Saturday, May 17, 2008

Zimamoto Kazini Cambridge Leo III

Karibu na napokaa kuna nyumba ulianza kuunga moto. Bahati wameiwahi. Tunasikia harufu ya moshi. Zimamoto na polisi wamefanya evacuation ya nyumba karibu na pale. Nyumba iliyoungua iko karibu na sehemu ya kufua nguo (laundromat) mtaani River St.


Gari ya Polisi ikizuia magari kupita mtaa wa Pleasant St. kwenda River St.
Gari ya Polisi ikiuia magari kupita River St. Hiyo basi No. 70 ilikwama hapo hapo! Abiria walishuka na kutembea kwenda Central Square. Zimamoto juu ya nyumba inayoungua River. St.

Mzimamoto akivaa nguo zake haraka kwenda kuwasaidia wenzake
Gari ya Zimamoto, Chifu wa Zimamoto wa Cambridge ni yuke aliyevaa koti ya njano
Fire Hydrant (Bomba la maji) ambayo walitumia kupata maji kuzima moto. Wadau Mareknai mnajua ni mwiko kuegesha magari mbele au karibu sana na hydrant maana utapata faini kali! Iko kwenye kona ya River na Pleasant St.



Yalikuja zimamoto kutoka vikosi vyote vya Cambridge






Zimamoto walipanda kwenye fire escape ya hiyo nyumba Pleasant St. na kucheki kama kuliwa na watu ndani. Waliamuru watu wanaokaa block yote ile ya Pleasant na River watoke kwenye fleti zao kwa usalama wao.

7 comments:

Anonymous said...

Da Chemi naona leo umefanya reporting.

Wadau hebu ona hela ya walipa kodi Marekani inapoenda! Inaenda kenye huduma kwa wananchi. Wananunua vifaa vya zimamoto safi. Hebu ona mji wa Cambrodge siyo kubwa lakini wana vofaa vyaa kisasa na magari kadhaaa ya zimamoto. Dar es Salaam ni mji mkubwa sana, tuna engine za zimamoto ngapi?

Da Chemi nimecheka kuhusu Hyrdant! Bongo watu wangezigeuza mradi kama zingekuwa na maji!

Anonymous said...

Anony wa kwannza nakubaliana na wewe. Bongo tuna safari ndefu sana!Niliona ktk moja ya blogs last week nafikiri, fire wameenda ilikua K'koo km sikosei, wamefika gari halitoi maji! Kai ipo sana kwa nchi zetu za kiafrika!

Anonymous said...

Mimi niliwahi kupaki gari mbele ya hydrant somewhere hapa USA! Sikujua sheria, niliona space tu. Kurudi gari ilikuwa towed. Towing fee na fine ilikuwa karibu dola $300! Ziheshimu hydrant zinaokoa maisha. Na ni kweli Bongo zingegeuzwa mradi kama zingekuwepo!

Anonymous said...

kusema ukweli,dar au tanzania nchi ya mwisho kwa kufuatilia huduma za kimiji na jamii,kusema ukweli.mwalimu nyerere anastahili kuheshimika katika historia ya tanzania baada ya uhuru,yaani enzi ya mwalimu nyerere fire brigade zilikuwepo mikoa yote,ambulance cars,town buses..sasa hebu tuangalie hizi awamu za 2.3,4, zimeleta nini?hasa katika hudumu kama hizi za maji,fire brigades,umeme?n,k very very shamefull,mimi naona hata aibu kujiisifia eti bongo tambarare,hiyo tambarare.tunayojidaia ni ipi hata huduma muhimu hatuna?nchi toka tumepata uhuru hakuna hata zoezi la kutoa vitambulisho vya wananchi?tanzania ni nchi pekee aina national identies,kwa raia wake?ni aibu.yani warundi,wasomali,waethiopia.na wengine wanaishi kiolela na kupewa hata ardhi kulima au kujenga ovyo ovyo,sababu huwezi kumjua ni nani ni mzaliwa halisi,sababu hatuna national identity cards kama kenya,jirani zetu.shame shame kwa taifa letu ambalo limeshafikisha 47 years of independence,hata fire brigade cars hakuna,ambulance.town buses hakuna..inshalllha tunakuomba mola turejeshe musa wa israel aje kutukomboa.

Anonymous said...

Hivi kweli habari hii iko "relevant" na mimi mdau wa kigilagila? au ndo ubishololo wa maisha mnayoishi huko kwenu?

Anonymous said...

Wala wasilete hayo magari ya zimamoto! Kwanza mkuu wa Kikosi angekuwa anitumia kupeleka maji nyumbani kwake na kwenye nyumba ndogo zake. Kama moto inatokea kweli unakuta gari halipo! Na kweli hydrant zingekuwepo watu wangezigeuza mradi! Mzungu anasimamia kidogo, akiondoka mambo yameharibika!

Anonymous said...

Hao wanalipwa vizuri pia. Kuna watu amabao wanagombania hizo kazi. Bongo tunalipa zimamoto wetu kiasi gani?