Tuesday, June 12, 2007

Marudio - OmbaOmba


Leo nimeona nirudie topiki ya ombaomba hapa Boston. Nikitokea South Station kwenye subway leo asubuhi kuna ombaimba fulani anaitwa Gus, alikasirika na kutupa hela kwenye sidewalk. (Kisa alipewa pennies (senti moja moja). Huyo Gus amekaa pale miaka na miaka zaidi ya miaka 15. Kila siku hakosi, wakati wa Lunch makao yake ni Federal Street. Wikiendi anazunuguka kwenye subway siku nzima, kula kwake ni pale Food Court ya South Station. Hizo pennies alizopewa na huyo mzungu mwanamke zilikuwa anyingi kidogo, basi kazitupa chini kwa hasira. Kazoea noti.

Nashangaa sana. Hao si wanasema wanataka spare change? Lakini ukiwapa na hazitoshi wanatupa chini kama kukutukana. Hao ombaomba wana viwango vyao na kama huna usiwape chochote. Mara nyingi wanakuwa na hela kuliko wewe mfukoni.

****************************************************************
From: December 31, 2005

Hapa Boston kuna ombaomba kibao! Tena wengi ni wazungu. Hao ombaomba wengi wao ni walevi na watumia madawa y kulevya na wenye ugonjwa wa akili. Miaka nenda, miaka rudi, ombaomba ni hao hao!Unapita njiani, unasikia “Spare Change”! Utaona mtu kasimama na kikombe chake anakitikisa. Kuna wengine usipowapa kitu wanakutukana matusi ya nguoni.

Halafu kuna wale wakali wanakufuata mpaka ndani ya ATM. Basi watu kwa uoga wanatoa walichonacho na kuwapa kwa kuhofiwa kupigwa au kuibiwa. Haya, lakini ni lazima niongelee kitu ambacho nimeona, na labda wengine hapa USA mmeona. Kuna ubaguzi katika kile watu wanachotoa kwa ombaomba. Tuseme mtoaji ni mzungu, na ombaomba ni mweusi, basi kama atampa kitu anampa vichenji. Huyo huyo mzungu atatoa noti kwa ombaomba mzungu. Nimeshuhudia mara nyingi tu.

Nimeona ombaomba wa kizungu wakipewa noti za $1, $5, $10 na hata $20! Lakini mweusi atapewa vichenji, kwa nini? Je, ni kwa vile mzungu anajisikia vibaya kuona mzungu mwenzake katika hali hiyo, hivyo ni jitihada ya kumwinua? Je, ni kwa vile anaona kuwa mweusi ni hali ya kawaida kuwa maskini? Sijui kama tutaelewa sababu. Halafu utaona weusi wako tayari kutoa kwa yeyote. Atampa mzungu, atampa mweusi lakini mara nyingi nimeona weusi wakisaidia weusi wenzao kuliko mzungu. Kisa, anajua kuwa yule mzungu anaweza kuishi maisha mazuri akitaka maana Marekani maana bado kuna ubaguzi Marekani.

Lakini nisiseme kuwa wazungu wote ni wabaguzi, maana mwaka juzi kuna ombaomba Cambridge, anaitwa Ramsey, alikuwa amesimama pale Memorial Drive. Basi Mzungu jike tajiri kapita ndani ya gari yake ya fahari na kampa noti ya $100. Ndiyo kampa dola mia moja! Halafu mzungu kamwambia Merry Christmas, maana ilikuwa Christmas Eve. Lakini jambo kama hiyo kutokea ni bahati nasibu.Utaona wazungu wana jaribu kusaidia wazungu wenzao kupata public housing na huduma zingine. Lakini mweusi anaweza kupitwa. Kuna magari ya kuwasaidia zinapita mitaani, lakini hebu cheki, hao ‘volunteers’ wataenda kwa wazungu kwanza halafu mweusi ataambulia kilichobaki.

Ajabu na si kitu cha kushangaza sana ni kuwa hao ombaomba wa kizungu wakienda kuoga, ku-shave, kuchana nywele na kuvaa vizuri, anaweza kupata kazi kabla ya wewe mweusi na digrii zako!Na kama hamniamini ukipita barbarani tazama mwenyewe. Ngoja niishie kwa leo, na kwa maksudi sijaongelea habari ya welfare, na shelters maana hii blogu ingekuwa ndefu mno!

No comments: