Saturday, June 02, 2007

Marudio - Ulafi wa bia Haipendezi Marekani


Orignally Posted: Tuesday, March 28, 2006


*************************************************************************

Ulafi wa Bia Haipendezi Marekani!Hivi majuzi nilienda kwenye ‘Party’ ya waBongo hapa Boston. Party ilifanyika kwenye basement ya nyumba. Na kama kawaida waBongo walijaa. Na kama kawaida chakula kilikuwa kingi na vinywaji tele. Kwa ‘Party’ waBongo ndo wenyewe maana wanachanga bia na chakula bia shida. Huyo anakuja na kesi ya bia, yule anakuja na kesi, yule anakuja na tray ya mapochopocho, mambo swafi kabisa!

Basi kuna MBongo kashuka kwenye ndege juzi juzi, alikuwa kalala kwenye Lawn Chair ndefu anastarehe huko akipunga upepo wa USA. Jamaa kalala kwenye hiyo lawn chair tena bila wasiwasi wowote, huko anaongea na watu. Nikamcheki, jamaa kalegea kabisa na kikofia kichwani anakula maisha ya USA. Basi chini ya hiyo Lawn Chair alikusanya kama chupa kumi za Heineken.

Nikasogea kwa huyo jamaa kumcheki, kama ni mzima au taira au nini, au labda mtu hajiwezi, ndo maana kalala hivyo. Kuongea na jamaa nikakukuta ni mzima kabisa. Basi nikamwuliza sababu ya kulundika mabia chini ya kiti wakati ziko tele jikoni. Na nikamwuliza kama hapendi bia baridi maana kuziweka chini ya kiti zinapata joto. Nikamwambia jamaa kuwa ni mshamba na anajiaibisha.

Jamaa kabisha kasema yeye ana bia tele chini ya kiti atakuwaje mshamba na hawezi kujiaibisha. Hakuwa na habari kabisa kuwa wageni waliokuwepo walikuwa wanamsema chini chini. Lakini jamaa hakujali maana kajiona kafika! Tena kafika USA.

Nadhani watu wangemwona kafika kama hizo bia kununua yeye, na hiyo nyumba ilikuwa yake.

Kwa kweli tabia zingine za Bongo tunaweza kuziacha Bongo. Maana nakumbuka kwenda kwenye shughuli mbalimbali Bongo, na kuona watu wanakusanya bia chini ya kiti. Hiyo kukusanya bia chini ya kiti watu walikuwa wanafanya wakidhania bia zitaisha. At least walikuwa na akiba na rafiki akija wana kitu cha kumpa. Halafu ilikuwa ni sifa kuonyesha kuwa una hela ya kununua bia zote hizo.
Hapa USA karibu kila mahala kuna liquor store na kuna bia tele. Hela yako tu. Na kwenye party za waBongo hata siku moja sijawahi kusikia bia zimeisha, au zikiisha basi watu wanaenda kununua zingine.Jamani eh, tabisa zingine zinafaa ziachwe huko Bongo. Mnasemaje?

18 comments:

Anonymous said...

We mwanamke acha ujinga wako wa kuikandia Bongo. Naamini kabisa kwamb huyo bwana hiyo ni tabia yake ya ulafu, haina cha kulinganisha na ubongo. Maana jamaa zake wa huko wangemshauri kwamba USA maisha yanakwendaje vipi. Wengi tumetembea nje ya TZ naamini kabla hujavamia maisha basi unaskilizia kwanza, othrwise huyo jamaa alikuwa taahira au wewe ni muongo kwa kuandika ujinga wako humu.

FC

Anonymous said...

We anony FC, huyo jamaa alikuwa ni exception.

Anonymous said...

Chemi, you said something that somebody had to say it." Wabongo with Henekeen", it's just like they were starving for this damn thing back in africa.Its just everywhere here in the US, the male-Tanzanians consume this stupid huchie too much. whenever they have a get together even in some funeral activities they misbehave with too much of this booze. Shame on you Tanzanians who forget to make something big out of the richest country in the world and help your poverty stricken country---tz,all the time waste your time on being drunk, godamn it!

Anonymous said...

ina maana bia alianza kuzionea usa?
Chemi nawewe wakati mwingine! kwanza usa yenyewe hata bongo afadhali taabu tupu. bia alificha kwa tabia yake, sio kwa vile yuko USA.

Anonymous said...

Naungana na Anonymous wa kwanza (FC), kama huyo mlevi aliwatia aibu huko USA kwa ulevi wake au tabia yake, that very personal has nothing to do with UBONGO, ina maana hata nyinyi akina Chemi na Watanzania wote ndivyo mlivyo na mitabia yenu ya kuficha bia chini ya viti, wote nyie si wabongo na mlitoka TZ mkiwa mijitu mikubwa kabisa.

ngono said...

duh..... hiyo noma sana!

ngono said...

http://pichazangono.blogspot.com

Anonymous said...

chemi, hiki cheti cha uandishi ulinunua kwenye blackmarket nini, some of the things you write make me wonder,mambo mengine mwachie michuzi. you are bigger than that,tunaingia kwenye blog yako to read something constructive only to be confronted by ulevi,udaku and other nonsense, u doing a good job, but at times you overstep the mark

Anonymous said...

wewe chemi pia unatakiwa ukapimwe akili. Usituandikie hoja za kifalafala humu. Oooh wabongo acheni ushamba, ooh wasio na makaratasi kukiona/kupumua, ulafi wa bia, .... kama huna cha kuandika ni bora kutumia muda wako kufanya mapenzi na unayependana naye kuliko kuja kutapika utumbo huu humu.

Anonymous said...

Kwani wa marekani wenyewe hawanywi? Labda jamaa alitaka ajinywee bila bugudhi ya kuomba ningine kila baada ya bia oja? Hiyo tabia siyo ya watu waliotoka bongo tu.

Anonymous said...

Wabongo kwa bia! Wanavyoitetea. Wabongo kazi kulewa na kutafuta ngono! Yule mwehu aliweka bia chini ya kiti anawakilisha wabongo wote!

Anonymous said...

Da Chemi,
nafikiri hilo ni tukio la watanzania wachache -labda wa huko Boston-sidhani kama kuna haja ya kujadili "isolated cases".

Anonymous said...

Da chemi hivi huwa una matatizo gani? mi nina wasiwasi na shule yako. mambo unayotuandikia hayaendani kabisaaaa!. Wewe ni mtu mzima, unatakiwa uandike vitu vya maana badala ya kutuandikia ukandiaji usio na maana! usijifanye kwa kuwa uko USA basi ndo mwerevu! kwanza huko USA choka mbaya.. Mbona wewe ulipokuwa Dar majuzi juzi ukiongea na waandishi wa habari pale maelezo hatukukandia lile gauni lako ulilokuwa umevaa????

Anonymous said...

We Chemi unajifanya babu kubwa lakini point zero. Watu wanahitaji kuona issues sio udaku. Kwanza smae on you, mwili mkubwa lakini unaandika vitu vya ovyo ovyo. I guess wewe ni journalist, fanya mambo kama fani yako yaani elimisha jamii sio kufanya blog yako bora blog

Unknown said...

Ebu mwacheni Chemi,
Yaani tabia ya kuficha beer chini ya kiti ni nzuri? Mtu anapokwambia kitu kibaya usifanye ina maana anakupenda, isitoshe hakuna anayependa kusikia eti "aah watanzania bwana wakienda party kazi kuficha beer chini ya viti"

Tuwe reasonable jamani kizuri tusifie kibaya tukemee huo ndoo upendo wa kweli!
Waridi

Chemi Che-Mponda said...

waridi, hiyo tabia ya bia hoarding haifai hapa. Kwanza bia zilikuwa nyingi, alivyoweka chini ya kiti zinaanza kupata joto. Hazikwisha. Lakini nadhani watu walichukia zaidi kumwona kajistretch kwenye lawn chair na kufanya tabia hiyo. Yaani ilikuwa uone ndo uamini umeona kweli.

Anonymous said...

bia kama kawaida ila wewe chizi nini basement TX pole danganya waliopo rukwa mwehu wewe TX kuna nyumba ngapi zenye Basement i think u'r not even from TX au ndio hela zenu za HP zinaishi ishia angalia wenzako wako wapi!!! uliza K city team nzima wana kalia kopo 25 federal time mwehu wewe

Anonymous said...

Mimi nilichoelewa watu walichochukia ni Chemi kutumia lugha mbaya kwamba wabongo tuache tabia huko huko nyumbani sidhani ni kauli nzuri inamaana yeye ndugu zake au wazazi wake walioko bongo wanatabia mbaya kwasababu wako bongo.lakini kitendo alichofanya huyo jamaa sio kizuri tuseme kweli ubinafsi ndio ulitawala hapo.nakuomba sana na wewe chemi usipende kukandia bongo kiasi hicho kuna watu wa mataifa ya majirani zetu wanaingia hapa pia