Friday, May 09, 2008

Karibuni Kwenye Sherehe ya Kuadhimisha Miaka 10 - International Gospel Church, Boston MA

Pastor Jared Mlogecha na Mke wake Gisele Mlongecha


Wadau, kanisa letu hapa Boston, The International Gospel Church inasherekea miaka 10 tangu ianzishwe. Kwa wanaokumbuka Askofu Kakobe alikuja kubariki kanisa letu. Karibuni kwenye sherehe. Pia tunafanya mkutano mkuu May 22-25. KARIBUNI!

****************************************************************************

Pastor Jared and Mrs. Gisele Mlongecha, together with the Family of the International Gospel Church invite you to join us as we celebrate our ‘10th Year Anniversary’. Our Annual Conference also coincides with our Anniversary. WELCOME!

Dates:
Thursday, May 22, 2008 – Sunday, May 25, 2008

Venue:
International Gospel Church
85 Crescent Avenue
Chelsea, MA 02150

For more information call: 617-884-1951
*************************************
HARVEST RAIN MIRACLE CONFERENCE
PROGRAM


Thursday, May 22nd, 2008
6:00pm – 9:00pm Revival Service

Friday, May 23rd, 2008
9:00am – 2:00pm In Depth Biblical Teaching
6:00pm – 9:00pm Miracle Service

Saturday, May 24th 2008
9:00am – 2:00pm Workshops
Couples, Singles, Youth (Teens)
6:00pm -9:00pm Miracle Service

Sunday, May 25th, 2008
10:00am – 1:00pm Worship Service

Anniversary Celebration
6:00pm - 10:00pm
Sit Down Dinner
Live Concert featuring Les Mas, Wimbo Mpya
and IGC Worship Team

Suggested Donation
Adults $20.00 Children $10.00

6 comments:

Anonymous said...

Kero za makanisa marekani ndiyo hiyo.Hata kuingia kanisani kuhudumiwa lazima ulipe kiingilio cha lazima wenyewe wanaita donation.Hivi mpagani akiona hilo tangazo na kiingilio atakuja kweli?

Kwa uchunguzi wangu makanisa yote yasiyotoza watu viingilio kwenye huduma zao kama Katoliki,Lutheran,Assembiles of God,Anglikan n.k yana washirika wengi na yamesambaa dunia nzima kwa kasi wakati ya matajiri wakubwa wa marekani kama Cleflo Dollar,Benny Hinn,Kenneth Copeland,Kenneth Hagin,Oral Roberts,T.D.Jakes n.k yako marekani tu pamoja na pesa walizonazo hayajasambaa kufikia miji na vijiji ikiwemo Tanzania.

Yesu angekuwa anacharge viingilio kwenye huduma zake kanisa lisingesambaa dunia nzima kama ilivyo leo lingekuwa la watu wachache na lingefia huko alikozaliwa bethlehemu.

Anonymous said...

Anonymous 4:32am acha ushamba. Hiyo siyo admission fee. Ni mchango na si lazima utoe kama huna usitoe kitu. Ndo maana inaitwa suggested donation.

Anonymous said...

Kama siyo fee kwa nini waweke kiwango? kama ni sadaka ya kawaida wasingeweka kiwango.Mtu angekuja na sadaka yake akatoa.

Ilikuwa nije lakini siji kwa sababu ya hiyo suggested donation labda muiondoe kwenye hilo tangazo ndipo nitakuja.Si kwamba hela sina ninazo kibao lakini napinga kitendo cha kuweka viingilio kwenye makanisa yanapofanya huduma. Viingilio hivyo viitwe fees au suggested donation au lolote napinga na siji.

Anonymous said...

Inawezekana kuna kutokuelewa hiyo sugested donation. Naamini kua imekusudiwa kwa ajili ya sit down dinner together with the concert ambayo inafanyika Sunday night. I have been to every single one of the conferences that this church has hosted and I have not seen them charge fees for people to hear the word of God dispite the fact that watumishi wanaohudumia wanatoka Tanzania and sometimes nchi nyingine za nje ya Marekani. Watumishi kama Bishop Kakobe, Mtumishi Mwakasege, mchungaji Hiza, to name a few wameshiriki in some of the conferences in the past, these things cost money!. Sijui ndugu nyie mmeshiriki kiasi gani kwenye shughuli za makanisa hapa Marekani, lakini kila kitu kinalipiwa na sio hela ndogo ndogo, kuandaa a sit down dinner with the perfomance ya wanamuziki kama Les Mas all the way from Belgium sio bei rahisi. Siamini kama kanisa litawakataza watu kuingia incase hawatakua na fedha but suggested donation is there for people who are open to chip in. Hili kanisa limeshakua na shughuli mbalimbali including the famous Krystaal Band from Canada perfomances ambazo kama ingekua ni watu wasio wa kanisa wangeweza kuchaji kiingilio lakini sijawahi kuona mtu hata mmoja akizuiliwa.
Just come on down to Boston! You will be so blessed, you would wanna give a twenty!!
Be blessed and stay blessed!
Mantissa

Chemi Che-Mponda said...

Asante Dada Mantissa kwa maelezo mazuri. Tutaonana kwenye Conference.

Ni kweli hakuna kiingilio na hakuna mtu ambaye atarudishwa mlangoni shauri ya kutokutoa donation. Ni kweli hiyo donation ni ku offset bei ya chakula, usafiri na gharama zingine.

Wote mnakaribishwa.

Anonymous said...

You can win the argument but not win the person whom you argue with.