Thursday, May 29, 2008

Ajali ya Treni Boston

Marehemu Terrese Edmonds



Wadau, hapa Boston mwezi huu kumekuwa na ajali kadhaa kwenye usafiri wa treni. Juzi kulitokea moto kwenye njia ya kupita treni chini ya ardhi (subway) maeneo ya Park Street. Bahati mbaya ilitokea rush hour wakati watu wanatoka kazini. Nilipata shida sana kufika nyumbani siku hiyo lakini nilifika.

Jana, maskini kwenye Green Line, treni mbili ziligongana. Kwa bahati nzuri ajali ilitokea karibu mwisho wa njia hivyo watu wengi walikuwa wamekwishashuka. Bahati mbaya, dereva wa treni iliyogonga lingine, alifariki. Watu zaidi ya kumi waliumia na ilibidi wapelekwe hospitalini kwa matibabu.

Dereva ametambulika kama Bi Terrese Edmonds alikuwa na miaka 24. Ni Mmarekani mweusi. Na tayari wanaanza kuelekeza chanzo cha hiyo ajali kwa Bi Terrese. Kuna watu amabao wanadai alikuwa anatumia cell phone yake wakati anaendesha treni. Maiti haiwezi kusema ilitokea nini.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

Jana stesheni za TV zote za Boston walikluwa na live coverage ya ajali na jitihada za kumwokoa Bi Edmonds. Kwa muda mrefu MBTA waliktaa kusema hali yake, ndipo nikahisi kuwa huyo dada alishakata roho.

Baba yake mzazi alikuwa kwenye TV akisema kuwa anamtafuta binti yake, ni dereva wa treni amepita hospitali kadhaa kumtafuta na hakumpata, simu yake hapokee. Alisema aliamua kwenda kwenye ajali baada ya kuambiwa na mfanyakazi mwenzake Terrese kuwa yeye ndiye alikuwa anaendesha hiyo treni.

Baba yake aliwaambia waandishi wa habari kuwa binti yake alipenda sana kazi yake na alikuwa ameifany kwa miezi sita tu. Nilichukia sana kusikia waandishi wa habari wakimchimba huyo mzee kuhusu habari zake binafsi. Mfano, je, una kaa na mama yake? Jamani! Mtu ana huzuni na wasiwasi halafu mnaanza kumchimba tena kwenye TV!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.necn.com/Boston/New-England/Area-hospitals-prep-for-victims-of-train-accident/1212016597.html

2 comments:

Anonymous said...

Dada yangu chemi ukishakuwa na ngozi nyeusi huku ni gundu tushukuru mungu angalau na siye tunatoka Afrika marorosa polisi wanatuona bado tuna kiwi cha macho lakini african americans wanapatashida sana ndio maana hasira zao wanahamishia kwetu. Nao siku wakiamua watatuchoma moto kama wasoza kule sauzi lakini inshaalah mungu ameshatunusuru kwa mengi . Tuombe mungu Obama alete mabadiliko ingawa hatujui hatma ya uhai wake itakuwaje. Pamoja na rangi yetu kunyanyasika sijutii hata kidogo!

Anonymous said...

Chemi ujue unafanana sana na marehemu Terrese Edmonds.
Mungu amlaze mahali pema.