Saturday, June 09, 2007

Mkenya yuko jela New Hampshire baada ya kutarisha maisha ya Mtoto!


MKenya Esther Ngari (20)anshsikiliwa na polisi, wa Nashua New Hampshire, kwa dhamana ya $50,000 baada ya kuhatarisha maisha ya mtoto aliyekuwa anamwangalia.
Esther alikuwa ana babysit watoto wadogo wawili, moja alikuwa na miezi 18 and mwenzake alikuwa na miezi sita tu. Hakujuana nao mpaka jana hiyo hiyo.
Sasa huyo mwenye miezi kumi na nane alienda chumbani kwake na kula vidoge vya Esther vya ugonjwa wa kifafa. Wakati huo Esther kalala. Angetoa taarifa mapema kuhusu tukio isingekuwa shida sana. Tatizo ni kuwa Esther alijua kuwa mtoto alimeza vidonge lakini hakusema kitu.
Baba wa watoto alikuja kuchukua wanae. Aliona kuwa mtoto anapata shida kukaa macho na pia alikuwa anashindwa kunyayua kichwa. Walivyofika nyumbani mtoto alianza kutapika ndo kapiga simu 9-11. Mtoto alikuwa hoi kiasi kuwa ilibidi apate MedFlight (ndege) hadi Children's Hospital Boston.

Madakatari wana wasiwasi kuwa huenda, ubongo, ini ,na moyo wa mtoto zimehairibiwa. Anasema kama Esther angesema mapema mtoto asingeugua kiasi hicho.
Polisi wanasema kisheria ilikuwa jukumu la esther kuhakisha kuwa mtoto hawezi kupata hizo dawa.
Kesi itakuwa mahakamani wiki ijayo, lakini kwa sasa vyombo vya habari vimerukia habari hizo. Esther amekuwa nchini Marekani kwa miezi mitano tu. Alikuja kama mwanafunzi. Aliwaambia polisi kuwa aliaacha mfuniko wa chupa ya dawa wazi kwa vile ilikuwa shida kuifungua. Hapa wanatengeneza vifuniko vya dawa, 'childproof' kusudi watoto washindwe kufungua.

Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

Anonymous said...

du!! hii ni kali-nafikiri elimu ndogo na kutojua kumesababisha hili tukio la kusikitisha-lakini mzungu anasema "ignorance is not an excuse".

Sitashangaa kama huyu binti watamtundika mvua kadhaa kule jela kwa kosa la "criminal negligence" au "manslaughter" kama mtoto atakufa.

Fundisho:
mabinti wanaotoka nyumbani kuja kulea watoto inabidi kuelimishwa na waajiri wao kuhusu "safety environment" ya watoto na kwa ujumla.