Tuesday, June 26, 2007

Safari ya Boti



Nimeona hii picha ippmedia.com leo. Caption ilisema kuwa ni wakazi wa Dar es Salaam wakienda kustarehe Bongoyo Island, kwenye boti iiliyotoka pale Slipway Dar.

Picha ni nzuri lakini iliniaacha na maswali. Mbona wazungu tu wamevaa lifejackets? (vifaa vya kuokoa maisha). Bila shaka hizo lifejackets ni zao binafsi. Na mawimbi hayo, duh! Ama kweli watu wameweka maisha ya mikononi mwa malaika. Lifejackets ni muhimu kama unasafiri kwenye boti na kwa bahati mbaya inapinduka au inazama. Maana unaweza kuelea kwenye maji kwa muda hata kama hujui kuogelea. Mara nyingi watu wanazama shauri ya uchovu kama hawajivaa.
Nakumbuka miaka ya nyuma Tanzania, maboti kadhaa yalipinduka na watu walikufa maji shauri ya kutokujua kuogelea na kuzama. Hata boti zilizama Lake Victoria na Lake Nyasa na watu kadha walipoteza maisha yao. Watu wangepona kama wangekuwa wamevaa lifejackets.
Na hata ukipanda kwenye ndege kitu cha kwanza wanakuambia hizo lifejackets ziko wapi kama kwa bahati mbaya ndege inaanguka kwenye maji.

Sidhani kama kuna sheria inayolazimisha hao wenye boti wawe na lifejackets za kutosha kwa ajili ya abiria yao. Na huenda ingekuwa ghali sana kwa hao wenye boti. WaBongo tuna maarifa lakini na hata dumu tupu inaweza kusaidia kuokoa maisha maana inalea kwenye maji.l
Lakini Mungu yupo na atatulinda. Ni kuomba kabla hujaingiwa kwenye boti.

2 comments:

Anonymous said...

Kuna umuhimu sana wa serikali kujitahidi kuanza kueliminisha na kuifahamisha jamii na wananchi katika maswala ya umuhimu wa maisha na hata lishe bora hususan katika mashule yetu.

Kwa sababu ni kisema hivi, watanzania hivi sasa lazima tuendane na wakati na tufahamu umuhimu wa maisha yetu.

Na vile vile itasaidia kubadilisha mentality za wengi tu, kwa mfano ukiangalia hiyo picha hao unaoona wamesimama wanajihisi kama wao mahodari, wanaweza kusimama katika hali ya hatari kama hiyo wakati boti iko kwenye mwendo.

Vile vile unaweza kuiita show off, ambayo ni similar na wale matan boy katika magari ya kupakiza abiria, wanasubiria gari iondoke wao ndio wadandie, na siyo kupanda ndani ya gari kabla gari haijatia moto, yote haya yanaletwa na mentality mbovu, yakutothamini maisha yao na yale abiria wengine katika chombo cha moto.

Kwa hiyo muhimu tuelimishane ili kuondokana na ujinga huu. Ni mategemeo yangu nimeeleweka

By Mchangiaji.

Chemi Che-Mponda said...

Michuzijr,

Je, ni suala ya kutojali au suala ya kuzembea?

Nakubaliana na Mchangiaji kuhusu u-show-off. Sasa hao vijana waliosimama hapo wanaweza kupindua hiyo boti watu wakawmagwa kwenye maji.

Lakini sijui kama kuna mtu ambaye anakumbuka ilivyozama ile meli Bukboba. Baada ya hapo kulikuwa na kampeni ya lifejackets kwa abiria na hata kuweka madumu matupu kusudi waweze kuzimtumia kama meli ikizama.