Wednesday, May 21, 2008

Dr. Daudi Balali Amefariki!

Habari kutoka ippmedia.com zinasema kuwa aliyekuwa Gavana wa Beni ya Tanzania, Daudi Balali alifariki dunia siku ya Ijumaa iliyopita tarehe 5/16/08 huko Washingtom D.C.. Atazikwa Washington D.C. kesho. Sasa hii siri aliyotake kufichua ni upi? Naona kazi ya wapelelezi umeisha. Wanaweza kurudi Tanzania na kupeleleza mambo mengine.

****************************************************************
Kweli Balali kafariki!

2008-05-21

Na Mwandishi Wetu, Jijini


Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, BOT, Dokta Daud Balali amefariki dunia. Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyake nchini na huko Marekani, zimethibitisha kuwa Dk. Balali alifariki dunia Ijumaa iliyopita.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa Dk. Balali alifariki baada ya mashine iliyokuwa ikimsaidia kupumua kuondolewa. Aidha, vyanzo hivyo vimedai kuwa kabla ya kifo chake, Dk. Balali aliandaa ujumbe mzito, ambao ndani yake umeanika ukweli wote kuhusiana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikielekezwa kwake, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na kashfa ya upotevu wa mabilioni ya pesa za nchi kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.

Alasiri imeambiwa na vyanzo hivyo kuwa Dk. Balali alimkabidhi ujumbe huo wenye siri zote ndugu yake mmoja anayemuamini na kumpa maelekezo ya namna ya kuufikisha kunakohusika na hatimaye Watanzania kujua ukweli wa suala zima.

Hata hivyo, chanzo hicho kimedai kuwa hadi sasa haijafahamika ni ndugu yupi ameachiwa ujumbe huo. Imedaiwa zaidi na chanzo hicho kuwa Dk. Balali aliamua kuandaa ujumbe huo wenye siri zote kwa vile hakutaka achafuliwe peke yake wakati wahusika wa sakata hilo wapo na anawafahamu.

Aidha, imedaiwa alikuwa akisema kuwa hakutaka aondoke na siri nzito kuhusiana na yote aliyokuwa akielekezewa kidole. Dk. Balali alifukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete baada ya uchunguzi uliofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernst &Young kubaini upotevu wa Shilingi Bilioni 133 zilikuwa zimechotwa BOT kupitia EPA wakati wa uongozi wake.

Dk. Balali alienguliwa nafasi ya ugavana na Rais wakati akiwa nje ya nchi kwa matibabu na tangu wakati huo, hakuwahi kurejea nchini mpaka umauti ulipomkuta. Habari zinadai kuwa Dk. Balali anatarajiwa kuzikwa keshokutwa huko Jijini Washington DC, Marekani.

SOURCE: Alasiri

3 comments:

Anonymous said...

Dead men tell no tales. Lazima wamemkolimbaditto huyo!

Anonymous said...

Hakuna lolote,

Hilo watoto wa mjini tunaita ni "CHEZO" limechezeka,

Hapo inatafutwa maiti ya mtu mwingine na kusingiziwa ni ya Balali kisha watu wanazika,

Kwa kua ni Muislamu hakuna mambo ya kuacha sura wazi

Then Jamaa anahamia kwengine na hakuna atakaemjua na ndio wa mwisho wa skendo wa EPA,

Na serikali itawajibika kwa hili suala,

Kwan imemuachia mpaka kafariki (kama kweli)

Inasikitisha kwa Taasisi nyeti kama ikulu kudai kua balali alikua hatafutwi kwani si muajiriwa wa serikali na hana kesi ya kujibu mpaka tuhuma dhidi yake zitakapothibitishwa,

Huu ni uhuni na utapeli wa kisiasa,
kwani ye ndie mtuhumiwa mkuu wa skendo la EPA, iweje asishitakiwe mpaka eti tuhuma zithibitike??

Plse michuzi, Nasisitiza tena, KAPUNI NO

Anonymous said...

Sikubali! N'goo! Tunataka kuona maiti yake! Iweje azikwe marekani? Hata ni fixi tu anachukua identity mpya, ukute anaitwa Solomon Goodman na anakaa Idaho kwa raha mustarehe na pesa zetu!