde Mohammed told Reuters by telephone.

"We cannot confirm the story, but the goat is in our custody. We cannot base our information on something mystical. It is something that has to be proved scientifically, that a human being turned into a goat," he said.

Belief in witchcraft is widespread in parts of Nigeria, Africa's most populous nation. Residents came to the police station to see the goat, photographed in one national newspaper on its knees next to a pile of straw .

6 comments:

Anonymous said...

inamaana ulikuwa hujui kama nigeria inaongoza kwa uchawi africa ikifuatiwa na southafrica.na imeshawahi kuripotiwa na aljazeera kuwa mauaji ya albino yalishamiri bongo kutokana na kuingia kwa movie nyingi za kinaigeria ambazo kwa asilimia tiisini ni zinaongelea uchawi.nadhani ni muda wa sherikali kuzuia movies zote kutoka nigeria kuziuza bongo,na kupiga marufuku waigizaji wa tz kutengeneza movies za kichawi,maana ndo zinawaharibu watu kwa imani za ajabu

Chemi Che-Mponda said...

Kama ni kweli sinema za Nigeria zinachochea mauji ya albino basi kuna haja ya serikali kuzizuia! Unakumbuka ile censorship board iliyokuwa chini ya Tanzania film Company enzi za Mwalimu? Wakati huo hatukusikia albino wanauawa ovyo na mambo mengine ya ajabu!

Anonymous said...

da chemi hivi na huko boston mbuzi choma ipo? maana bongo imezidi haswa dodoma kwetu na dar.

Chemi Che-Mponda said...

Hapa ukisema unakula nyama ya mbuzi watu wanakushangaa maana wanaona mbuzi kama pets. Unakumbuka kuna mbongo aliwahi kufungwa hapa kwa ajili ya kuchinja mbuzi nyumbani kwake? Siku moja moja unaweza kupata nyama ya mbuzi kwenye supermarkets. Lakini hasa ukiitaka nyama nzuri ya mbzuri inabidi uende Haymarket kwenye bucha za waislamu/halal.

Anonymous said...

Na mimi niko tayari kusaidia kumla!

Anonymous said...

dada chemi unakumbuka ile story ya mchaga aliiba mbuzi watu walivyomstukia akamuinua miguu ya mbele huku akisema na wewe masawe ukishalewa unalia kama mbusi