Friday, June 22, 2007

Zanaki Girls Secondary School (ZASESCO)


Baada ya Disco 1979 shule ya wasichana ya sekondari Zanaki. Kati ni Mwalimu wetu wa Physics Mr. Tamba, wakati huo alikuwa anasoma Education University of Dar es Salaam ,Fourth year, na kaja kufanya Practicals.

Tuliomzunguka, mbele kabisa mimi, kulia kwangu ni Natujwa Mbagga ambaye siku hizi ni Mama Shilla. Patricia Kassamia, mwenye bun (nimesahau jina), Kulthum, na huyo dada mwingine alikuwa anasoma darasa la Commerce.

Hapa ni baada ya Study Group tukiwa Form Four 1980. Watoto wa Aga Khan nursery walikuwa wamekwenda nyumbani ndo tukavamia playground yao kwa ajili ya kupiga picha.

Mbele kuanzia kushoto - Mimi, Lilian Maganga, Emily Mbagule, Theresia
Nyuma kuanzia kushoto - Dorothy Kihampa, Neema Kingswaga, na (Jina nimesahau)

Hapa ni Darasa la Form Four Science One! Sayansi Wani! (Enzi hiyo top floor kwenye corner) na tulikuwa wanafunzi 25 tu kwenye hiyo darasa. Tulikuwa wasomi kweli, maana mwalimu alikuwa antoa tuition bure, lakini wachache walibakia kuifaidi. Karibu wote walioenda Form Five kutoka Zanaki mwaka huo walitoka darasa letu la Science One.

Mbele, kuanzia kushoto -Demetria Joseph, Lucy Masamba, Rosemary
Nyuma, kuanzia kushoto -Dorothy Kihampa, Batuli, na mimi

Historia fupi - Kabla ya kuwa Zanaki Girls, ilikuwa Aga Khan Girls School. Shule ilitaifishwa baada ya Azimio ya Arusha. Katika hiyo compound kulikuwa na shule ya vidudu (private) na shule ya msingi na Hostel. Nasikia Hostel imerudishwa kwa Aga Khan.

Sketi za bluu. Tulianza kuvaa sketi za bluu nikiwa Form Two. Kabla ya hapo walikuwa wanavaa sketi za kijani. Nakumbuka walifanya kama fashion show asubuhi wakati wa mazoezi na gwaride na hiyo design ya bluu ilichaguliwa.

11 comments:

Anonymous said...

thats my hood chemi,zanaki primary ndipo nilipopata basics za kuface the world,tumeiba sana kuku, na Mwalimu Massasi katuchapa sana viboko, i would give my arm and leg to go back to those sweet days

Chemi Che-Mponda said...

Jack,

Tuliwachinjia na kusafishia walimu kuku sana! Those were the days indeed.

Pale Zanaki primary kulikuwa na mwalimu mwenye roho mbaya sana, mwanamke, ngoja nijaribu kumkumbuka jina. Sijui ndo huyo Mwalimu Masasi!

Simon Kitururu said...

Duh!Bomba la kumbukumbu hili!Lakini umenikumbusha kitu fulani bomba. Nilipitia darasa lililo kuwa na jina Sayansi wani pia.

Anonymous said...

CHEMI, me has been made to understand that KISWAHILI umejifunza ukubwani, is that true au wazushi tu

Anonymous said...

Jack...That's non-issue... The important thing is that she speaks swahili fluently...Big up!!!!!

Anonymous said...

chemi hivi una mdogo wako ambaye anaitwa malaika au ni jina tu la che mponda alikuwa akitumia?nakumbuka tuliwahi kucheza nae tukiwa zanzibar miaka ya 80 na kitu hivi sikumbuki mwaka kamili.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 3:22am, ndiyo Malaika ni mdogo wangu.

Anonymous said...

hi dada chemi ahsante sana kwa kunijibu, nafurahi kusikia kuwa kumbe una undugu na malaika, alikuwa mcheshi sana na tulikuwa tunampenda sana.

Anonymous said...

The picture of you ladies on top of the iron railings brings back memories! I played and played and hurt myself on those very railings. I was in the vidudu class at AgaKhan 1979/1980s. All this time my 35 year old mind was thinking those railings were actually green. The fact that I still remember this, means that the railings had such an impact on my development. Very good memory nonetheless.
Thanks for the nice touch...
--Jaliwa,

Chemi Che-Mponda said...

Jaliwa,

Pole sana. Well actually we never went into that compound but that day I think we asked the mlinzi to let us a take a photo there. I remember at the time Aga Khan vidudu was like an exclusive nursery school. But it wasn't nationalized.

I visited Zanaki Sec a few years back and was sad at the deterioration of the building. I was toldthey didn't even have enough desks for students.

Anonymous said...

EEH wadad mmenikumbusha mabali kani mimi nimesoma zanaki primary mwaka 1979 na nilipo malizza nikaingia secondary hapo hapo zanaki. Tena nilikua dara hili hilo la sayansi. Du! huyo mwalimu mmwenye roho mbaya sidhani kama alikua ni mama masasi maana nakumbuka nilipoanza alikua ndo mwalimu mkuu wangu. Anyway kila shetani na mbuyu wake. All in all my days at Zanaki compound were soooo precious mpaka leo huwa naota niko maeneo hayo.