Wednesday, January 28, 2009

Makubwa Benki Kuu!

(picha ya juu kutoka Michuzi Blog)
Bank of Tanzania Personnel and Administration director Amatus Joachim Liyumba (R) and the bank`s Projects Manager, Deogratius Dawson Kweka,at the Kisutu Resident Magistrate`s Court in Dar es Salaam yesterday.


Watu wawajibike sasa huko Bongo! Hii Kali!

********************************************

Kutoka ippmedia.com

BoT Yatikiswa

2009-01-28 11:00:08
Na Richard Makore

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, jana alipandishwa kizimbani akiwa na mfanyakazi mwenzake wakituhumiwa kwa kosa la kutumia madaraka yao vibaya ya utumishi wa umma na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 221,197,299,200.95 kupitia ujenzi wa maghorofa pacha ya benki hiyo.

Sambamba na Liyumba, mwingine aliyesomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), John Lubangila, ni aliyekuwa Meneja wa Mradi wa ujenzi huo, Deogratius Kweka.

Watuhumiwa hao wawili walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana mchana wakiwa katika gari la Takukuru lenye namba za usajili T 319 ATD aina ya Toyota Land Cruiser la rangi ya kijani.

Aidha, kabla ya kusimamishwa kizimbani, watuhumiwa hao waliendelea kukaa ndani ya gari katika viwanja vya mahakama kwa takribani saa tatu, ndipo watolewa na kuingizwa mahakamani.

Baada ya kupanda kizimbani, ghafla watuhumiwa walianza kutokwa na jasho kali hali iliyowasababisha muda wote kujifuta kwa kutumia vitambaa vyao.

Aidha, waliingia kizimbani wakiwa wameshika chupa za maji na kutaka kwenda kusimama nazo wakati wanasomewa mashtaka, lakini askari polisi alitokea na kuyachukua.

Mbali na makosa ya kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha, pia walishitakiwa kwa kutoa maamuzi bila kushirikisha Bodi ya Wakurugenzi wa BoT pamoja na kukiuka sheria ya manunuzi ya serikali na sheria ya uendeshaji wa benki hiyo.

Mwendesha Mashtaka aliiambia mahakama kuwa walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2001- 2006.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Khadija Msongo, wa mahakama hiyo.

Hakimu Msongo aliiambia mahakama kuwa dhamana ya watuhumiwa hao ipo wazi na itatakiwa kutolewa thamani ya nusu za fedha zinazodaiwa kupotea.

Nusu ya fedha hizo ni sawa na zaidi ya Sh. bilioni 110 ambapo zikigawanywa kwa watuhumiwa wawili, kila mmoja alitakiwa kutoa fedha Sh. bilioni 55 au mali isiyohamishika inayolingana na kiasi hicho cha fedha.

Mshtakiwa namba moja, Liyumba, alianza kuwasilisha nyaraka za mali mbalimbali ili aweze kupata dhamana, lakini upande wa mashtaka ulioomba mahakama kusitisha zoezi hilo.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa unaomba hivyo ili upate muda wa kupitia nyaraka hizo ili kuona kama sio feki na zina thamani ya fedha zinazotakiwa.

Mahakama ilikubaliana na upande wa mashtaka na hivyo kusitisha dhamana hiyo na watuhumiwa kupelekwa rumande hadi Februari, 10 mwaka huu.

Majengo ya BoT yamekuwa ni gumzo kubwa nchini tangu wakati wa utawala wa awamu ya tatu, huku kukwa na taarifa kwamba ghama yake ni ghali kuliko ujenzi katika miji mikubwa ya mataifa ya magahribi. Hadi sasa inakisiwa kwamba ujenzi huo umekwisha kugharimu Sh bilioni 700.

SOURCE: Nipashe

2 comments:

Anonymous said...

Jamaa kazidi kujifanya all that sasa mwone!

Anonymous said...

Mzee Ruksa alikuwa na Fagio la Chuma. Hii sijui tuiteje!