Nasikia ule ugonjwa wa 'Nairobi Red Eyes' (Conjuncivitis) umeingia tena Tanzania. Huo ugonjwa mbaya kweli maana unasambaa kirahisi sana. Wagonjwa walalamika kuwa ni kama vile kuwa kwenye michanga kwenye macho. Pia macho yanatoa machozi na tongotongo kwa wingi. Waznungu wanaiita 'pink eye'.
Jinsi pekee ya kuepukana nayo ni kunawa mikono kila mara, na usifikiche jicho/macho. Ukishake hands na mtu vijidiudu vinasambaa ukigusa alipogusa mwenye nacho pia unaweza kuambukizwa. Pia usi-share dawa ya macho ya mgonjwa.
Huo ugonjwa ulianza kuitwa Nairobi Red Eyes baada ya kuwa epidemic miaka ya 80. Haikukawia na ugonjwa huo ukaingia Dar es Salaam na kuwa epidemic. Ndo watu wakaanza kuita Nairobi Red Eyes kwa sababu waliona ilianzia Nairobi. Wakati ule maji shida, basi ilikuwa vigumu watu wanawe mikono kila mara, ndo ulikuta kila kona mtu mgonjwa, unamkwepa.
Kaeni Macho!
Kwa habari zaidi someni: http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/06/13/92441.html
3 comments:
Nakumbuka niliupata ugonjwa huu nilivyokuwa nasoma boarding ya wasichana kule Lushoto miaka 15 iliyopita, yaani ugonjwa ulivyosambaa kwa haraka it's unbeliavable, sisi walikuwa wanawatenga wenye nao na wanafunzi wengine, mpaka wapone, dawa yako ni kusafisha macho tu kila siku na kuacha kukuna maana yanawasha kishenzi.
safisha kucha wewe na uache bangi labda uanaweza kusaidiwa watu wengine bwana mnatupotezea muda wa kuwaangalia
We anony wa 3:25 una lako hila, ugonjwa ni ugonuwa tu, sia abjabu wewe una kifafa lakini watu hawakujaji, sasa maana ya hiyo point yako ni nini, kama hamna ya maana ya kuongeo bora mkae kimya, eti acha bangi, huu ugonjywa research wise unajulikana unasababishwa na nini halafu wewe mwenye mabangi yako unajifanya kuto comment, if you have nothing good to say, then you better just your stinking ass mouth up, get a life!!
Post a Comment