Friday, June 08, 2007

Paris Hilton alie tu!








Binti tajiri na aliyeharibiwa kwa unasa, Paris Hilton, (26)amerudishwa jela huko Los Angeles, California.

Binti huyo anyejiona mrembo kuliko binadamu yeyote duniani na aliyezaliwa katika utajiri wa ukoo wa Hilton (Hilton Hotels), alitoka jela ghalfa siku ya Alhamisi, baada ya kukaa siku mbili tu alisababisha mzozo mkubwa kwenye vyombo vya habari Marekani.

Mchungaji Al Sharpton alisema, "Paris angekuwa ni mtu maskini, au mwanamke mweusi angekuwa bado yuko jela!" Ajabu watu wengi wanaopingana na mawazo ya Sharpton walikubaliana naye. Mweusi au maskini asingeweza kutoka jela Marekani kwa kusingizia atapata kichaa. Lazima pesa zilitembea.

Leo, Paris huko mahakamani kamlilia mama yake kama mtoto mdogo. Kama vile kusema "mama hebu walipe hao wapuuzi waniachie".

Alivyotoka jela Alhamisi ilikuwa amalizie kifungo chake nyumbani kwake. Nyumba enyewe ni ya kifahari kweli kweli. Na ilikuwa avae bangili kwenye mguu kusudi polisi wajue yuko wapi wakati wote. Ilikuwa akae siku 23, lakini hata tau hakufisha, huyooo, nyumbani!

Kisa cha Paris kuonja jela ni hivi, Septemba mwaka jana alikamtwa akiendesha gari amelewa. Alipewa probation ya miezi 36 and fine ya $1,500. Baada ya hapo alikamatwa mara mbili akiendesha gari bila leseni. Alisema eti hakujua kuwa leseni yake imesimamishwa kwa muda.

Jumatatu alivyoenda jela baada ya kwenda kwenye party ya matajiri, wanasema alikataa kula chakula cha jela na alikataa kulala. Haya yeye kazoea kula kweli mahoteli na restaurants za bei mbaya, chakula cha jela hakiwezi kwa sasa. Lakini nasema akishikwa na njaa atakula tu.

Jaji amemrudisha jela leo na atakaa sentensi yake ya awali ya siku 45. Alikuwa amepunguziwa hadi siku 23, lakini baada ya upuuzi huo kutoea jana Jaji kasema apate fundisho. Awe mfano kwa matajiri wengine Marekani, maana inaelekea matajiri wana sheria yao na maskini wana sheria yao!

6 comments:

Anonymous said...

hayo ni matatizo madogo ya kwao, hayatuhusu hata kidogo, bora ungeandika kuhusu kuachiwa kwa ditopile wakati aliuwa kwa kupiga risasi, ama jadili khusu kifungo cha babu seya na wanae!

Unknown said...

she won't even stay inside for long..

Anonymous said...

She will serve ten days at the maximum.

Anonymous said...

Hayo ndiyo ya kujifunza sisi Watanzania, maana mtu kama Ditopile anaua halafu serikali inamsaidia kutoka gerezani. Inatakiwa majaji wawe strong kama huyo jaji wa Marekani. Kazi kweli kweli.

Anonymous said...

hii ndio shida ya chemi ushamba wewe ni mwandishi mzuri lakini ni mshamba fulani hivi mpaka leo hii ujajajua bongo kila mtu ana access na habari unazozitafsiri yaani watu wanazipata hizo hababri kabla hata wewe hujafikiri kutafsiri tena nimeona wewe unamentality fulani hivi kwa kifupi ni mshamba na limbukeni nanai hajui hayo mambo unayotafsiri ndio shida yenu hii mkiwa mnaishi huko nje ktk maisha yenu ya kitumwa

Anonymous said...

Wewe anony wa 6:33AM inaonekana una hasira na maisha, si kila mtu ana access kama unavyozungumzia wewe, pia sisi tunapenda tu kutembelea blog hii ya Chemi just because we can, na si kwamba tunataka kutafsiriwa una jazba, una dhiki na hasira za maisha, hebu jitengeneze kwanza ndio urudi hapa, popo bawa we!!!