Tuesday, June 12, 2007

Rais Bush aiibiwa Saa yake Albania!


Kuna habari kuwa Rais Bush ameibiwa saa yake ya mkononi akiwa kwenye ziara Albania. Wanasema kuwa Bush alifurahi sana jinsi wananchi wa walivyokuwa wanamshabikia kiasi kuwa aliamua kwenda kuwasalimia. Hiyo kusalimiana na wananchi haikupangwa. Ndo hapo wajanja wakawai saa yake.
Wengine wanasema hata pete yake ya ndoa ilibiwa pia.

Wanasema saa ilikuwa ya bei mbaya kweli. Lakini bila shaka ilikuwa na inusrance kali kama Lloyds of London.
Serikali ya Marekani inakataa kuwa saa yake iliibiwa. Lakini mbona video haidanganyi? Mara unaona saa mara haipo. Cha kuchekesha msemaji wake, Tony Snow, kasema "Baada ya kutazama video tulithibitisha kuwa saa yake haikuibiwa." Jamani! Kama haikuibiwa kwa nini mlitazama video kuona kama imebiwa?
Kwa habari zaidi someni:

6 comments:

Anonymous said...

Inaonekana Bush alikuwa haijui Albania, amuulize Silvio Barlusconi ampe habari kamili. Waalbania in wezi hakuna mfano kuna utani waitaliano wanasema kuwa kama umeibiwa basi nenda albania utakikuta ulichoibiwa.

Anonymous said...

Chemi
Ile saa haikuibiwa ila Bush aliiondoa mwenyewe baada ya mtu mmoja kuishika (na saa ikawa loose mkononi!?). Bush alishusha mkono wake wa kushoto na kuitoa kwa mkono wa kulia na nadhani walinzi waliichukua au aliiweka mfukoni upande wa kulia!
Ni kweli kuna mtu aliishika saa mkononi kwa Bush na kuiparaza, lakini haikuibiwa. Nina imani saa iko salama.
Nimeangalia leo asubuhi footage ktk 'angles' tofauti na kuthibitisha kuwa aliiondoa yeye mwenyewe Bush!!!

Anonymous said...

Ukitazama picha kutoka angle moja utadhani aliibiwa, lakini ukiangali kutoka angles nyingine utagundua haikuibiwa ila aliitoa yeye mwenyewe.
Saa haikuwa ya bei mbaya. Inasemekana saa ni aina ya TIMEX yenye thamani ya £25 tu, ila ilikuwa na 'presidential seal', na alipewa saa hiyo na rafiki yake anayefanya kazi TIMEX.

Anonymous said...

Hao waalbania si ndo wanaitwa ma GYPSIES! Wanajulikana kama wezi hata marekani

Anonymous said...

Huyu mjinga achana naye, kifo chake kitakuwa kama cha Hitlar. Hata Hitlar aliingia madarakani kwa kuchaguliwa.

Kwa jina la Bush watu waliofariki duniani ni wengi kuliko vita vya Vietnam. Aende Irak na kuwapa mikono waIrak kama alivyofanya Albania endapo yu maarufu.

Anonymous said...

Hajapanda daladala eh ?