Wadau, nimeona hii picha kwenye blogu ya Michuzi. Anasema hii ni vazi la kitaifa la akina mama. Siyo mbaya, na ina lubega. Naona kama kitambaa ni kaniki iliyo pambwa na bendera. Lakini mshono si mbaya kwa kweli.
Mnaoinaje?
Blogs in Kiswahili, the main African language of EAST AFRICA.
5 comments:
Siyo Mama Salma Kikwete huyo? Na yule si Kikwete amekaa kwenye kochi?
Da Chemi siku hizi umekuwa modo!
mi nadhani aliekaa kwenye kochi ni Bernard Membe waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
Jamani naomba kufahamishwa!ivi kwani vazi la kitaifa tanzania ndilo hilo kweli au ni just kilibambikiza tu.je kweli ndilo vazi rasmi la wanawake wa tanzania au?na nani kasema?vipi kwa wanaume?
Tanzania hatuna vazi la taifa as such, kama vile Ghana, Nigeria na nchi nyingine......
Kuvaa nguo iliyo na bebdera ya TZ haina maana limekuwa vazi la taifa, au labda tuseme khanga ndoo vazi letu.... Maoni yangu
Post a Comment