Huko Bongo Celebrity kuna Mahojiano na Msanii/Mrembo Miriam Chemmoss.
Kutoka Bongo Celebrity:
Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).
Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho.Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza.Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.
Kama ilivyo kwa wasanii wengi,safari ya Miriam katika ulimwengu wa sanaa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi mdogo.Lakini ni pale alipohamia jijini New York mwaka 2004 na kujiunga na kundi maarufu lililojulikana kama The Marvallettes Revue lililokuwa chini ya Pam Darden, ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara ipasavyo. Baadaye alijiunga na kundi lingine maarufu la Soukouss Stars kama mwimbaji pekee wa kike na mnenguaji kabla ya kuamua kuimba peke yake(solo artist) mwaka 2006.
Kwa upande wa uigizaji,Miriam ameshaigiza katika show mbalimbali maarufu ikiwemo ile ya “District” katika kituo maarufu cha televisheni cha CBS.Pia ameshiriki katika “Bedford Diaries” ya Warner Bros.Sauti yake imetumika katika matangazo mbalimbali ya biashara kama vile Western Union(USA-African Market) nk.Kwa upande wa mavazi Miriam amewahi kuwa model wa jeans za Levi’s,Getty Images/Brazilian Salsa Club(Print),Bebe Noir Clothing Line,New York nk.Mwaka 2007 mtandao wa Jamati.com ulimtaja Miriam katika orodha yao ya Top 10 Sexiest African Women akiwa ni miongoni mwa wasichana wawili kutoka eneo la Afrika Mashariki.
BOFYA HAPA KUSOMA MAHOJIANO NA MIRIAM CHEMMOSS
http://bongocelebrity.com/2008/05/18/one-on-one-with-miriam-chemmoss/#more-1417
5 comments:
tumeshaona kule bongo celebrity
Dada chemi naomba nikuulize kitu.Uku nyumbani wadada wengi wanapata tabu sana ya kufanikisha malengo na ndoto zao kwa kile kiitwacho 'Nipe nikupe'.Je uko hali ikoje?Ninauliuza hilo kwa sababu ukiangalia story ya huyo dada Miriam Chem inaonyesha wazi kwamba kama angekuwa huku nyumbani nahisi angekuwa alishazeeshwa na watu wanaoitwa wadhamini mara promotor na mafanikio kama haya yasingepatikana.Kuna mifano mingi ya wasichana hapa Bongo wenye vipaji lakn wanaumizwa na mapromota tu.
I agree with the person above! Just look at Flaviana Matata she is also on that Top 10 Sexiest African Women List you mentioned.
Anonymous wa 4:37am, umeuliza swali nzuri sana. Nakubaliana na wewe kuwa warembo huko Bongo wanakuwa epxloited. Yaani unaweza kukuta mrembo yuko 'penniless' hajalipwa lakini Promota anafaidi matunda ya mteja wake.
Issue ni kuwa hii business ya Fesheni/Sinema bado ni changa Bongo. Kumbuka miaka mingi yalipigwa marufuku. Je, kuna regulations Bongo kwa mamodels na actors? Sheria gani zinawalinda? Promoter anakuna regulated namna gani? Je, hao models wanajua promoter kapata kiasi gani?
Hapa USA kwa kawaida Agent anapata 15% na Promoter anapata percentage pia. Lakini pia anakuwa na gharama zake mfano kama kamnunulia nguo, kamlipia usafiri etc. Hata hivyo hakuna sababu ya Mrembo Bongo kuwa penniless. Nilisikitika sana nilivyokuwa Bongo mwaka jana na kusikia habari ya hiyo exploitation.
Teshi, I agree Flaviana Matata is one of Africa's beauties and the world has taken note.
Kwa kweli huyo dada ni mzuri. Mrembo hasa.
Post a Comment