Sunday, June 24, 2007

Jamani mbona mmetukana!

Nimepokea hii story kwenye e-mail. Sijui kama ilitokea kweli, lakini naweza kuamini ilitokea. Watu wakianza kutamka lugha ambazo si zao wanatukana bila kujua.

Nilisimuliwa visa hivi viwili:

- Mchungaji wa kutoka kanisa fulani Ulaya, alifika kwenye hoteli fulani Mwanza. Naye alikuwa amejifunza kiswahili kabla ya kutua Bongo. Alipofika Reception akawasalimia wahudumu pale vizuri halafu kasema:

Father Mzungu - Naomba Mchumba

Receptionist - (Kashutuka kweli) Heh! Unasema nini?

Father Mzungu - Nimesema nataka Mchumba

Receptionist - (wakati huo na wafanyakazi na wageni wengine wanamtazama kwa mshangao wakidhani anataka changudoa) Dada mwenyewe kashindwa aseme nini.

Father Mzungu - Ndiyo nina mchumba. Mchumba yupo leo?

Ndo hapo kaingilia mgeni na kumwuliza kwa lugha yake alitaka nini. Kumbe mzungu alitaka chumba cha wanaume.

**********************************************************************

Wajapani wawili walifika pale Embassy Hoteli Dar na kujiandikisha Reception.

Wale wapokezi wakashindwa kutamka majina yao.

Yalikuwa - Mr. Kumamoto na Mr. Takeuchi!

Kumamoto pia ni mji huko Japani. Na wana majina yanayofanana ya Bongo, kama Maeda

*************************************************************************
Na hii nilishuhudia mwenyewe nikiwa mwandhis wa habari Daily News.

WaJapani walitoa msaada sehemu fulani miaka ya tisini. Sasa siku ya kuzindua mradi akaja mtu mzito kutoka wizara iliyohusika na mradi. Alishindwa kutamka jina la mgeni kutoka Japani, naye alikuwa anaitwa Mr. Kumamoto. Yule mzito wa wizarani alimwintroduce kama 'Rafiki yetu kutoka Japani' .

^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^

E-mail enyewe ndo hii:

Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mfadhili (Mzungu) wa mradi wa maji safi huko katika kijiji cha Mkomazi, Mkoani Tanga.

Mfadhili huyu kutoka ubalozi wa nchi moja - Majuu amewahi kujifunza kiswahili kwa muda wa miezi mitatu hivyo kutohitaji kufuatana na mkalimani wa ubalozi.

Alikuwa na hayamachache:

>Mzungu: Jambo wanakijiji wa Mkuma Wazi?

(akimaanisha Mkomazi)

> Watu walibaki kumtumbulia macho na kujikausha wengine

Wakicheka kichini chini. Mzungu akadhani amepatia sana lugha ya kiswahili, akazidi kujitutumua:

Leo mimi na uke yangu (mkewe!)tumekuja hapa Mkuma wazi kukagua

mitombo ya mboo zenu inayoendeshwa kwa nguvu ya pepo

( Mitambo ya mbao inayoendeshwa kwa nguvu ya upepo!)

na Visimi yenu inatoa maji(Visima jamani!).

Mitombo hii ni pesa kidogo na wake yenu haitakuwa na maumivu zaidi kubeba maji.

Watu wakaduwaa kabisa!

Mzungu akaropoka tena:

Mbona watu mko pumbu wazi? (Alikuwa ana maanisha bumbuwazi

lililowapata wanakijiji! Wanakiji wakaanza kuzoza chini chini

hatimaye sauti zikawa za juu wakimuuliza Mzungu kwa nini

amewatusi kiasi hicho.)Mzungu wa watu akazidi kubomoka kiswahili:

Mzungu:

Pepo kubwa inafanya mitombo kufanya kazi bila kulala na visimi yenu

kutoa maji salama na mama wamepata uja zito na watoto yenu wanakuwa salama!


Wanakijiji wazidi kuzoza.


Mzungu:Nasema sikiliza watu wote, Kima, Nyama zenu!!!

Hapa alikuwa akitaka kusema watu wote kaeni kimya, nyamazeni!

Mzungu wa watu baada ya kufanikiwa kuwanyamazisha wananchi

akaendelea kuwaambia kwamba ameridhishwa na hali ya usafi wa visima

ikilinganishwa na siku za nyuma.


Mzungu wetu akaendelea kusema:

Mzungu:

Mimi na uke yangu tumechota maji kutoka visimi yenu na kuyaweka kwenye chupi yetu!

Akimaanisha wamechota maji toka kwenye visima na kuyaweka kwenye chupa.

Akazidi kubonga:

>

Mzungu:

Sasa mimi na uke yangu tutatoa chupi yetu na tutakunya mbele yenu!

lahaula lakwata wanakijiji waanza kuondoka:

Alikuwa anamaanisha kwamba watayamimina maji na kuyanywa mbele yao

ili kuwathibitishia kwamba ni safi na Salama.

Lugha ya watu bwana...

10 comments:

Anonymous said...

Wewe Chemi hukui jamani, mambo gani haya sasa? Hadithi hii mbona ya watoto wa Sekondari au kwakuwa umeweka picha zako za Sekondari zikakukumbusha na hayo.

Anonymous said...

Da Chemi,
Bilashaka hujambo.Pole ya kazi.Mie huwa nakufikilia natamani siku moja nikutane nawe.Nadhani unajua mambo mengi kupitia uzoefu wa umri wako ,fani yako lakini na UTUNDU WAKO.Nakupenda na nakutakia maisha mema.

Chemi Che-Mponda said...

mnyampori,

Sasa unataka ni 'ignore' mambo kama hayo ambayo yanatokea kila siku.

Hizo story inahusu watu wazima.

Anonymous said...

Chemi hizi story za kutaja sehemu nyeti unazipenda sana kwani si mara ya kwanza kuandika hizi story. Unahitaji kukutana na mtaalamu ukafanya ka vitendo na kwa utundu kabisa. Narejea topic yako keywords-- kisimi, mboo, uke, mitombo, nk

Anonymous said...

kisimi, mboo, uke, mitombo si maneno yua kiswahili hayo. Je kufira, kutomba, kinembe?

Anonymous said...

Chemi nimekubali Mama yanatokea kila siku lakini lazima tuwe na kiasi katika mambo yote.Kiasi gani kwako wewe hayo nakuachia maana ni suala binafsi

Anonymous said...

Chemi nakupenda, nakutaka, na nakutamani sana tu!

Anonymous said...

Chemi nimekuvulia kofia,wewe ni kiboko.Niko Juba South sudan tena kwenye ofisi ya heshima ya world bank,ila nilishindwa kujizuia kucheka peke yangu.basi mizungu ikabaki mapumbuwazi ooh samahani wakabaki na bumbuwazi huyu mtanzania kulikoni

Unknown said...

haya bhana

Tumaini Geofrey Temu said...

Na yle aliyema kuchimba kisimi cha maji