Friday, June 15, 2007

Halahala mnaosema mtoto si wako!




Miaka mingi nimeudhika sana na tabia ya wanaume kukataa watoto wao. Wanatembea na mwanamke, anapata mimba, na wanasema si wakwao. Mwanamke anabisha, na wanasema oh huyo mwanamke malaya katembea na wengine, huyo mtoto si wa kwangu. Nasema Shenzi Taipu mkome tabia yenu mbaya!

Halafu ndugu wanasema oh, sijui tungojeee tuone mtoto anafanana na nani. Loh, je kama mtoto anafanana na mwanamke na ndugu zake ndo mmepata kisingizio. Eh he! Si nilikuambia huyo mtoto si wakwangu. Pumbavu kabisa nyie wanaume, cheki dental formula ya mtoto mbona ina fanana na yako. Au mtoto kazaliwa na vidole sita kwenye mguu kama wewe, japo sura kafanana na mama yake. Wanaume kwa kupenda kukwepa majukumu yao!

Miaka mingi wazungu wamekuwa na njia za kugundua baba mtoto hasa ni nani. Walikuwa wanapima damu. Lakini siku hizi kuna 'fail proof' njia ya kuhakisha nayo ni DNA Testing. Na kama ulikuwa hutaki kupima utapimwa tu, maana kajinywele kinatosha kupima. Kama uliacha shahawa kwenye shuka inatosha kupimwa hata kama imekauka. Kama ulikuwa unapiga busu na mama mtu na kuacha denda kwenye blausi yake, inatosha kabisa kupata hiyo DNA. Hata kama umegusa mahala unaweza kuacha chembe chembe za ngozi na kupimwa DNA!

Kesi maarufu za DNA ni:

Mtoto wa marehemu Anna Nicole Smith. Wanaume wanne waligombania mtoto wake wa kike, DannieLynn na kudai ni wakwao kwa vile alitembea nao. Huyo mtoto ni bilionea maana anarithi mapesa ya mama yake. Basi, Anna kaolewa na mwanasheria wake, Howard Stern, huko wanaume wengine wanadai oh, mtoto wa kwao. Wote walipimwa DNA. Kumbe baba mtoto ni wa mpiga picha, Larry Birkhead. Duh! Baada ya testi huyo stern alimkabidhi mtoto kwa Birkhead bila ubishi wowote.

Na kwa sasa mcheza sinema Eddie Murphy anapimwa kwa ajaili ya mtoto aliyezaa Spice Girl Melanie Brown. Murphy anaseme mtoto wa Scary Spice si wa kwake, lakini mmh sijui kwa kumtazama tu naweza kusema hakuna haja hata ya kupima mtoto ni wa Murphy. Anywy, hiyo DNA test ndo itamaliza maswali yote.

Prince Harry, mtoto wa marehemu Princess Diana na Prince Charles (?) wa Uingereza. Watu wanadai ni mtoto wa mpambe wa Diana, James Hewitt, maana katembea naye akiwa ameolewa na Prince Charles. Harry mwenyewe anataka DNA test kujua nani baba yake amalize maswali ambayo yamemsumbua miaka mingi.

18 comments:

Anonymous said...

Eti ummempiga demu buus basi mtoto ni wako?Huo ni uhuni.

Anonymous said...

Da Chemi nadhani wale wanaosema watoto si wao siku hizi ni kutokana na tabia chafu za wanawake wao, kwa hiyo nadhani ndio maana wana doubt, lakini kama ni wasafi basi hakuna haja ya kuwa na utata. Pili unajua siku hizi dada Chemi baadhi ya wanawake wanainvest toka kwenye child maintanance(yaani hiyo hela ya matumizi baba atakayo tuma ndiyo hiyo mama atajinunulia makeups na chakula)hata TZ hiyo ipo sana, ooh humtunzi mtoto, halafu hela ikitumwa inatapanywa kwenye familia, it sucks, mi nimeshuhudia mwenyewe, anyways DNA ni technology nzuri na pia ina visebu sebu vyake, haya kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe!!!!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 11:03PM, asante sana kwa mchango wako. Na wala sikataii kuwa kuna wanawake wenye tabia chafu ya kutembea na wanaume wengi. Halafu wanasingizia yule mwenye pesa nyingi ndo baba mtoto. Hilo sikatai nami nimeshuhudia. Lakini nimeshudia wasichana wa shule na wengine wakiachwa kwenye mataa na baba watoto wao.

Hiyo DNA ni komesha. Dawa mwanaume afikirie mara mbili kabla ya kupachika jamaa. Ajiulize hiyo raha ya sekunde ni worth it?
Pia ni kweli kuna wale ambao wanapewa hela ya matumizi lakini hela inaishia kwenye viatu, nguo, na vipodozi. Mtoto anavaa viraka na hata akiumwa hospitali hapelekwi.

tanzanianboy said...

Chemi,

Naona hili suala la kukataa watoto unaliangalia kwa mtazamo mmoja tu tena kupitia miwani ya kike. Nchini kwetu Tanzania naweza kudai kwamba wanawake wengi wamewambakia waume zao (hata mabwana wao wanaotembea nao) watoto kuliko wanaume walivyokataa watoto "wao".

Kwahiyo kwakuwa tumeanza kutumia DNA Testing huko nyumbani nadhani TUWASHAURI pia watu walio ktk familia waende kucheki DNA na watoto wao kujua kama ni wa baba husika au vipi. Nina imani ndoa nyingi zitasambaratika.

Chemi, hivi unajua kwanini wahenga waliibuka na usemi kuwa "kitanda hakizai haramu"? Ni kwasababu hawakuwa na namna ya kujua ukweli wa baba wa mtoto aliezaliwa hivyo wakaleta "usanii" huo ili wanaume wasikatae watoto wao na kwa maana nyingine wadumishe ndoa zao.

Katika nchi kama Tanzania watu wengi wana hakika sana na mama zao kuliko baba zao. Chemi, pamoja na kwamba hoja yako ina feminism ndani yake (hasa kwa jazba na matusi uliyotumia dhidi ya wanaume) lakini ni vizuri kabla hujatukana ukafanya utafiti kidogo (hasa katika mazingira ya kitanzania).

Wanaume wangapi wamebambikiwa watoto ktk familia zao wenyewe (nchini Tanzania) v wanaume wangapi wamekataa watoto wao halali (Tanzania)?

Hivi kwa mfano nina mke halafu najua kabisa kuwa kuna jamaa anatoka nae ingawa ushahidi wa moja kwa moja wa kumuacha mke wangu sina halafu ghafla anapata ujauzito ambao siuelewi, je nikisema mtoto huyo si wangu tayari naingia ktk kundi hilo ulilolitusi hapo juu?

Hata kama ninaamini, beyond doubt, kwamba mke wangu ni mke "wetu" basi nikikataa mtoto ni kosa? Chemi makala zako zikiwa na jamabo linalohusu man v woman basi lazma utamkandamiza mwanaume tu. Kwako wewe wanawake hawana makosa ila wanaume tu. Tena basi unajisahau hadi wachangia mada "wakukumbushe".

Chuki yako dhidi ya wanaume isikufanye ushindwe kutoa mada isiyo na bias dhidi ya wanaume. Sio wanaume wote ni kama afande wako wa JKT! Wengine ni baba zako na kaka zako pia!

Anonymous said...

Tanzaniaboy ametoa hoja nzuri!

Huo msemo wa "kitanda hakizai haramu" nafikiri wakonga wetu walikuwa na "vision" ya kujua kwamba mtoto anahitaji "stability" ya kuwa na baba na mama hata kama sio baba wa kweli.

kama Tanzaniaboy alivyosema, kuna wakati huwezi kujua kama kweli ni wewe ni baba wa mtoto , hasa hasa kwa wale wanaofanaya mapenzi ya chapuchapu-yaani mapenzi yasio ya kudumu.

Mie nafikiri cha maana zaidi ni wale akina baba ambao hawajawakataa watoto wao lakini hawataki kuwatunza kwa sababu wamekorofishana na Mama mtoto-nafikiri hao ndio wa kuwasema. Na hawa wapo wengi tu.

Anonymous said...

Chemi,
Naona mchango wako kwenye issue ya kukataa watoto umelenga kutetea u-Beijing zaidi kuliko haki za mtoto na baba. Kamavile mtoto alivyo na haki ya kukubaliwa na kulelewa na baba yake "HALISI" baba pia ana haki ya kulea mtoto wake "HALALI". Tumebahatika Tanzania sasa hivi pale kwa Mkemia Mkuu wa Serikali wanapima DNA na data from very reliable source zinasema kwamba kwa kila couples 10 za kitanzania zilizowasilisha samples pale baba wanne wanalea watoto ambao sio wao hivyo 40% ya wanawake wa kitanzania wanasingizia watoto kwa wanaume eidha kwa makusudi au kwa kutokujua kwa kuwa "KUFULI" zao hazina funguo kila abishae hodi anaingia. Cha kusikitisha bado hatuna sheria ya DNA Tanzania hivyo bado unaweza ukabambikiwa mtoto na mahakama isitumie majibu ya DNA kama kielelezo. Kazi kwao wanasheria wetu inabidi waende na wakati.........

Anonymous said...

Chemi,
Mada nzuri mara nyingi uwa unaziharibu wewe mwenyewe pale unapokuwa one sided na matusi juu. Ki umri nafikiri unakaribia 40's kama sio zaidi, hivyo ningekushauri arguement zako ziendane na umri. Hii mada uliimalizia vizuri kwa examples nzuri, lakini mwanzoni ilikuwa hewani tu na matusi na maneno ya kiswahili.

Nafikiri ni vyema kwanza ukapitia tafiti ambazo zimefanywa kuhusiana na hii mada, ila tabia yako ya kufanya generalization na wrong conclusion sio nzuri. Ipo mifano mingi mfano hasa tanzania, mwanamke akipata mimba kwanza hajui ni ya nani, anaweza kuwapachika mtu zaidi ya mmoja. Kumbuka kuna wanawake wana wapenzi zaidi ya mmoja, je huyo akipata mimba atajua nani baba wa mtoto.

Mifano ni mingi sanaa kwenye jamii yetu, na huitaji kutumia DNA. Sometimes you neeed to sound as a Tanzanian. Penye ukweli toa credit, si kwa kuwa mimi sipendi wanaume kila kitu unakuwa biased.

Mbona mifano uliyoitoa inapingana na dhana yako ya kukataa watoto?

Remember blog watu wanapenda mijadala, lakini isiwe limited, one sided and closed.

Bora karibisha hoja, na wewe changia kwa mtazamo wako. Najua blog ni yako lakini mijadala inatuhusu wote, na tuna experience tofauti na mitizamo tofauti.

Anonymous said...

mi huwa najiuliza hivi unaanzaje anzaje kutukana? tena public hujui maneno uyatoayo ndiyo kioo cha wewe mwenyewe? hapo miaka 43 ulipokuwa 20's sijui ilikuwaje

Anonymous said...

We annoni unaejiita tanzanian boy, inaonekana kuna experience similar na hii ilikukumba, anywayz point ni kwamba Chemi hakutumia jazba dhidi ya wanaume kama unavyopotray wewe, nimeshaona wanaume wengi wanaotunza watoto wao wa nje, sasa cha msingi ni kuwa %kubwa ya wenye matatizo ya ulezi wa watoto wao ni wanaume na sio wanawake, mpaka mama aje amkatae mwanae labda ana ugonjwa wa ubongo au kuna tatizo kubwa linalomkabili otherwise sio rahisi kabisa, narudia tena sio rahisi kabisa, suala hili mpaka limekuja kuonekana ni issue kubwa ulimwenguni ni kwa sababu wanaoongoza kimahesabu katika kukataa watoto wao ni wanaume!!
Kitanda saa nyingine kinaweza kikazaa haramu kama baba ni looser!
Jaribuni sana kuwa karibu na wake zenu, hustle a lot na kuhakikisha mnawasiliana kwenye mahusiano yenu ili mambo kama haya yasitokee, yakitokea atakayeyazoa ni DNA, good luck!!

Anonymous said...

Kuna njemba flani Dar alimkataa mtoto wakati kila mtu kajua kaetmbea na mama mtoto. Alikataa kabisa. Mtoto kaziliwa sura ya baba, ilibidi amkubali. Sasa hiyo DNA ingekuwepo isingechukua miaka miwili kujua mtoto wa nani.

Anonymous said...

Unaweza kumtia mwanamke mimba kwa mapenzi ya chapuchapu. Pia anaweza kupata mimba hata kma umwaga 'nje'. Askari wanatembea. Ukikataa na baadaye unagundua mtoto ni wako ni aibu kwako.

tanzanianboy said...

Anon wa 5:22 PM,

Mimi situmii "anon",rekebisha. Pili naona kama (mwanzoni) uliacha mpira ukanikanyaga mguu. Vilevile inaelekea hujaisoma makala ya Chemi vizuri (hasa mwanzoni). Hivi mtu akiandika matusi (kama shenzi) sio kagadhibika huyo (ana jazba)?

Kila mtu anajua kuwa mama hawezi kumkataa mtoto (tena basi hiyo wala haikuwa hoja hapa-wewe ndio umeileta) kwasababu za kibaolojia zaidi. Yeye ndie anaebeba ujauzito na mtoto anatoka mwilini mwake kuja "duniani". Sasa itakuwaje akatae kitu alicho na hakika nacho kwamba kimetoka tumboni mwake?

Wanaume (wachache) wanaokataa watoto wanakuwa na sababu zao kama kuogopa/kukwepa majukumu ya ulezi,kulinda ndoa au mahusiano yao (kama mtoto kazaliwa nje ya ndoa au uhusiano unaotambulika rasmi),kuogopa mkondo wa sheria (hasa kama kamzalisha mwanafunzi au mtoto),kukwepa aibu mtaani (labda kama mwanamke husika ana "sifa mbaya",mlemavu,ana "hali duni","sio mzuri" au mdogo kiumri zaidi yake),n.k

Lakini kubwa zaidi liwafanyalo wanaume wakatae watoto ni kutokuwa na uhakika au imani kama hao watoto ni damu zao "halali". Hii inatokana na mashaka kwamba labda "hawakuwa peke yao" au kuna wanaume wengine "walichangia" upatikanaji wa hao watoto. Lakini bado nasisitiza kuwa ktk ndoa nyingi tu Tanzania wababa wengi wanalea watoto "wasio wao" aidha kwa kutokujua (uwezekano mkubwa huu) au kwa kuamua tu "kufumbia macho".

Nina hakika na haya niliyoyaandika ingawa naambiwa "inaonekana kuna experience similar na hii ilikukumba". Watanzania huwa hatuamini mtu anaweza kusema kuleta kitu ambacho hakijamkuta (hatuamini ktk research kabisa) ndio maana ukileta hoja watu watataka kujua uhusika wako na hiyo hoja. Ukimwambia mtu,kwa mfano, kuwa Chad kuna joto sana atataka kujua kama umewahi kufika D'jamenna.

Hii DNA Testing ikianza kutumika mikoani na vijijini itaumbua wanawake wengi sana walio ktk ndoa na hata wanaume wanaowapa mimba wasichana na kuwakataa. Nasubiri tu kuona jinsi ndoa zitakavyosambaratika (ingawa sifurahii hili litokee) na watoto wengi watakavyomiminika kwenda ofisi za vizazi na vifo kubadili "surnames" zao.

Katika nchi kama yetu ambapo watu wengi wana mpenzi zaidi ya mmoja (ndio sababu hata UKIMWI unasambaa sana,HASA miongoni mwa wanandoa) pia kuna uwezekano MKUBWA kwamba mtoto anaezaliwa huenda akawa na baba "zaidi ya mmoja" anaejulikana.

HOJA KWA HOJA.

Anonymous said...

Sometimes kukataa ni muhimu sana na hasa katika mazingira ambayo wana ngono hawana huduma za kupima DNA. Sisi tuna kaka yetu mkubwa ambaye baba alimkataa kata kata. Lakini kwa mambo hayo ya kitanda hakizi haramu akalazimishwa katika familia. Yule bwana hafanani na sisi hata pesa mbili, mkorofi, mwizi, muongo, mlozi na yeye ndo mkubwa kuzaliwa kwa mamaake. Huyu jamaa kila siku analeta matatizo kwenye familia, "anagombea" mirathi hata kama waliochuma mali zao bado hawajafa. watu wakamvumilia mpaka kuna siku wakamwambia kwamba baba yake mzazi alimkataa.

Anonymous said...

We anon ulitoa mfano wa kaka yenu ambae anatabia ya ajabu ambyo haifanani nayie wote--hiyo sio fact--inategemea huko alikolelewa na pia kumbuka ktk gunia hutokea samaki mmoja akaoza. Sisi kwetu tunamdogo wetu kafanana na baba kila kitu lakini jamaa pia tabia yake ni ya ajabu. Mala ya kwanza alikuja home kasubiri kila mtu kaondoka akaiba bike--ambapo sisi kuiba kwetu ni mwiko maana jamaa atauwa. Tabia ni malezi na kawaida watoto waliozaliwa nje malezi yao yanakuwa si sawa na wale wandani kwani baba hayupo kuangalia na kurekebisha hiyo tabia ya mtoto

Anonymous said...

Anony wa 6.39 kama vile unajua:inatosha kumwaga nje, na wakati jamaa unavuta pumzi baada ya shughuli mwanamke kwa kutumia vidole anafunga goli. Hapa hata ulieje wakitumia DNA test hupati kitu hata kama ukisema wallah! there was no penetration!! Historia kama hiyo nimeipata, na hapo mwanamke kafanya makusudi kabisa. Je hapo jamaa ana makosa akimkana mtoto, Chemi?
Chemi sawazisha lugha yako dada, lugha yako haifanani na umri ulionao. na umri wako nadhani umepanda kidogo, nikijilinganisha na mimi kwani wakati ulipokuwa Zanaki Girls mimi nilikuwa jirani Dar Tech.

Anonymous said...

Naona Eddie Murphy amekomeshwa na DNA. Yule mtoto wa Spice Girl ni wake eti 110%. Lakini hata kwa kumtazama utajua mtoto ni wake.

ndolela said...

Anonymous wa 1:43, I dont see anything wrong with Chemi's statement. Its true, men should asks themselves first before having physical relationship with a woman,"starehe ya dakika chache, is it worth it"? Its an important question which most of US dont usually think about.

Anonymous said...

Da Chemi kwa kweli wanaume wakati mwingine huwa wanakataa watoto,simply kwa sababu wanawake si waaminifu,kitendo cha wewe kutolala nae,nikiimaanisha kuwa labda mwaishi makazi tofauti,ukiagana nae ukienda kwako huku nyuma atiwa na mtu mwingine.Nina mfano hai,nilikuwa na girlfriend kwa miaka 2.Nashukuru mungu muda wote nilikuwa natumia zana(condom).Sasa baada ya huo muda nikashangaa mwenzangu baadhi ya vitu alivyovipenda akawa havitaki tena mfano perfume etc.I had a friend doctor nikamueleza,akaniambia ni dalili za pregnancy.Hee mimacho ikanitoka.Anyway,tuyaache hayo kama sio kutumia condom leo siningekuwa nalea mtoto wa mwenzangu?Thats why sometimes men are sceptical..TUSIWALAUMU SANA