Sunday, May 11, 2008

Happy Mother's Day





Wadau,

Nawatakia akina mama wote sikukuu njema ya Siku ya Mama (Mother's Day). Wote tuna mama, hebu tazama kitovu chako hiyo ndo linki ya daima kati ya wewe na mama yako.

Nani kama Mama? Hakuna. Kumbuka ulivyokuwa unaumwa, ulivyoanguka na kuanza kulia, aliposota kukupatia mahitaji yako. Alivyokuwa anakulinda usiumie.

Na kitu kingine, akina mama wengine wanaumwaga wakiwa na mimba. Mimi moja wao. Halafu uchungu wa kuzaa (labor pains) ndo usiombe. Wanasayansi wanasema kuwa mwanaume hawezi kusika maumivu makali kama sisi wanawake tunavyosika kwenye uzazi. Ajabu tukimwona mtoto, tunasahau!

Leo umkumbuke Mama yako, kama uko mbali umpigie simu. Umnunulie zawadi ya shukurani kama unaweza, kamtembelee. Kama ametangulia kwenye mahala pema mbinguni umwombee.
Happy Mother's Day!

AKINA MAMA OYEEEEE!

6 comments:

Anonymous said...

oyeeeeeeeeeeeeeee

Anonymous said...

Akina Mama Oyee!

Simon Kitururu said...

Tukumbuke pia mama wa kambo WAZURI na wenye sifa za unyanyasaji na mama watupao watoto vilevile kama tunataka kuukubali ubinadamu

Anonymous said...

Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Anonymous said...

Haya mambo ya Mothers day sijui fathers day sio utamaduni wetu. Naomba tuwakumbuke mama zetu kwenye fikra na kila kitu kila siku sio kungojea siku maalum. Kama ulivyosema Chemi kitovu chako ni ushahidi kila unapokiona umkumbuke mama yako. Na kama zawadi usisubiri eti hadi mwezi march. Hayo waachieni wamarekani.!!

Anonymous said...

OYEE!