Thursday, January 08, 2009

Sophia Simba Mwenyekiti Mpya wa UWT

Sofia Simba (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

Kutoka Lukwangule Blog:

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais Utawala bora, Sophia Mnyambi Simba ameibuka kidedea na kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM na kuwabwaga wagombea wenzake Janeth Kahama na Joyce Masunga.

Katika uchaguzi uliofanyika jana usiku na matokeo kutangazwa leo katika ukumbi wa kilimani na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Seif Khatibu, Sophia Simba aliibuka kidedea baada ya kupata jumla ya kura 470 sawa na asilimia 54.4 ya kura halali 862 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.

Janeth kahama alipata jumla ya kura 383 sawa na asilimia 48.4 huku Joyce Masunga akiambulia jumla ya kura 10 kati ya kura 862 zilizopigwa sawa na asilimia 1.1.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu mwenyekiti wa UWT taifa alikwenda kwa Asha Bakari Makame ambaye alikuwa mgombea pekee na hivyo kupigiwa kura za ndiyo na hapana ambapo alishinda kwa jumla ya kura za ndiyo 736 kati ya kura halali 815 sawa na asilimia 90.3 huku kura za ndiyo zikiwa ni 79 sawa na asilimia 9.7.

Naye Ofisa uhusiano wa Benki ya NMB, Shy Rose Bhanji aliibuka mshindi na kuukwaa uwakilishi wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM), toka UWT baada ya kuwabwaga wenzake watano kwa kupata jumla ya kura 499 kati ya kura 807 zilizopigwa huku Mbunge wa Viti maalum Martha Mlata aliibuka kidedea na kupata nafasi ya uwakilishi wa jumuiya ya wazzai toka umoja wa wanawake.

Kwa upande wa nafasi za wawakilishi wa baraza kuu la umoja huo upande wa bara waliochaguliwa katika nafasi hizo ni pamoja na Magreth Mkanga, Betty Malanga, Ellen Magoha, Amina Msenza na Sifa Swai.

Wawakailishi wa baraza kuu la UWT upande wa Zanzibar waliochaguliwa ni pamoja na Zulekha Yunus Haji, Lilian Grace Limo, Catherine Peter Nao, Subira Mohamed Ali na Latifa Nassor Ahmed.

Akiongea baada ya matokeo hayo kutangazwa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UWT taifa, Janeth Kahama alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa mgumu sana na kwamba ulikuwa na rafu nyingi na matusi yalitawala.

“Mimi sina ugomvi na mtu ila ninamuomba radhi sana mume wangu kwa matusi ambayo nilikuwa natukanwa kupitia simu nisamehe sana mzee mwenzangu “ Alisema.

Aliwaomba wanachama wa umoja huo kumpa sapoti mwenyekiti mpya kwa kuwa bila wanachama hakutakuwa na uwt imara na kuongeza kuwa yeye atakuwa tayari muda wowote ambapo mwenyekiti mpya atamuhitaji.

2 comments:

Anonymous said...

Hivi hawa viongozi wana muda wa saa ngapi kwa siku kuweza kufanyakazi ya u-Waziri na u-Mwenyekiti na "biashara" nyinginezo pembeni?

Kiongozi mmoja; wadhifa mmoja!

Achieni na wa-Tanzania wengine nao wapate "maisha bora"!

Circulation of the elite iko wapi?

Anonymous said...

Kapata njia ya kupata mshiko mwingine! Hivi amefanya nini cha maana akiwa waziri?